Simba SC yatoa taarifa rasmi, yataka kupewa ushindi kwa Yanga SC kususia kuingiza timu uwanjani

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
18,511
68,141
Ifuatayo ni taarifa yao rasmi.

E09ChO8XMAA7OYR.jpg
E09ChPdWYAAr-Lp.jpg
 
Japo mimi ni Simba SC ila kwa hili tamko lao lililokosa support ya kanuni au sheria kupinga kile walichosema Yanga SC jana kuhusu kanuni ya ligi No. 15 (10) wamekosea.

Nawaona Simba wametoa sababu nyepesi sana, unless kama hiyo kanuni waliyoitoa Yanga iwe na exception kwamba inaweza badilika kulingana na mazingira fulani yatayojitokeza ndio Simba waitumie hiyo exception but not otherwise.

UPDATE:
Nimeona Rage amesema hicho kifungu walichonukuu Yanga SC kina exception kama nilivyoeleza pale juu, Rage anadai Yanga hawakusoma sheria yote japo nae hajanukuu hicho kifungu cha kanuni, ila kama huu ndio ukweli basi Simba SC wanaelekea kuwa sahihi kwa ule uamuzi wao wa kuingiza timu uwanjani saa moja usiku.
 
Kama Yanga kweli walipigiwa wakakubali then wakademka na kudeka baada ya reaction ya mashabiki wao sioni namna ya deko hilo kutokuchukuliwa adhabu.

Na kanuni ya 31 inailinda TFF kuwa ikiona ni dharura yaweza ahirisha muda wa mechi

Tatizo ni kwamba kama yanga ilikubaliana na Bodi ya Ligi kama ni kweli siwaungi mkono
 
Simba ni club kubwa lazima wana vyanzo vyao pia vya kunusa na kusikia. Kutakuwa kuna kitu lazima. Uchunguzi ufanyike na majibu yapatikane na WA kuwajibishwa apate kinamchostahili. Inaweza kuwa ilikua imeratibiwa vyema sana hiyo sio juujuu tu.
 
Kuhairishwa Kwa sababu zipi?
Simba Kama wanatii maagizo na maelekezo ya TFF iweje tena wapinge maelekezo ya kuahirishwa mechi mpaka itakapopangiwa tarehe nyingine? Simba waache uoga na kutaka pointi za mezani ili kukwepa kipigo!
 
Na hapa nanusa mbuzi wa kafara mkanganyiko ulikuwa mkubwa mno
 
Watanzania tusifanywe wajinga, kwa huu uhuni uliofanyika jana na siku za nyuma basi tumtake WALLACE KARIA AJIUZULU, ALMAS KASONGO wa Bodi ya Ligi nae aachie ngazi

Msimu uliopita bodi ya ligi katika kupanga ratiba ya mechi ilishawahi kuisahau Yanga katika kuipangia mechi, ikapita takribani siku Tatu ndipo wadau wakastuka kwamba mbona Yanga haipo ratibani, kiongozi bodi ya ligi akaomba radhi nako ikapita kimya kimya

Marefarii wakifanya mistakes za uwanjani wanakula ban karibu miezi mitatu mpaka mwaka

Sasa kwa hili lililotokea la Simba vs Yanga,,, KARIA na KASONGO muondoke ktk hizo nafasi,, hamfai

#KariaOut
#KasongoOut
 
Hakuna kifungu chochote kusupport hoja yake(sio yao). Nina uhakika huyo aliyeandika hiyo taarifa ni Manara. Pale Simba hakuna kiongozi mwingine mwenye elements za kujipendekeza kwa serikali zaidi ya Manara. Halafu eti anasema tulipewa taarifa za mapendekezo ya kusogeza muda wa mechi mbele tukakubali wala hatuhoji. Empty set.
 
We Simba wewe! Toka lini serikali ikapanga ratiba au muda wa kucheza soka? Wewe kama ulikubali maelekezo ya kusogeza mechi masaa mawili mbele bila kupewa sababu, unakataa je maelekezo ya kuahirishwa mechi bila sababu kutoka kwa huyo huyo aliyekupa maelekezo ya awali?

Lakini we simba, unayo maandishi yanayothibitisha kwamba Yanga walikubaliana na maelekezo ya kusogeza muda wa mechi kutoka saa 11 hadi saa 1? Kama unayo yaweke hadharani kukazia hoja yako!

We Simba we, unachopaswa kufanya ni Kuungana na Yanga kulaani upuuzi wa TFF wa kuvunja kanuni walizojitungia badala ya kusukumiza Zigo kwa Yanga!

We simba, nakutaarifu kuwa Ki kanuni, Yanga wanastahili point 3 na magoli2. Wewe simba imeingizwa chaka na TFF nawe ukakubali kurubuniwa ukashindwa kuingiza timu uwanjani, umedanganywa.
Kumbuka tarehe 8/5 siyo siku ya wajinga. Ingekuwa tarehe 1/4 tungekufikiria fikiria kuwa kwakuwa ilikuwa siku ya wajinga basi!

Simba wewe ulikubali maelekezo FEKI hivyo unastahili kupokonywa Pointi ki roho safiiii!
 
Back
Top Bottom