Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha juu ya CHADEMA

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,571
Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Kutoka Ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha

Taarifa ya ajali ya moto katika Ofisi za CHADEMA


Ndugu wanahabari,
Mnamo tarehe 03/12/2013 muda wa saa 5:00 asubuhi, polisi mkoani hapa tulipokea taarifa juu ya kuchomwa moto kwa jengo ambalo lina ofisi za chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) zilizopo mtaa wa ngarenaro halmashauri ya jiji la arusha.

mara baada ya taarifa hiyo askari walikwenda katika eneo la tukio na kukuta moto umezimika. Jengo hilo ambalo lina uzio mrefu wa matofali na geti moja la mbele lina ofisi tatu za chama hicho ambazo ni ofisi za wilaya, mkoa na kanda ya kaskazini ambazo zinatumia bafu na choo kimoja.

aidha uchunguzi uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na idara ya zimamoto imegundua mambo yafuatayo:-

kwanza, ofisi hizo zinalindwa na walinzi wa chama hicho "red brigades" na siku ya tukio mlinzi aliyekuwa zamu alikuwa kitumbwizi s/o bahati (42) mkazi wa olasiti ambaye aliingia kazini tarehe 02/12/2013 muda wa saa 12:00 jioni na kutoka tarehe 03/12/2013 muda wa saa 12:00 asubuhi. Aidha ofisi hizo zina katibu muhtasi mmoja aitwaye jenifer d/o mwasha (25) mkazi wa sombetini ambaye uwa anaingia kazini saa 1:30 asubuhi kila siku lakini siku ya tukio aliingia saa 4:00 asubuhi.

pili, uchunguzi umeendelea kubaini kuwa, hakuna mahali palipovunjwa kutoka kwenye uzio wa ofisi hizo kuruhusu mtu/watu kuingia ndani.

tatu, mlango wa nyuma wa ofisi hizo katika veranda kuligundulika tundu katika dari kuelekea bafuni tundu lenye upana wa futi moja na nusu kwa nusu (1[SUP]1[/SUP][SUB]/2[/SUB]x[SUP]1[/SUP][SUB]/2[/SUB]) ambalo ni dogo kiasi cha kutowezesha mtu kupenya kuingia ndani ya ofisi hizo.

nne, ndani ya bafu kulipatikana majivu na kwenye sakafu na juu ya sinki yakiwa makavu bila maji maji yoyote.

tano, kuta zote za bafu na choo hazikuwa zimeungua.

sita, eneo lililoungua kwenye dari ni 3/4 (robo tatu mita) lenye upana wa mita 1 kwa urefu wa mita 3.

saba, eneo ambalo moto ulionekana umewaka, mbao katika dari zilionekana kuungua upande wa chini na upande wa juu wa mbao na ceiling board hazijaungua kuomyesha moto ulianzia chini.

nane, kumepatikana kipande cha chuma kilichokuwa na karatasi zilizoungua pamoja na tochi ndani ya dari eneo ambalo moto ulikuwa ukiwaka lakini vitu hivyo havikuonyesha dalili za kuungua au kushika moto, na inaonyesha vimewekwa baada ya moto kuzimwa.

tisa,
kuna uwezekano mkubwa moto huo ulizimwa kwa kutumia hewa chafu/co[SUB]2.[/SUB]

kufuatia tukio hilo jeshi la polisi bado linaendelea kuwahoji mlinzi wa ofisi hizo kitumbwizi s/o bahati pamoja na katibu muhtasi jenifer d/o mwasha, huku upelelezi zaidi juu ya tukio hilo ukiendelea.

Asanteni kwa kunisikiliza.

imetolewa na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa arusha,

kamishna msaidizi wa polisi (acp) japhet lusingu

tarehe 04/12/2013.
 
Taarifa hii inaleta ujumbe gani hasa? Kwamba CHADEMA wamechoma jengo wenyewe? Kwanini uchunguzi huu umekwenda haraka hivi?

Tupatupa wa Lumumba
 
Kuna mtu kanisimamisha mitaa ya Kijitonyama. Akaniambia "braza najua wewe uko kwenye mambo ya siasa, naomba nikuulize swali".

Nikamwambia kama mambo ya kuhusu Zitto kawaulize Chadema wenyewe.

Akasema sio hivyo.

Nikamwambia uliza.

Akaniuliza "hivi kwanini Chadema Arusha wamechoma ofisi yao?"

Nikamwambia mimi sijui, ila nimesikia wameitisha mkutano wa hadhara. Kwavile mkutano huo walianza kuuandaa kabla ofisi haijaungua na kwavile wamesema mkutano huo unahusu kuungua kwa ofisi, basi tusubiri labda watatangaza sababu ya kuiunguza hiyo ofisi.

Nikamwambia kwanini umeulizia ofisi ya Chadema?

Akasema kwa sababu kama miezi miwili iliyopita alitoa mchango wa kujenga ofisi ya Chadema, sasa anahofia kama ofisi zenyewe baadae Chadema inaziunguza basi pesa yake itapotea bure.

Nikamwambia asihofu, Arusha tatizo ni Lema tu. Otherwise mikoa mingine hakuna mkakati wa kujiunguzia ofisi.

Kama kuna mdau mwenye jibu naomba tumsaidie huyu mwananchi
 
Taarifa hii inaleta ujumbe gani hasa? Kwamba CHADEMA wamechoma jengo wenyewe? Kwanini uchunguzi huu umekwenda haraka hivi?

Tupatupa wa Lumumba

Vuta Nkuvte , Chadema wanatakiwa kupata majibu toka kwa katibu muhtasi na mlinzi kuna connection hapo.Uchunguzi kwenda haraka ni vyema kuondoa sintofahamu kwa jeshi la Polisi .Nakubaliana na Polisi kwa speed yao.
 
Sijaelewa kwanini Lema aliandaa mkutano wa kuzungumzia tukio la ofisi kuungua kabla ofisi yenyewe haijaungua!
 
Hii ofisi ya Arusha atakua ameichoma Zitto na Kitila hii. Na wametumwa na Ccm wachome ofisi!!
 
Vuta Nkuvte , Chadema wanatakiwa kupata majibu toka kwa katibu muhtasi na mlinzi kuna connection hapo.Uchunguzi kwenda haraka ni vyema kuondoa sintofahamu kwa jeshi la Polisi .Nakubaliana na Polisi kwa speed yao.

Katibu muhtasi wa Chadema Arusha ni binti MWASHA.

Huyu huwa kila siku anaingia kazini asubuhi saa moja na nusu, lakini siku ya tukio alifika kazini saa nne!!!

Cc Ritz
 
Last edited by a moderator:
Vuta Nkuvte , Chadema wanatakiwa kupata majibu toka kwa katibu muhtasi na mlinzi kuna connection hapo.Uchunguzi kwenda haraka ni vyema kuondoa sintofahamu kwa jeshi la Polisi .Nakubaliana na Polisi kwa speed yao.

Vipi kuhusu bomu la Kanisani Olasite na Soweto! Uchunguzi bado?
 
Mbona hatujaona polisi wakitoa taarifa kama hizi haraka namna katika matukio makubwa kama ya Ulimboka, Kibanda, mabomum kanisani na kwenye mkutano wa chadema na sehemu nyingine nyingi kulikotokea madhara makubwa kama lile la Mwangosi.
 
Baada ya magamba kushindwa kuhujumu chama kwa njia za kuwatumia mamluki, naona sasa wameamua kuchoma moto ofisi za CHADEMA (plan B). Na jinsi Mungu alivyo mkubwa ameyaumbua magamba mchana kweupe--moto umezimwa na maisha yanaendelea. Pole zenu magamba, wabakaji na majangili wakubwa!
 
Polisi wameendeleza gemu lile lile la kisiasa, taarifa zinazohusu chadema wanatoa kirahisi, kwamba chadema wamejichoma wenyewe, kama walivyosema kwenye bomu la soweto chadema walijilipua wenyewe.
Chakushangaza zaidi mpaka leo Polisi hawajatoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya mwanamke aliyetaka kumpiga risasi askari polisi aliyekuwa analinda CRDB Mapato
 
Sasa kama uchunguzi unaendelea hii taarifa ya haraka haraka ni ya nini? Policcm hawaaminiki hata kidogo.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom