Taarifa kwa vyombo vya Habari: Jumuiya ya Wazanzibari waishio UK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa vyombo vya Habari: Jumuiya ya Wazanzibari waishio UK

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HUNIJUI, Oct 19, 2012.

 1. HUNIJUI

  HUNIJUI JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 1,441
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jumuiya ya Wazanzibari waishio UK ZAWA UK inasikitishwa na matukio ambayo yanaendelea kutokea huko nyumbani Zanzibar yaliyoanza kujitokeza jana tarehe 17/10/2012 ambayo yamesababisha vurugu kubwa katika Miji ya Zanzibar na vitongoji vyake.

  Matukio hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa maisha ya askari wa jeshi la polisi,mali za Umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya siasa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuvunjwa Maduka, vyombo vya usafiri, kukatwa miti ovyo na nguzo za umeme, pamoja na kuchomwa moto maskani za CCM

  Kutokana na vitendo hivyo, ZAWA UK kinaalaani vikali matukio hayo ambayo yamepelekea uvunjifu wa mkubwa wa amani ya nchi, na kusababisha hofu kubwa kwa raia pamoja na wageni wanaotembelea Zanzibar.

  Pamoja na vurugu hizo, ZAWA UK kimepokea kwa mshangao mkubwa taarifa ya Serikali ya Zanzibar pamoja na ile ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kupitia jeshi la Polisi iliyoeleza juu ya kutoweka kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed katika mazingira ya kutatanisha.
  Katika Taarifa hiyo, Serikali zimethibitisha kuwa vyombo vyake vyote vya ulinzi havijamkamata Sheikh Farid, jambo ambalo limezidisha hofu na wasi wasi kwa wananchi juu ya mahali alipo na hali yake kiongozi huyo wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar.

  ZAWA UK kinaziomba Serikali zote mbili kuendeleza juhudi zote za kuhakikisha taarifa za ukweli na za uhakika zinapatikana juu ya kadhia ya kutoweka kwa Sheikh huyo kwani Sheikh Farid ni raia wa nchi hii, na Serikali hii ni kwa ajili ya wananchi wote, ili kuondoa hofu na wasi wasi ambao umesababisha baadhi ya wananchi kujengwa na dhana mbaya.

  Vile vile ZAWA UK kinawaomba wananchi wote kwa ujumla kutojiingiza na kutofanya vitendo vyovyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi yetu.

  Sote kwa pamoja tukatae kabisa kujihusisha na vitendo vya kuleta vurugu kwa vitendo na kauli zitakazopelekea kuiondolea sifa njema nchi hii ya Zanzibar.

  Mwenyekiti ZAWA UK

  Hassan Mussa Khamis
   
 2. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kwani aliyekamatwa na kufikishwa mahakamani kisutu sio ponda na huyo farid?
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Bora nyie Mumgu wenu amewaongoza kulaani............inasikitisha kuona baadhi ya watu wanafurahia
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  Farid hajakamatwa manake wala hajulikani alipo
   
 5. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,331
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  Zanzibar sio nchi, ebooo, kwa nini mnakuwa wagumu namna hiyo kuelewa! Yaani kila kitu lazima Polisi watumie virungu kuwaelimisha?
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ila mleta mada naye mbona umesahau kuwa makanisa yalichomwa Zanzibar? Maandishi yako yanaonesha nawe ni UAMSHO kwa asilimia 100%.
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  hawa hakuna la maana walilolaani, kama kweli wao sio mastermind, basi walaani kitendo cha sheikh farid kujipeleka mwenyewe mafichoni na kuwachochea wafuasi wake wafanye vurugu. Time will tell, atakamatwa tu.
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  kwa destur za waislam wenye misimamo mikali yuko mafichoni na inaelekea ndio wanaofadhili haya si bure na hivi wa tz wana njaa ndo kabisaaaa
   
 9. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,594
  Likes Received: 2,399
  Trophy Points: 280
  Tamko zuri lakini nawashauri mrudi nyumbani kwenu muwaelimishe ndugu zenu, kama huyo Bwana Farid haonekani wakichoma ofisi za CCM, kuangusha nguzo za umeme na kukata miti ndio tuwaeleweje au ndio Bwana Farid atarudi?

  Sitaki kusema hili lakini inabidi kusema tu % kubwa ya wenzetu zanzibar ni waislamu hali inayofanya wakristo waishi kwa hofu kutokana na matukio yanayoendelea ya kuchoma makanisa, sijui nyinyi mlioko huko uingereza Nchi inayoongozwa kwa misingi ya Kikristo mngejisikiaje kama mngechomewa Nyumba za Ibada, naamini uislamu si vurugu na wala haufundishi vurugu njooni muwaambie ndugu zenu jinsi munavyoishi kwa raha katika Nchi za magharibi japo munauchukia umagharibi.
   
 10. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni kweli gfsonwin ......njaa mbaya manake inapelekea watu wanatumiwa vibaya......hilo sio siri kuwa Farid kajificha
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  nawashangaa sana mwenzao Osama alijificha mwisho wa siku aliuawa kama kuku, sadaam hussein kadhalika hata gaddafi sasa nae huyu anataka kutuaminish akwamba nae ni mtu wa iman kali kama hawa atakufa kama mbwa tena asipoangalia atafia chooni.

  kama anahoja aje alete hoja zake mezani asikilizwe ila si kununuliwa na nchi za kiislam ili kuharibu amani ya taifa hili
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ana hoja atoe wapi dia?.......hana lolote ni ujinga tu unamsumbua
   
 13. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Seen and seen
   
 14. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  Ndugu zake(uamsho) wamemficha ili wapate sababu ya kufanya fujo
   
 15. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  na sidhani kama wanaweza kurudia makosa kama kwa Ulimboka
   
 16. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ujinga ni mzigo heri kubebaa gunia la mavi
   
 17. majany

  majany JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 30, 2008
  Messages: 1,199
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  bora umesema.
   
 18. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,333
  Likes Received: 2,335
  Trophy Points: 280
  kenehe mwanamayoo tokoja mahe lolo gwabhipaga.Haya ma mtu tuyafanye nini?
   
Loading...