Taarifa kwa vyombo vya habari kufafanua kuhusu miradi ya utafutaji na uvunaji wa gesi

Ushahidi wa yanayotokea hapa hapa nchini na nchi nyingine za Africa zenye rasilimali nyingi unaonyesha kwamba wananchi wa kawaida hawafaidi rasilimali zilizo kwenye maeneo yao bali ni viongozi na mabwana zao wa nje. Ni lazima wananchi kuanzia Mtwara hadi kona zote za nchi hii kusimama kidete kuhakikisha kuwa hatuburuzwi na viongozi wetu tena. Wananchi wa Mtwara wana haki ya kuelezwa kiwango cha mapato ya gesi kitakachorudishwa mkoani kwao ili kuinua hali ya maisha yao ambayo kwa kiwango cha TZ ni duni sana. Liwalo na liwe, wananchi wa Mtwara hakuna kulala mpaka kieleweke
 
"hata walipa kodi hawajaandamana" hii inamaanisha kuwa watu wa lindi na mtwara hawalipi kodi!!!!!??????na vipi kuhusu korosho???

Ushahidi wa yanayotokea hapa hapa nchini na nchi nyingine za Africa zenye rasilimali nyingi unaonyesha kwamba wananchi wa kawaida hawafaidi rasilimali zilizo kwenye maeneo yao bali ni viongozi na mabwana zao wa nje. Ni lazima wananchi kuanzia Mtwara hadi kona zote za nchi hii kusimama kidete kuhakikisha kuwa hatuburuzwi na viongozi wetu tena. Wananchi wa Mtwara wana haki ya kuelezwa kiwango cha mapato ya gesi kitakachorudishwa mkoani kwao ili kuinua hali ya maisha yao ambayo kwa kiwango cha TZ ni duni sana. Liwalo na liwe, wananchi wa Mtwara hakuna kulala mpaka kieleweke
 
Mwizi hawezi kuacha kuiba wakati anaiba; mpaka akamatwe. Na hutamkuta mwizi anayekubali kuwa alikuwa anaiba hata ukimkuta na kitu mkononi. Kwenye stendi ya Tanga (kati ya Barabara ya 11 na 12 kibaka mmoja alijaribu kumchomolea mjomba wangu hela; mjomba (alikuwa mjeshi) alimkamata kidole kabla hakijachomolea na kumuuliza. "Unatafuta nini kwenye mfuko wangu"; jamaa bila hata kufikiria sana alisema "kifungo changu cha shati kilitumbukia kwenye mfuko wako"!....

Mjomba alivunja kidole cha jamaa...kama matokeo ya makubaliano ya kutoitiwa mwizi!
 
.........

Mjomba alivunja kidole cha jamaa...kama matokeo ya makubaliano ya kutoitiwa mwizi!

Nina imani mfano wako huu unalenga mada iliyoko mezani.

Kwa tafsiri yangu ya haraka ya mfano wako. Je. Unashauri tuvunje Kidole cha serikali kwa kushinikiza Prof. Muhongo ajiuzuru na kusitisha kabisa huu mradi wa gesi kutoka Mtwara mpaka mswada unaoandaliwa wa gesi upitishwe bungeni, au tuiitie mwizi serikali kwa kuanzisha "Watanzania Wazalendo Spring" ambayo itaiindoa serikali ya sasa madarakani kabla ya 2015 kutokana masuala mengi baadhi ya watendaji wake wanafanya ya kifisadi?
 
Watu wa mtwara wameonyesha njia watanzania wote tuwaunge mkono.
Kwa hili ninawaunga mkono kwa hali na mali wakazi wa Mtwara.

Gesi inayochimbwa Mtwara ni lazima ianze kuwafaidisha kwanza wakazi wa Mtwara.
Kwanini keki ya taifa itafunwe Dar pekee yake?
 
Huyu kiongozi alianza kutuambia Mtwara kuna gesi kidogo sana kuliko iliyopo Dar, sasa kwanini wasiisafirishe hiyo ya Dar ikawanufaishe watanzania wenzetu wa Mtwara? Hayo madini yamewasaidia vipi wakazi toka wilaya/mikoa yenye hiyo migodi? Kilasiku tunasikia malalamiko ya kufikuzwa wakazi katika maeneo yenye madini, na hata wale wachimbaji wadogo wamefukuzwa kwenye maeneo mazuri na hata wengine kufukiwa ardhini. Hiyo Tanzanite inayopatikana Tanzania tu, inashangaza kuona inawafaidisha wakenya ama South Afrika zaidi kuliko sisi.

Tunasikitika sana kuona Prof. Dr. Sospeter Muhongo anayeheshimika kwenye taaluma yake sasa anatumika kisiasa na kuingia kwenye mtego wakupika propaganda ili kuficha maovu ya watu. Profesa unaharibu image ya wasomo nchini, unataka kutuaminisha kuwa wanamtwara madai yao hayakuwa na msingi na kutaka kuwatenganisha na wapinzani hata kwenye ukweli. Tunavyofahamu vyama vya upinzani viliwafumbua macho na kujua njia sahihi ya kufikisha kilio chao kwa watawala wa kimabavu. Hivi hiyo mifano yako kunainayowakilisha madai ya msingi kwa wana Mtwara?
TAFADHALI SOMA HAPA: Kufuatana na Sheria za nchi yetu zinazotumiwa kugawa mipaka ya mikoa iliyopo kando kando mwa bahari (isivuke 12 nautical miles au 22.22 km kuingia baharini), Gesi Asilia iliyogunduliwa hadi sasa katika Mkoa wa Mtwara pekee ni asilimia 14 tu ya gesi yote iliyogundulika nchini. Kwa kutumia kigezo hicho cha Sheria za mipaka ya ki-utawala ya mikoa yetu, Lindi inayo 7% ya gesi yote, Pwani 1% na huku Kina Kirefu cha Bahari (Deep Sea) ndicho chenye gesi nyingi (78%) kuliko mikoa yote ikiwekwa pamoja! Kwa hiyo, hakukuwa na haja ya kufanya maandamano kwa sababu Gesi Asilia nyingi inapatikana kwenye bahari ya kina kirefu ambayo iko ndani ya mipaka ya nchi yetu bila kujali mipaka ya mikoa yetu. Isitoshe Gesi Asilia imegundiliwa kwenye miamba tabaka (sedimentary rocks) yenye umri wa Miaka kati ya Milioni 199.6 hadi 23.03. Mipaka ya Bara la Afrika, ya nchi yetu na ile ya mikoa yetu haikuwepo wakati huo!
 
Watu wa mtwara wameonyesha njia watanzania wote tuwaunge mkono.
Kwa hili ninawaunga mkono kwa hali na mali wakazi wa Mtwara.

Gesi inayochimbwa Mtwara ni lazima ianze kuwafaidisha kwanza wakazi wa Mtwara.
Kwanini keki ya taifa itafunwe Dar pekee yake?

Basi Kama Ni hivyo hata dagaa wanaotoka Ziwa Victoria waanze kuwanufaisha kwanza wakazi wa ukanda huo. Ni aibu wakati wa karne ya 21 na mfumo wa kidigitali kuanza kuongea mambo kianalogia
 
Watu wa mtwara wameonyesha njia watanzania wote tuwaunge mkono.
Kwa hili ninawaunga mkono kwa hali na mali wakazi wa Mtwara.

Gesi inayochimbwa Mtwara ni lazima ianze kuwafaidisha kwanza wakazi wa Mtwara.
Kwanini keki ya taifa itafunwe Dar pekee yake?
TAFADHALI SOMA HAPA: Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia pia unaendelea tukiwa wa mategemeo makubwa ya upatikanaji wa raslimali hizi katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Kigoma, Mbeya, Njombe, Rukwa, Katavi, Morogoro na Tabora pamoja na kwenye kina kirefu cha maji baharini kuanzia mpaka wetu na Msumbiji hadi mpaka wetu na Kenya. Hatutarajii mikoa hii nayo ifanye maandamano ya kutaka kuhodhi raslimali za Gesi Asilia na Mafuta zitakapogunduliwa mikoani mwao.
 
mimi naona kuna watu especially viongozi kama muhongo wanataka potosha umma. ukifatilia sakata la Mtwara utaona kuwa wana Mtwara siowamekataza gesi la hasha bali wanataka viwanda vya kusafishia hiyo gesi pamoja na mitambo ya umeme ijengwe Mtwara then hiyo gesi isafirishwe ikiwa tayari imeshakuwa purified na sio crude. kwa nini usafirishe crude umbali mrefu kiasi hicho wakati unaweza jenga mitambo palepale ambayo itawapatia ajira wakazi wa eneo husika. leo hii kama tunavyoona wala sio kwa kusimuliwa kila project ni Dar,dar kuna nini hivi maeneo mengine sio tanzania? huo ubaguzi serikali inaufanya yenyewe then inakuja na stupid idea eti wana-Mtwara wabaguzi sio kweli kabisa sana sana tunajua serikali inaweweseka kwa sababu watu walishaanza kula hela za project ya hilo bomba so mimi sio mwana mtwara but naunga 100% mawazo ya wanamtwara. kama mtakumbuka kuna chama flani kilikujaga na sera za majimbo nadhani watu walibeza sana wakasema ooh mikoa ya kusini itapata shida sasa nadhani tumejionea wenyewe kuwa zile zilikuwa porojo za serikali hii dhalimu kwa kujua kua mradi wao wa kukusanya kila kitu kotka mikoa yote na kuvirundika dar ungeyeyuka na hilo linaonekana sasa. viva wana Mtwara hadi mkoloni mweusi huyu asiliti amri
 
Kusema kweli napata taabu kama kweli taarifa hii imeandaliwa au kupitiwa na mtu anayeitwa Prof.
Kama ndiyo. Kweli huko mbeleni Nchi hii lazima damu itamwagika.

Nimeisoma mara tatu sijaona mahali Waziri amejenga hoja ya maana zaidi ya kulalamika na kugeuza madai ya Wana-Mtwara kuwa suala la Kisiasa.

Huku nikufilisika kimtazamo au Kuna Masilahi binafisi katika zoezi zima la kusafirisha Gesi na mahali itakapokwenda kuhifadhiwa na kufanyiwa Uzalishaji.

Ningeliona Thamani ya U-prof.

1.Kama Waziri angeleta hoja ya kwanini Kiuchumi kuna faida kubwa kusafirisha Mali ghafi Dar es salaam (gesi isiyosafishwa) Kuliko Gesi iliyosafishwa au Kujenga Mitambo ya Umeme Mtwara na Kusafirisha Umeme Dare es Salaam.
2. Angeleta ufananuzi tu wa namna gani Wana Mtwara wanafaidika na mradi huu kuliko kejeli ya eti wamekuwa wakiishi kwa fadhila za mikoa mingine toka tupate Uhuru!

Ila na imani bado ana Nafasi ya kujirudi na kwa kufanya hivyo anatakiwa atuletee takwimu na Upembuzi yakinifu uliofanywa na Wizara yake katika kufikia hitimisho la kuwa Gesi Ghafi isafirishwa na kusafishwa Dar es Salaam na Si kuisafisha Mtwara na Kusafirisha Gesi au kuzalisha Umeme Mtwara na kuusafirishwa Dar es Salaam
(COST ANALYSIS)
na sio hizi hoja mfu ambazo si madai ya WanaMtwara !



Tusikubali kuvunja nchi yetu vipande vipade kwa kisingizio cha raslimali zilizopo mikoani mwetu.
Tusikubali kuvunjavunja mikoa yetu kwa kisingizio cha raslimali zilipo kwenye wilaya zetu.
Tusikubali kuvunjavunja wilaya zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye tarafa zetu.
Tusikubali kuvunjavunja tarafa zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye kata zetu. Tusikubali kuvunjavunja kata zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye vijiji vyetu na mitaa yetu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, DUMISHA UHURU NA UMOJA WETU

Prof Dr Sospeter Muhongo (Mb)
WAZIRI WNISHATI NA MADINI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
 
Watu wa mtwara wameonyesha njia watanzania wote tuwaunge mkono.
Kwa hili ninawaunga mkono kwa hali na mali wakazi wa Mtwara.

Gesi inayochimbwa Mtwara ni lazima ianze kuwafaidisha kwanza wakazi wa Mtwara.
Kwanini keki ya taifa itafunwe Dar pekee yake?

UBINAFSI HUO.. raslimali zilizopo nchini ikiwemo gesi asilia, madini,makaa ya mawe, wanyama pori, misitu, milima ya utalii, mito, maziwa, bahari n.k ni za Wa-Tanzania wote kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Raslimali hizi zinapatikana, zinatunzwa na kuzalishwa maeneo mbalimbali nchini mwetu na mapato yake yanatumika kwa maendeleo ya Wa-Tanzania
wote bila kujali maeneo raslimali hizo zilipo. WANAMTWARA mmetuonesha your true colours!
 
Unaweza kuita Siasa ni ugonjwa mbaya sana Kuliko Malaria.Watanzania na wana Mtwara wanataka kufahamishwa na kuhakikishiwa watafaidika vipi na Mradi huu ambao kwa namna moja au nyingine utawaletea Uharibifu wa Mazingira na mambo mengine ya Kiuchumi na Kijamii. Lakini Ufanunuzi wa Waziri ulitakiwa kukita katika kuwapa matumaini watu wa Mtwara na Kueleza sababu za kiuchumi za kwanini Gesi Ghafi isafirishwa mpaka Dar kama baadhi ya maandiko yanavyoeleza mlinganyo ulivyo katika Gharama kati ya kusafirisha malighafi gesi badala ya kusafirisha Umeme au zao litokanalo na Gesi ghafi.
Natural Gas and Electricity Transmission Lower costs of energy transmission A specific advantage of gas transmission compared to electricity transmission is that for gas in growth markets much larger economies of scale can be realised than for power transmission and thus much lower costs per kwh. For electricity, a maximum scale of 2-3 GW is technically achievable, after which multiple (parallel) lines are required*. However, gas pipelines have a capacity between 10 and 25 GW. Gas transportation for electricity generation can be combined with gas for other consumers in other market segments, leading to substantial economic advantages. Lower costs of energy transmission with economies of scale Overhead power transmission Capital costs:
C:\DOCUME~1\HR\LOCALS~1\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif
at least 2-3 x more expensive per unit of energy than gas pipelines sized for high volume transmission
C:\DOCUME~1\HR\LOCALS~1\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif
only in the case a gas pipeline is laid only to transmit gas for power generation, as may be the case in an emerging market, the capital costs are of the same order of magnitude Underground power transmission
C:\DOCUME~1\HR\LOCALS~1\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif
Capital costs: at least 10-15 x more expensive per unit of energy than gas pipelinesized for high volume transmission
C:\DOCUME~1\HR\LOCALS~1\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif
Lower losses from energy transmission
C:\DOCUME~1\HR\LOCALS~1\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif
Losses pipelines: 0.2-0.4% per 100 km
C:\DOCUME~1\HR\LOCALS~1\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.gif
Losses (AC): 2-4% per 100 km
C:%5CDOCUME%7E1%5CHR%5CLOCALS%7E1%5CTemp%5Cmsohtmlclip1%5C01%5Cclip_image001.gif
Losses (DC): 0.2-0.4% per 100 km plus 1% one-off conversion loss www.igu.org/gas-advocacy/2012-Mar_Natural-Gas-Facts.../file
 

Attachments

  • 2012-Mar_Natural-Gas-Facts-Figures.ppt
    9.4 MB · Views: 95
Watanzania wanakumbushwa kuwa raslimali zilizopo nchini ikiwemo gesi asilia, madini, makaa ya mawe, wanyama pori, misitu, milima ya utalii, mito, maziwa, bahari n.k ni za Wa-Tanzania wote kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Raslimali hizi zinapatikana, zinatunzwa na kuzalishwa maeneo mbalimbali nchini mwetu na mapato yake yanatumika kwa maendeleo ya Wa-Tanzania wote bila kujali maeneo raslimali hizo zilipo. Tusikubali kuvunja nchi yetu vipande vipade kwa kisingizio cha raslimali zilizopo mikoani mwetu.
Tusikubali kuvunjavunja mikoa yetu kwa kisingizio cha raslimali zilipo kwenye wilaya zetu.
Tusikubali kuvunjavunja wilaya zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye tarafa zetu.
Tusikubali kuvunjavunja tarafa zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye kata zetu. Tusikubali kuvunjavunja kata zetu kwa kisingizio cha raslimali zilizopo kwenye vijiji vyetu na mitaa yetu.
Rangi nyekundu wanaofaidika ni mafisadi wa CCM na siyo watanzania..
Rangi ya kijani, CCMmnataka kupotosha hoja ya wana mtwara waambieni watanufaka vipiwasije kuwa kama wasukuma waliobakiwa na mashimo tu huku Mafisadi waki tunisha akaunti zao huko nje za nchi..

Mtwara komaeni, sisi wasukuma tuna waunga mkono sisi walianza kutukamua kabla hatuja amka...
 
Basi Kama Ni hivyo hata dagaa wanaotoka Ziwa Victoria waanze kuwanufaisha kwanza wakazi wa ukanda huo. Ni aibu wakati wa karne ya 21 na mfumo wa kidigitali kuanza kuongea mambo kianalogia
Kwani haiwezekani, mbona mazao naona wanafanya hivyo kutoa ngunia la mkaa, mahindi kuna sehemu una kuta wanatoza kiasicha pesa...
 
Binafsi nimekua nikifuatilia hili sakata la gesi nimejikuta njiapanda sijajua nani yuko sahihi kati ya WanaMtwara na Serikali.

Nimegundua kuna vitu hapa zinakinzana;
1. Watu
2. Ardhi
3. Viongozi
4. Siasa
5. Maendeleo
Likanijia wazo la kukumbuka maneno ya Mwl. J.K. Nyerere "ili nchi yetu ipate maendeleo tunahitaji vitu muhimu vinne Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi bora"

Watu wapo, Ardhi tunayo. Kiini cha vurugu nyingi sasahivi ni kukosekana kwa Siasa safi na Uongozi bora.

Viongozi wetu wanatoa kauli za vitisho na kejeli badala ya kutoa muongozo sahihi wa nini kifanyike. Badala ya kwenda kukaa na wanamtwara wakajadiliana na kuelimishana kwa faida ya Taifa zima, na wao wameingia kwenye vijembe kama nyimbo za taarabu.

Siamini kwamba wanamtwara hawataki gesi itoke au itumike mtwara kwanza isipokua hajaelimishwa kitaalam wakaelewa na isitoshe hata hao viongozi watakaenda kuelimisha wana makovu kibao ya tamaa na uroho kiasi kwamba imani haipo. Pia kufanya maamuzi kwa usiri na mtazamo wa serikali pasipo kuwashirikisha wananchi na kuwaeleza malengo ya serikali hilo nalo ni tatizo.

Au suala la gesi nalo liko mahakamani halipaswi kuzungumzwa?? au ni taarifa za kiinterejensia??? Viongozi wetu wanajitazama wao zaidi na ndio hapo mtafaruku unapoanzia.

Inakera sana hii serikali yetu na maamuzi yao jamani. Ona sasahivi wananchi wanavyohangaika na hivyo ving'amuzi haieleweki kipi ndio kipi na yupi ndio mkweli, full kuchanganyana je tukisema ni dili la viongozi na startimes watasema majungu???
 
Huwa napata wakat mgumu kutafakar juu ya taarfa kama hizi cjajua ni usomi wake(prof) au siasa ndo inamharibu? Korosho c inapatkanaMtwara
 
Back
Top Bottom