Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
KANDA YA MAGHARIBI (TABORA, KIGOMA NA KATAVI)
---------------------------------------------------------------
[HASHTAG]#Tarehe[/HASHTAG]: 29/01/2017.
[HASHTAG]#Utangulizi[/HASHTAG].
Ndugu waandishi wa habari, awali ya yote Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tunapenda kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayo fanya kuhakikisha wanachi wanapata taarifa ya kile kinachoendelea nchini licha ya serikali kuliweka taifa ili katika giza nene ili wanachi wasijue yale yanayofanywa na viongozi wao walio wachagua.
Aidha tunawapa pole sana waandishi wa habari kwa kukosa fulsa ya moja kwa moja kupata Habari zinazoendelea Nchini kutokana na sheria ngumu uliyopitishwa na Bunge yenye ukandamizaji mkubwa hususani katika mamlaka ya kutoa habari, hii ni ukiukwaji wa haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari na hvyo sote tunapaswa kupaza sauti zetu kulitetea hili.
UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO WA MADIWANI.
Ndugu waandishi wa habari, itakumbukwa kuwa Mwaka jana tume ya uchaguzi ilitangaza uchaguzi wa marudio ngazi ya udiwani na ubunge kwa maeneo yaliyo wazi kutokana na sababu mbalimbali.
Ndani ya kanda ya magharibi, nasi tulikuwa na uchaguzi wa marudio katika mkoa wa Katavi wilaya ya Mlele halmashauri ya Mpimbwe kata ya Kasansa. Katika uchaguzi ambao umefanyika tarehe 22/01/2017 kama chama nasi tulisimamisha mgombea katika kinyang’anyilo hicho.
Ikumbukwe kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka Octoba 2015 Kata ya Kasansa ilikuwa na jumla ya wapiga kura 4162, watu waliopiga kura ni 2601 ambao ni sawa na asilimia 62.5%. kura halali zilikuwa 2582 sawa na asilimia 99.3% na kura zilizo kataliwa ni 19 sawa na asilimia 0.7%. katika uchaguzi huo CHADEMA TULIPATA KURA 1088 sawa na asilimia 42% na CCM WALIPATA KURA 1494 sawa na asilimia 58%.
Katika Kata hiyohiyo uchaguzi wa marudio CHADEMA tulisimamisha Mgombea anayejulikana kwa jina la EMANUEL PAUL MALIMA ambaye ndiye aliyegombea uchaguzi wa mwaka 2015. Katika uchaguzi huu wapigakura walikuwa 4162 na waliopiga kura walikuwa 1870 sawa na asilimia 45%. Kura halali zilikuwa 1831 sawa na asilimia 98% na kura zilizokataliwa ni 39 sawana asilimia 2.1%. katika uchaguzi huo CHADEMA TULIPATA KURA 883 sawa na asilimia 48.2% na CCM WALIPATA KURA 948 sawa na asilimia 51.8%.
TATHMINI YA CHAGUZI ZOTE KWA MATOKEO YA 2015 NA 2017
Kwa kuangalia matokeo hayo utagundua kuwa mwaka 2015 CCM ilishinda kwa tofauti yakura 406 ambayo ni sawa na asilimia 15.7% lakini mwaka 2017 januari CCM imeshinda kwa kura 65 sawa na asilimia 3.5%. Hii inaashiria kuwa CCM imeshuka kwa asilimia 12.2% na CHADEMA imepanda kwa asilimia 6.2% kutokana na kiwango cha ushindi mwaka 2015 na 2017.
Aidha mwaka 2015 CCm ilishinda kwa asilimia 58% lakini mwaka 2017 CCM imeshinda kwa asilimia 51% na CHADEMA mwaka 2015 ilipata asilimia 42% na mwaka 2017 ilipata asilmia 48.2%. hii inaashiria kuwa CCM imeshuka kwa asilimia 7% na CHADEMA kupanda kwa asilimia 6.2% kwa uchaguzi wa mwaka 2017.
CHADEMA KANDA YA MAGHARIBI TUNAPINGA PROPAGANDA ZA CCM ZA UPOTOSHAJI JUU YA MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO.
Tulimsikia Kiongozi wa Itikadi na uenezi Taifa wa CCM anaefahamika kwa jina Hamphrey Pole*2 akisema wameshinda kata nyingi dhidi ya Vyama vya Upinzani hii ikiashiria yakuwa chama ccm bado kinapendwa na kinaaminika na wananchi kitu ambacho si kweli kutokana kuficha ukweli katika mambo mbalimbali ambao ni pamoja na:-
1. Ameshindwa kulinganisha Takwimu za Matokeo kwa nyakati zote mbili na kujionea kama ameshuka, amepanda au la!.
2. Anashindwa kusema ukweli yakuwa pamoja na Kuzuia wananchi haki za kikatiba za kupata habari ambazo wamefungia, haki za vyama vya siasa kufanya mikutano ambazo hupelekea wananchi kupata elimu ya uraia wamezuia lakini bado tumewazidi.
3. Ameshindwa kusema ukweli kuwa wameshinda kwa kutumia Rushwa ambazo walikuwa wanagawa waziwazi hadi ccm kwa ccm wanafikia kupigana kusababisha wengine kwenda hadi hospitali kushonwa nyuzi.
4. Ameshindwa kusema ukweli yakuwa wanategemea kusaidiwa na viongozi wa kiserikali(wasimamizi), vyombo vya ulinzi na usalama (Polisi) ambao wote wanapewa oda kuangalia maslahi ya ccm.
5. Maeneo mengine mtaji mkubwa imekuwa kununua watu wetu na kuleta kura feki kupitia vyanzo vya uzalishaji na usimamizi wa kura.
6. Lingine TUME ya Uchaguzi ni ya wana CCM, Wasimamizi wote wanateuliwa na nani Je Kuna usawa hapa?
Hata yeye mwenyewe (huyu Pole*2) akiwa kwenye Bunge la katiba aliwahi yasema haya yakuwa “Kama uchaguzi ukiwa huru na haki basi CCM ikijiandae kutoka madarakani” Msingi wa Hoja zake zote ilikuwa ni hizo hapo juu.
Ila ccm waendelee kutambua yakuwa watanzania wa leo hawapo kwenye propaganda, si wajinga na si wale wa Jana, watanzania wanaendelea kuungana na kushikamana nasi CHADEMA na UKAWA kwa ujumla kwa kuwa CCM ni chama ambacho kimeendelea kuwa Janga Kuu nchini katika kushindwa kuleta Maendeleo Stahiki, Amani, Upendo na Mshikamano.
[HASHTAG]#Hitimisho[/HASHTAG]:-
Nawashukuru wanahabari na wananchi wote kwa kuitikia wito wa kuja kutusikiliza, Nawashukuru watanzania kwa kuwa wanajua kuchuja mambo na wanaendelea kushikamana hata katika kipindi hiki kigumu.
Nawaombea kwa Mungu Wanzania wote wakawe na mwaka mzuri mwenye neema pamoja na magumu wanayoyapitia.
Viva Watanzania, Viva CHADEMA, Viva Kanda ya Magharibi.
General Reuben Kaduma,
Katibu CHADEMA-Kanda ya Magharibi.