Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari - Kongamano la Wanataaluma Ijumaa 18-12-09 Golden Tulip | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari - Kongamano la Wanataaluma Ijumaa 18-12-09 Golden Tulip

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Sanctus Mtsimbe, Dec 16, 2009.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Dec 16, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
  Kongamano la Kwanza la Wanataaluma Waishio Ndani na Nje ya Nchi 2009
  Mada Kuu: Wanataaluma Na Vipaumbele Vya Taifa na Jinsi Wanavyoweza Kuchangia na Kuchochea Maendeleo ya Nchi na ya Watanzania  Mtandao Wa Wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network – TPN ) ukishirikiana na Tume ya Sayansi na Technolojia (Commission for Science and Technology Tanzania – COSTECH); Open University of Tanzania; University of Dar Es Salaam; na Serikali imeandaa Kongamano la Siku Moja (Nyumbani Ni Nyumbani 2009) siku ya Ijumaa; 18th December 2009 kuanzia Saa 2.00 Asubuhi -11.00 Jioni litakalofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel Toure Drive, Masaki.
  Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano hili atakuwa Mheshimiwa Bernard Kamillius Membe (Mbunge), Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pamoja na mambo mengine Serikali itaongelea juu ya suala la Uraia wa Nchi Mbili (Dual/Smart Citizenship) na masuala mengine yahusuyo Watanzania wanaoishi nje ya nchi.

  Washiriki wa Kongamano hili ni Wanataaluma Wazalendo waliopo ndani na nje ya Tanzania. Kila Mwanataaluma wa fani yoyote anakaribishwa kuhudhuria. Kutakuwa na ada ya ushiriki ambayo ni TZS 50,000 (Kwa ajili ya kuchangia gharama za ukumbi; chakula; chai, vitafunio, matangazo, makabrasha ya mkutano, Vyombo vya Mawasiliano; ulinzi nk.). Viongozi wa Vyama Vya Kitaaluma na Wanataaluma Wanaharakati wa Maendeleo wawasiliane na TPN. TPN inapenda kutoa changamoto kwa Wanataaluma wote wenye mapenzi na uzalendo na Tanzania kuwa huu si wakati wa Kulaumu bali wa vitendo. Kama unaguswa na una mawazo mazuri juu ya kusaidia kuleta maendeleo ya nchi tafadhali sana usikose kuhudhuria. Ambao hawataweza kufika wanaweza kuwasilisha mawazo yao kupitia barua pepe: president@tpn.co.tz na watakaofanya "booking" mapema ya kutoa mawazo kupitia "Skype Video Conferencing/Chat" wanaweza kufanya hivyo kupitiaSkype ID ya: TPN_TZ

  Baadhi ya Mada zitakazojadiliwa, kuwekewa mikakati ya kiutendaji na ufuatiliaji ni pamoja na:
  1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara
  2. Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao
  3. Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.
  4. Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini
  5. Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi
  6. Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua za Kuleta Mabadiliko Na kwa Vipi?
  7. Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka/

  Kwa Kujiandikisha kuhudhuria Kongamano na kwa Maelezo Zaidi, tafadhali wasiliana na ofisi kupitia namba: 0715 740 047 na barua pepe: president@tpn.co.tz; www.tpntz.org. Tiketi zinapatikana Ofisi za TPN - TOHS Nyerere Road; Mayo 1999 Co. Ltd – Extelecom Samora Avenue; Zizzou Fashion Victoria na Africa Sana.

  Imetolewa: Wednesday, December 16, 2009 na:

  Sanctus Mtsimbe;
  Rais; Mtandao Wa Wanataaluma Tanzania
  (Tanzania Professionals Network, TPN)

   
 2. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Waandishi tutalipwa allowance??? Tutakuja ila kama hamtatulipa hatutaripoti kwenye magazeti. Mpo hapo waandaaji?
   
Loading...