Taarifa kwa UMMA: Waliokosa nafasi za kujiunga kidato cha tano second selection watakiwa kuomba kujiunga na vyuo.

Gamlemilwe

JF-Expert Member
May 26, 2013
290
200
TANGAZO KWA UMMA

OR-TAMISEMI imetangaza majina ya wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano kwa awamu ya pili tarehe 23 Agosti, 2017. Wanafunzi hawa ni miongozi mwa wanafunzi 34,727 wakiwemo wasichana 10,932 na wavulana 23,795 wenye sifa za kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi hawakuchaguliwa katika awamu ya kwanza baada ya kukosa Nafasi.

Wanafunzi 14,768 wakiwemo wasichana 6,763 (Sayansi 2,171 na Sanaa 4,592) na wavulana 8,005 (Sayansi 3,063 na Sanaa 4,942) wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika
awamu ya pili kujaza nafasi za wanafunzi ambao hawakuripoti katika awamu ya kwanza na nafasi zilizopatikana kwenye shule zilizoongeza miundombinu ya
Kidato cha Tano.

Aidha, wanafunzi 19,959 (wakiwemo wasichana 4,169 na wavulana 15,790) hawajapangiwa shule kutokana na kukosa nafasi. OR-TAMISEMI inapenda kuwasihi wazazi na walezi wa Wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na kidato cha tano mwaka 2017, waombe nafasi za mafunzo katika vyuo vya kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Ufundi (NACTE) ambavyo zoezi la kuomba linaanza mwezi Septemba, 2017.Fani zinazotolewa na vyuo hivi zinapatikana kwenye tovuti ya NACTE ya www.nacte.go.tz.


Imetolewa na
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais –TAMISEMI
25 Agosti, 2017
 
Back
Top Bottom