Taarifa kwa umma: Maazimio ya mkutano mkuu wa wilaya ya Arusha mjini - 3 agosti 2011

Nadhani viongozi wengi wa chadema hamkujua kuwa watu tumechoka kiasi gani na tabia za viongozi wabovu na wasio na msimamo na hapa sasa mnatakiwa mjue nguvu ya umma ina uwezo gani na inataka nini kwa viongozi wa chadema kwa kifupi ni hivi hao wasaliti hata wangekwenda kwa Mbowe akasema amewasamehe na kuwarudisha tungenyamaza lakini tungesha wajua kuwa kuwa viongozi wa chadema hawana tofauti na magamba wa Vasco Da Gama hivyo tungejiondokea kimya na kutafuta chama chenye mwelekeo na kuhamia huko na kwa jambo hili mmeonyesha ukomavu kwa kusoma alama za nyakati na kujua wananchi wanataka nini na sio ubabaishaji na vyeo na ndiyo maana tulikuwa tayari kukosa madiwani na hata tubakiwe na madiwani wawili au mmoja wenye msimamo na siyo mamluki ya madiwani wasioelewa wananchi wanataka nini.

Wameona mambo magumu sasa wanataka kuomba msamaha? Hasa Malla aliongea kwa jazba pia Bayo pale kijiweni kwenye pool karibu na stendi ndogo alikuwa anaongea kwa kujiamini sana kwamba tumechoka na maandamano pia mwafaka ni Wa halali, nashangaa kusikia wanataka kuomba msamaha bado siamini kama ni kweli.

Wakuu,hili ni tamko baada ya mkutano mkuu wa wilaya,ambao ni viongozi wa kata zote,uliokuwa na ajenda ya kuridhia kujiuzulu kwa viongozi wa wilaya,na viongozi wa kata zote za Arusha mjini,wakaazimia kwa kauli moja kuwa madiwani wasaliti hawafai tena,na kamwe wasisamehewe tena,hii ni baada ya hawa madiwani wasaliti kutafuta wazee maarufu ili kwenda nao dodoma kwenye kikao cha kamati kuu kitakachofanyika jumamosi hii.Baada ya hali kuwa mbaya na shinikizo la nguvu ya umma kuwa kubwa wanaomba msamaha kwa chama

Mh Nanyaro kwanza nikushukuru mno pili niweke wazi tuu kuwa kila jambo baya wanalofanyiwa watafutao Haki hulipwa hapa hapa duniani.Nanyaro usikate tamaa Mungu yupo upande wenu.Peoples Power.Msisahau Sauti ya wengi ni Sauti ya Mungu.

Hivi mbona Rostam kaombwa kujiuzulu na sikuona tume yoyote inayozungumzia yeye kujitetea..Chama kujivua magamba na hakuna tume yeyote kuwalinda magamba ambao wote ni Wabunge...Vipi wakuu zangu, mnataka kuchekacheka na hawa watu saba tena madiwani ambao wanaweza kuwa replaced kirahisi kabisa. Kuna sababu gani chama kiwakilishwe na madiwani ambao hawawakilishi sera za chama.. Kuna tofauti gani kati ya hawa madiwani na mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo, halafu kuna watu wanakuwa na ujasiri wa kusema - Mbwa mwitu apewe nafasi ya kujitetea..

It's very simple rule of royalty - Never take sides with anyone against Your family!
Na maadam hawa madiwani wameamua ku side na CCM kwa maslahi ya CCM wakisingizia wananchi kama kigezo cha maamuzi yao basi waondolewe Udiwani haraka iwezekanavyo na uchaguzi mpya ufanyike. Ni bora CDM i face changamoto leo ktk uchaguzi wa Madiwani kuliko kusubiri mwaka 2015 na wakashindwa vibaya kutokana na kazi mbaya ya hawa madiwani walio - shake hands with a devil. CCM wanajua sana jinsi ya kutumia nafasi kama hizi.

Ngonjera Ngonjera Ngonjera za Magwanda!
Kama lilivyo jina lako sishangai posti yako...chadema imebaki kuwa chama pekee hapa Tanzania kinachotetea maslahi ya watu maskini kabisa...naomba tusipoteze dira zetu, mapandikizi kama haya lazima tuyang'oe mapema ili tubaki na mbegu bora ya kizalendo kuliko kuwa hawa wasaliti waliokubali 10% ya magamba...hawatufai, hatuwataki na ikithibitika walipokea rushwa tuwe wakwanza kuonyesha mfano kwa kuwashtaki mahakamani vinginevyo nguvu ya umma tutawarekebisha...

Je tukiwafukuza hao saba tunaweza kutetea na je hayo maagizo mwisho lini

Mkuu ni bora wakafukuzwa ndani ya Chama kuliko kua na watu ambao niwa nafiki na wakaidi juu ya katiba ya Chama pia hawa waheshimiwa ni rahisi kuvujisha siri za Chama huko tuendako na wakatuharibia,naomba kamati kuu Jmos wafikie maamuzi ya kuwafukuza kabisa hawafai kua ndani ya Chama

Lazima waende,nafasi ya kujirudi walipewa,tabia hii ya kupindisha taratibu halafu kugawana vyeo kama kwa Kibaki au Mugabe hatutaikubali,sasa baadaye na hata milele!

Katika kumbukumbu zangu huyu mh. aliyekuwa amepachikwa u naibu meya wa jiji alijitutumua siku moja kwenye vyombo vya habari kwamba yeye amepata madaraka yale kwa muafaka halali wa pande zote mbili. Na kwa kuwa it was sounding so awkward to me I switched off my TV and left because it was so boring info to see.

Wafukuzeni ndio mtajua kama mtaweza kutetea.

mi naona bora kupoteza viti vya madiwani kuliko kukidhariri ha chama.tena huu mgogoro usipoangaliwa kwa mapana hata jimbo litapotea machoni mwa cdm

njaa kwakweli ndo inadumaza demokrasia hapa nchini, inawezekana kabisa hao madiwani 7 wamepewa mabahasha, ila bado hili sijalipa kipaombele kwa leo, bado akili zangu zipo kwa shimbo na trillion zaidi ya 3.

Hii mambo ya kuongelea hela kubwa namna hii kama vile unaongelea Tshs 10/= ndo hua inasababishaga inflation, maana mwisho wa siku watu wanaizoea hiyo figure,
Huyo jamaa akamatwe kwa kusababisha inflation pia

Ninakichukia chama cha Magamba kwa sababu ya ulegelege wake wa kutoa maamuzi. Ninawachukia Magamba na serikali yake kwani haionyeshi uongozi hasa kwenye maamuzi magumu. Rais wa Marekani G. W. Bush alimesema kwenye kitabu chake cha Decision Point, anachukia wanasiasa wengi kwani wanaogopa kutoa maamuzi magumu, wanataka kupendwa na kila mtu duniani. Huwezi kuwa kiongozi imara unayeepuka kutoa maamuzi.

CDM wajifunze leo kuwa uongozi sio kuangaliana sura, Tukishindwa kuitetea katiba ya chama kweli tutaweza kuitetea katiba ya nchi. Leo nchi inazalisha kina Shimbo, Rostam, El , Chenge kwa sababu watawala waliwaogopa wakati wakiwa dagaa, sasa wanagwaya kwani wamekuwa mapapa.
Tukishindwa vidagaa vinavyojifanya Miungu watu hatutaweza kupambana na mapapa.

Hawa madiwani uchwara ni mfano hai wa mawaziri, wakurugenzi, Rais, makatibu wakuu, wataalamu mbali mbali wanaoingia mikataba mibuvu kwa kupewa vijidola vichache na kuliingiza Taifa kwenye majanga, kama kukosa kodi, kukosa ajira, wananchi kunyanuaswa na wawekezaji. Kama Muafaka haukuwa wa Chama kwa nini mpaka leo ngonjera ni nyingi?

Katiba iweke wazi kuhusu mamlaka ya kila kiongozi na wapi mwanachama au kiongozi atakuwa amejifukuzisha mwenyewe bila kufukuzwa. Kama kweli hawa madiwani waliingia muafaka bila ya chama maana yake wao sio chama.
CDM toeni maamuzi acheni vikao kama magamba, onyesheni tofauti yenu na magamba, tunaichukia magamba kwa matendo yake. Kuweni makini na kauli zenu, kikomo kiwe kikomo chama sio viongozi wasaliti ni wananchi wasio viongozi waliotayari kufa na kupigwa mabomu, kudhalilishwa ili kutetea chama. Hawa wananchi wanahitaji heshima na utawala uliotukuka, uwajibikaji na viongozi wanofuata maadili na kulinda katiba, misingi na maazimio ya chama. Viongozi wanaoogopa rushwa za aina zote, fedha, madaraka, nk.

CDM tujenge chama imara sio mradi chama.

Hizi trilioni mpaka ziishe kutapambazuka kwa tabu sana. Nilisha sema katiba ifuatwe kwani katiba inasemaje kiongozi akisaliti Chama? Mbona vikao vinakuwa vingi badala ya maamuzi. Kama ni kufukuzwa wafukuzwe au tukae kimya kama Magamba. Too much politics. Wamekosea wamekataa kurudi kwenye katiba waondoke.

NAUNGA HOJA MKONO!

Back
Top Bottom