Taarifa kwa Umma: Polisi wavamia mkutano wa ndani wa Uchaguzi jumuiya CUF Handeni

View attachment 1653374TAARIFA KWA UMMA:

POLISI WAVAMIA MKUTANO WA NDANI WA UCHAGUZI WA JUMUIYA CUF HANDENI:

Jeshi la Polisi limevamia Mkutano wa Uchaguzi wa Jumuiya za CUF- Chama Cha Wananchi- Jumuiya ya Wanawake (JUKECUF) na Jumuiya ya Vijana ( JUVICUF) Handeni Tanga.

Kwa mujibu wa Maelezo ya Naibu Mkurugenzi wa Itifaki na Udhibiti wa Chama Mheshimiwa Masoud Omar Mhina, Jeshi la Polisi limevamia Mkutano huo kwa Shinikizo la Mkuu wa Wilaya ya Handeni. Viongozi kadhaa wamekamatwa katika tukio hilo.

CUF - Chama Cha Wananchi kinatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Wilaya kuwaachia huru Viongozi na wanachama wanaowashikilia/kuwabughudhi ili waendelee na Mkutano huo na si vema kujaribu mara kwa mara kuichezea Amani. Uvumilivu wa Watanzania ni zao la busara zao na kamwe isitafsirike kwamba hakuna ' nukta ya mwisho' ya uvumilivu huo.

Matukio haya ni muendelezo wa ukiukwaji wa Sheria za nchi ikiwa ni pamoja na Katiba ya nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa unaofanywa na Serikali ya Kimabavu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tukio hili linatokea ikiwa zimebaki siku mbili (2) kabla ya Kufanyika kwa KONGAMANO la Kudai Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya lililoandaliwa na wanachama wa CUF- Chama Cha Wananchi, linalotarajiwa kufanyika Jumapili Desemba 20, 2020 Ofisi Kuu Buguruni.

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!


Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Desemba 18, 2020
Ule ushirikiano wa Lipumba na ccm umeishia wapi ?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom