TAARIFA KWA UMMA - Sahihisho la TLS Juu ya Kichwa cha Habari cha Gazeti la Raia Mwema la tarehe Aprili 17-23 2019

Oct 15, 2018
17
153
Mnamo tarehe 11 Aprili 2019 nilifanya mahojiano na Mwandishi wa Gazeti la Raia Mwema, Mary Victor, kufuatiwa kuchaguliwa kwangu kuwa Raisi wa TLS. Sehemu kubwa ya mahojiano hayo imechapishwa katika Gazeti la Raia Mwema toleo Na. 658 la tarehe 17-23, 2019 kurasa za 12-13 na 16. Hata hivyo ukurasa wa kwanza wa Gazeti la Raia Mwema umeandikwa kichwa cha habari kinachosomeka: “Nshala: Mahakama imfukoni mwa Dola.” Napenda kusema kuwa kichwa hicho cha habari na jumuisho lake si sahihi ya kile nilichokisema na kumaanisha. Ujumbe mkuu niliousema ni kuwa Mahakama zetu si tu ziwe huru bali pia zionekane kwa Mwananchi wa kawaida kuwa zi huru.

Mkazo wangu ulijikita katika mtindo uliojitokeza hivi karibuni wa ushiriki wa majaji katika shughuli za kidola ambazo hazihusiani na shughuli za mahakama. Nilitoa mifano ya matukio ambayo yanaweza kuleta taswira hasi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa Jaji Mkuu katika sherehe za kupokea ndege au kupokelewa kwa ripoti za kiserikali na majaji kuhutubiwa na Raisi wa nchi pale mawaziri wa serikali wanapoapishwa kuwa kunaweza kuleta mashaka kwa wananchi juu ya uhuru wa mahakama na kuwafanya wao wadhani kuwa muhimli wa mahakama u mfukoni mwa dola. Katu kamwe sikusema kuwa muhimili wa mahakama u mfukoni mwa dola.

Nimewasiliana na Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema juu ya hilo na ameahidi kuwa watafanya sahihisho katika Gazeti lifuatalo. Napenda kutoa pole kwa Mheshimiwa Jaji Mkuu, Waheshimiwa Majaji, Mahakimu wote, na Mawakili wote ambao wameumizwa na kichwa hicho cha habari ambacho si sahihi. Ninapenda kusema kuwa mahakama zetu zi huru na ni lazima zilinde uhuru huo na kutoruhusu dhana kuwepo kwa taswira hasi inayoweza kuondoa imani ya wananchi juu ya uhuru wake.

Imetolewa Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 2019.

Dr. Rugemeleza A.K. Nshala
Raisi-TLS​
 
Attachments

  • Sahihisho la TLS Juu ya Kichwa cha Habari cha Gazeti la Raia Mwema la tarehe Aprili 17-23 2019.pdf
    315.8 KB · Views: 14
Kweli mhimili wa Mahakama kuwepo kila shughuli ya 'kisiasa ' ya mhimili wa dola / serikali unazua mashaka na mjadala mpana.
 
Nshala waambie pia wasichukue pesa toka serikalini...!! Unafikiri kuwa huru ni pale tu usipohudhuria shughuli za serikali itafika utawaambia wasishiriki hata kwenye sherehe za wafanyakazi wa serikali. Panua uwezo wa kufikiri msomi Wakili acha kukariri.
 
Mnamo tarehe 11 Aprili 2019 nilifanya mahojiano na Mwandishi wa Gazeti la Raia Mwema, Mary Victor, kufuatiwa kuchaguliwa kwangu kuwa Raisi wa TLS. Sehemu kubwa ya mahojiano hayo imechapishwa katika Gazeti la Raia Mwema toleo Na. 658 la tarehe 17-23, 2019 kurasa za 12-13 na 16. Hata hivyo ukurasa wa kwanza wa Gazeti la Raia Mwema umeandikwa kichwa cha habari kinachosomeka: “Nshala: Mahakama imfukoni mwa Dola.” Napenda kusema kuwa kichwa hicho cha habari na jumuisho lake si sahihi ya kile nilichokisema na kumaanisha. Ujumbe mkuu niliousema ni kuwa Mahakama zetu si tu ziwe huru bali pia zionekane kwa Mwananchi wa kawaida kuwa zi huru.

Mkazo wangu ulijikita katika mtindo uliojitokeza hivi karibuni wa ushiriki wa majaji katika shughuli za kidola ambazo hazihusiani na shughuli za mahakama. Nilitoa mifano ya matukio ambayo yanaweza kuleta taswira hasi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa Jaji Mkuu katika sherehe za kupokea ndege au kupokelewa kwa ripoti za kiserikali na majaji kuhutubiwa na Raisi wa nchi pale mawaziri wa serikali wanapoapishwa kuwa kunaweza kuleta mashaka kwa wananchi juu ya uhuru wa mahakama na kuwafanya wao wadhani kuwa muhimli wa mahakama u mfukoni mwa dola. Katu kamwe sikusema kuwa muhimili wa mahakama u mfukoni mwa dola.

Nimewasiliana na Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema juu ya hilo na ameahidi kuwa watafanya sahihisho katika Gazeti lifuatalo. Napenda kutoa pole kwa Mheshimiwa Jaji Mkuu, Waheshimiwa Majaji, Mahakimu wote, na Mawakili wote ambao wameumizwa na kichwa hicho cha habari ambacho si sahihi. Ninapenda kusema kuwa mahakama zetu zi huru na ni lazima zilinde uhuru huo na kutoruhusu dhana kuwepo kwa taswira hasi inayoweza kuondoa imani ya wananchi juu ya uhuru wake.

Imetolewa Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 2019.

Dr. Rugemeleza A.K. Nshala
Raisi-TLS​
Mkuu sheria(mfumo) za uchaguzi hazipo sawa kabisa tangu vyama vingi vianze. Sijui kama mnaliona hilo na mnasaidiaje
 
Kumekucha! Hawa si ndio akina mutungi na tibaijuka? Sasa huyo dada mere si unamharibia jina wakati mhariri ndiye aliidhinisha article husika?
 
Back
Top Bottom