Taarifa kwa vyombo vya habari - CHADEMA yakataa wito wa kamati ya Nchimbi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa vyombo vya habari - CHADEMA yakataa wito wa kamati ya Nchimbi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Sep 24, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  KATIKA kusimamia uongozi unaozingatia misingi muhimu ya haki za binadamu, sheria na utawala bora, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza msimamo wake wa kutotoa ushirikiano kwa kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi kuchunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel ten, Daudi Mwangosi, kilichotokea Septemba 2, 2012, Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa.

  Msisitizo huo umekuja baada ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo kukiandikia barua (isiyokuwa na Kumbukumbu Namba) CHADEMA, akiomba kamati yake ikutane na viongozi wa chama Septemba 25, ili kutafakari tukio hilo na matukio ya aina hiyo yaliyowahi kutokea hapa nchini.

  Itakumbukwa kuwa Marehemu Mwangosi aliuwawa na Jeshi la Polisi akiwajibika kwa jamii katika shughuli za uandishi wa habari, wakati askari wa jeshi hilo walipovamia ofisi za CHADEMA Kata ya Nyololo na kuanzisha vurugu wakati wanachama walipokuwa wakiendelea na shughuli halali za ndani za chama.

  Katika barua kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, CHADEMA kimesema wazi kuwa hakiko tayari kukaa na kutafakari juu ya kifo cha Mwangosi kama ilivyopendekezwa na kamati hiyo, kwani imeundwa kinyume cha sheria, huku pia ikiwa imeundwa na mtu ambaye kanuni za msingi za utawala bora, zinamtaka awe amejiuzulu au kufukuzwa kazi, kupisha uchunguzi huru juu ya mauaji hayo yaliyofanywa na jeshi la polisi, linalowajibika kwake kama Waziri wa Mambo ya Ndani. Kamati hiyo pia inawahusisha polisi ambao katika tukio hilo ni watuhumiwa namba moja.

  Mbali ya kusisitiza kuwa haiwezi kutoa ushirikiano kwa kamati ambayo haipo kwa mujibu wa sheria, CHADEMA kimeshangazwa na kusudio hilo la Kamati ya Nchimbi kutoa mwaliko wa kutaka kukutana na viongozi wa CHADEMA, huku ikitambua wazi msimamo wa chama hiki juu ya uwepo wa kamati hiyo mara tu ilipoundwa.

  Kutoa ushirikiano kwa kamati ambayo haina mamlaka ya kisheria ya kuhakikisha ukweli mtupu unajulikana na haki ionekane ikitendeka kutokana na kifo hicho na vingine vingi ambavyo vimefanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia, kwa masuala mbalimbali yakiwemo ya kisiasa, ni kuhalalisha uvunjivu wa haki za binadamu, Katiba na sheria za nchi. CHADEMA haiko tayari kuona hali hiyo ikifanyika.

  Katika kuonesha msisitizo wa kutokubali mwaliko wa Kamati ya Nchimbi inayotaka kutafakari matukio ya vifo ambapo Jeshi la Polisi limewanyang'anya watu wasio na hatia haki ya kuishi, katika barua yake ya majibu, CHADEMA pia kimeambatanisha nakala ya barua ya tarehe 10/09/2012 iliyowasilishwa kwa Rais, ili kamati hiyo iweze kuelewa msimamo mpana wa chama kuhusu mauaji ya kisiasa yanayofanyika nchini.

  Kwa taarifa hii, CHADEMA kinaendelea kusisitiza maazimio ya Kamati Kuu ya Chama, ambayo pamoja na mambo mengine, iliazimia kuwa kutokana na mfululizo wa matukio ya mauaji ya kisiasa yanayofanywa na Jeshi la Polisi katika shughuli halali za chama, Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile wawajibike kwa kujiuzulu au Rais awawajibishe kwa kuwafukuza kazi ili wapishe uchunguzi huru na wa haki.

  Pia Kamanda wa Polisi Iringa, Michael Kamuhanda, Kamanda wa FFU Mkoa wa Morogoro, na askari wote wanaoonekana kwenye picha wakiwa wamemzunguka Mwangosi muda mfupi kabla hajalipuliwa na kuuwawa, wakamatwe haraka na kushtakiwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Mwangosi. Kinyume na hapo ni kuchezea akili za wapenda haki na uwajibikaji, ikiwa moja ya misingi ya amani Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.

  CHADEMA inapenda kusisitiza kuwa itatoa ushirikiano kwa chombo kitachoundwa kwa mujibu wa Sheria huku ikitilia msisitizo wito kwa Rais kuunda Tume ya Kimahakama/Kijaji kuchunguza vifo vyote vyenye utata na vinavyohusishwa na masuala ya kisiasa kama tulivyopendekeza kwake hapo kabla.

  Imetolewa leo Septemba 24, 2012 Dar es Salaam na;

  Tumaini Makene
  Ofisa Habari wa CHADEMA
   
 2. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  makini sana.

  Imetulia, big up makene, big up CHADEMA
   
 3. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  makini sana.

  Imetulia, big up makene, big up CHADEMA
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kwani aliyeuwa Si alionekana kwenye picha? Kuna haja gani ya kuwapotezea muda viongozi wetu wa CDM kwenye jukumu tulilowapa la kuikomboa hii nchi kupitia M4C
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu kwa taarifa! At least Tumain Makene amewahi kutuhabarisha. Binafsi naunga mkono hoja!
   
 6. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  kamanda makene niko italia. message sent wataliano huwa wanasema kuwa- messagio inviato. message imetulia na imetumwa na watu wanaojua nini maana ya uofisa habari.
   
 7. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,977
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Yaani nyie mtuue halafu mpeane ulaji kupitia kamati zenu uchwara tena kwa kodi zetu. Kinachosikitisha zaidi repoti mtakayoitoa tayari inajukana itakuwa na sura gani. Mola inusuru Tanzania, inapoelekea siyo pazuri!
   
 8. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,031
  Likes Received: 37,800
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo utawependa chadema.

  Wana hoja na sababu za msingi za kuikataa kamati.

  Kikubwa wana msimamo.
   
 9. S

  STIDE JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwa UMAKINI TU CDM wako juu!! Chama hakibabaiki wala kupelekeshwa kipumbavu!!

  NAJIVUNIA KUWA UPANDE HUU!!
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu kwa taarifa! At least Tumain Makene amewahi kutuhabarisha. Binafsi naunga mkono hoja!
   
 11. Root

  Root JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,308
  Likes Received: 13,017
  Trophy Points: 280
  nice move
   
 12. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  sidhani kama hilo lilikuwa muhimu sana kuliandika
   
 13. j

  jigoku JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Keep it up CDM,hatuwezi kushiriki kwenye uppuzi kama huo.wakati alieunda kamati ya harusi ni mtuhumiwa,mjumbe mmoja wapo ni mtuhumiwa,na bado kamati hiyo ambayo ni sawa na ya harusi haina mamlaka kisheria.

  Makene asante mkuu kwa taarifa
   
 14. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  mwanangu umepotea!
   
 15. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mambo mengine kwa kweli ni kupotezeana wakati na fedha bure!!!Naomba kuuliza,hivi wanachunguza nini ambacho hakipo wazi?
   
 16. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Taarifa imenyooka sana.
   
 17. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Hapa sawa
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hata sioni umuhimu wa hiyo kamati. Naungana na CDM katika umakini wao wa kuchambua mambo!!!
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kesho mkutano wa M4C pale ngarenaro..
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  I support you!
   
Loading...