Taarifa kwa Umma: Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akutana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kattanga Ikulu ya Chamwino Dodoma

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,204
4,694
Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga

Mazungumzo hayo muhimu yamefanyika leo Aprili 20, 2021 Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.

Mpango-Kattanga.jpg
 
Hiyo salamu kumbe Corona ipo, sasa kuunda tume ili iweje mnachezea pesa tu.
 
Kwahiyo sasa imekuwa ndio mtindo kila viongozi wakikutana tuambiwe. Lakini cha ajabu hatuambiwi wanakutania nini.

Nje ya mada; Kuangalia hiyo picha inaonekana dhahiri Bashiru hakupaswa kabisa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Kuna nafasi nyingine zinaenda na haiba ya mtu. Hapo Bashiru angekuwa na kaunda suti yake kama mfuasi wa Mao.
 
ACHENI USANII NYIE WATU. WOTE OFISINI ZENU ZIPO HAPO HAPO IKULU KILA SIKU MNAONANA NA KUNYWA CHAI PAMOJA.

TUAMBIENI MMEONGEA NINI SIO KUTUMA PICHA TU.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Viongozi wote wapo Ikulu lakini mmoja kutoka mlango huu kwenda mwingine ni taarifa kwa UMMA!

Ningeelewa kama aliyeenda ofisi/mlango wa mwingine kutoa taarifa ya kizito kilichompeleka, lakini kupigiwa picha hivi wakati tunawafahamu na wote wapo geti moja kazini naona ni USHAMBA

Cc Uzalendo Wa Kitanzania
 
Ripoti ya CAG kuhusu pesa zilizotoka BOT mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tatu iko wapi?
 
Nimeipenda iyo nje ya mada yako.

Yani mtu yupoyupo tu. Unamtoa huko unampa ukatibu mkuu kiongozi. Hajawai kuwa hata DAS au DED achilia mbali RAS au Katibu mkuu.

Kweli Magufuli aliigeuza hii nchi kama familia yake binafsi. Bora Mungu alifanya yake Kwa kweli!

Back
Top Bottom