Taarifa kwa umma: Maazimio ya mkutano mkuu wa wilaya ya Arusha mjini - 3 agosti 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa umma: Maazimio ya mkutano mkuu wa wilaya ya Arusha mjini - 3 agosti 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chachana, Aug 4, 2011.

 1. c

  chachana Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA UMMA - 4 AGOSTI 2011

  Ndugu wanahabari, Jana tarehe 03 Agosti 2011 Baraza la Uongozi la CHADEMA Mkoa wa Arusha liliitisha kikao cha Mkutano Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kujadili hali ya kisiasa ya wilaya ya Arusha mjini hususan kufuatia muafaka wa madiwani wa CHADEMA na wale wa CCM katika manispaa ya Arusha na pia kufuatia kujiuzulu kwa wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji ya chama chetu wilaya ya Arusha mjini.

  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini (Kwa mujibu wa Ibara ya Katiba ya Chama Kifungu cha 7.4.5 sehemu (a) – (g) walihudhuria kikao hicho ambapo kati ya KATA 19 zilizopo wajumbe wote kutoka KATA 18 walihudhuria.

  Wajumbe walikutana jana tarehe 3 Agosti 2011 katika hotel ya Stereo chini ya Uenyekiti wa Mhe Samson Mwigamba (Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha) ambao kwa pamoja waliazimia yafuatayo.

  1.Wajumbe kwa kauli moja walikubaliana na Kamati Kuu kwamba hapajawahi kuwepo muafaka kati ya CHADEMA na CCM kuhusiana na mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa manispaa ya Arusha. Kile kinachoitwa muafaka wa madiwani wa CCM na wa CHADEMA ni makubaliano yaliyosainiwa na mkuu wa wilaya na diwani kupitia TLP ambao wote hawawakilishi CHADEMA wala CCM.

  2.Mkutano mkuu wa wilaya umeipongeza kamati kuu ya chama kwa maamuzi ya busara ya kuukataa muafaka huo sanjari na kuwataka madiwani waliopata vyeo vya unaibu meya, uenyekiti wa kamati ama ujumbe wa kamati kutokana na muafaka huo, wajiuzulu.

  3.Wajumbe wamesikitishwa na kitendo cha madiwani kukosa adabu kwa Kamati Kuu na Katibu Mkuu kwa kukaidi agizo la Kamati kuu lililowataka kujiuzulu nafasi walizozipata kufuatia muafaka batili wa UMEYA hapa Arusha mjini na kuomba radhi kwa kuingia na kukubali muafaka bila ya kushirikisha chama na kuwa kinyume na taratibu za chama.

  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya wamewapongeza sana madiwani waliotii agizo la kamati kuu na wanaiomba kamati kuu kuwapongeza madiwani watiifu lakini iwachukulie hatua kali ya kuwafukuza mara moja kutoka katika chama chetu madiwani wafuatao kwa vile ukaidi na kibuiri walichoonyesha kimewafanya wasiaminike tena na chama hata kama wataomba radhi leo. Madiwani hao ni:

  i)Mhe Estomih Mallah – Diwani wa Kimandolu

  ii)Mhe John Bayo – Diwani wa Elerai

  iii)Mhe Ruben Ngowi – Diwani wa THEMI

  iv)Mhe Crispin Tarimo – Diwani wa Sekei

  v)Mhe Charles Mpanda – Diwani wa Kaloleni

  vi)Mhe Rema Mohamed – Diwani wa Viti Maalum

  Aidha wajumbe wa Mkuano Mkuu wamependekeza kwa Kamati Kuu kuwa kwa vile muda wa kuomba msamaha umeshapita na kuwa walishapewa nafasi ya kwanza hawakuitumia badala yake wakakata rufaa yenye madai yasiyo na adabu kwa chama na kwa KATIBU MKUU, na pia wakapewa mwongozo ambao uliwapa tena siku tatu na hapo wakashindwa kuomba radhi ndani ya muda, Wajumbe wa Mkuano Mkuu wameazimia kuwa madiwani hawa wafukuzwe kwa maana hawana nidhamu kwa chama na wanahatarisha umoja na usalama ndani ya chama

  4.Wajumbe wa Mkutano Mkuu wamesikitishwa na Uongozi wa Wilaya uliokuwepo ambao kwa hiari yao walijiuzulu tarehe 01 Agosti 2011 baada ya kushindwa kufanya majukumu yao ya kikatiba. Aidha Wajumbe wa Mkutano Mkuu wameafiki na kukubaliana na hatua ya kamati hiyo kujiuluzu kwani ilishindwa kabisa kutimiza majukumu yake na kusababisha ombwe la uongozi hapa Arusha mjini ombwe ambalo mkutano mkuu ulilitafsiri kuwa chanzo hata cha mgogoro uliopo sasa kati ya madiwani na chama.

  Mkutano mkuu pia ulilipongeza Baraza la Uongozi la Mkoa ambalo kwa mujibu wa Katiba ya Chama kifungu cha 6.1.3 wana mamlaka ya kuteua kamati ya muda ili kuratibu shughuli za chama na wanachama kwa kipindi kilichowekwa. Wajumbe kwa kauli moja wameiridhia kamati hiyo ya muda chini ya uenyekiti wa Mh. Ephata Nanyaro na wameahidi kutoa ushirikiano kwa kamati hii katika kuratibu kazi za chama wilaya na kuimarisha mtandao wa chama kuanzia ngazi ya msingi.

  5. Wajumbe wamekubaliana na kuazimia kuwa, endapo kamati kuu itawavua uanachama madiwani wakaidi basi viongozi wote wa chama kuanzia ngazi ya msingi wataungana kwa pamoja kuhakikisha kuwa KATA hizo zinarudi mikononi mwa CHADEMA.

  Mwisho, tunawataka wanachama wote wa CHADEMA katika wilaya ya Arusha Mjini kuendelea na harakati katika kukijenga chama wanachokipenda cha CHADEMA na kusimamia haki na ukweli kwa maendeleo yetu sote. Kamwe asiwepo na tusimruhusu mtu kuja kutuvuruga kwa kisingizio kuwa anakipenda chama kuliko sisi. Tunalaani jitihada zote za wahuni na watu wasio na adabu ambao wamekuwa wakifanya hila za kutaka kusambaratisha chama.

  WANACHADEMA tunasimama imara na Mungu yupo upande wetu.

  Mhe Samson Mwigamba
  MWENYEKITI WA MKOA WA ARUSHA.
   
 2. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hizi trilioni mpaka ziishe kutapambazuka kwa tabu sana. Nilisha sema katiba ifuatwe kwani katiba inasemaje kiongozi akisaliti Chama? Mbona vikao vinakuwa vingi badala ya maamuzi. Kama ni kufukuzwa wafukuzwe au tukae kimya kama Magamba. Too much politics. Wamekosea wamekataa kurudi kwenye katiba waondoke.
   
 3. n

  nzom Senior Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Je tukiwafukuza hao saba tunaweza kutetea na je hayo maagizo mwisho lini
   
 4. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Magwanda bana kweli hamuishi kutapatapa, km ni kweli maafikiano yasainiwe na diwani wa TLP peke yake imekuwaje hawa wengine wa CDM wang'ang'anie vyeo na mpaka kamati maalum ikaundwa ?. Soma ripoti ya kamati ya kina Marando utajua ukweli wote
   
 5. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Wasiyo tii maagizo ya chama watimuliwe.Hapo tutajenga chama imara na bora
   
 6. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I concur with you comred Mwigamba, this is what we wanted. Kile kitendo cha kufoji sahihi ya viongozi wa juu wa CDM ni jibu tosha kabisa kwamba hakuna muafaka wowote uliofikiwa. Hatuogopi kwenda kwenye uchaguzi mdogo. Comred Samsoni Mwigamba ndiyo maana mimi hupenda sana kusoma makala yako Tanzania Daima. Kwa jinsi suala hili lilivyo kuna uwezekano bahasha ya JAIRO ilifanyakazi. Ngoja tusubiri tuone Trilioni 3 za huyo **** Shimbo, Mungu huwa hamfichi mnafiki.
   
 7. D

  Deo JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,191
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pendekezo hili liungwe mkono hata kama ni chungu.
   
 8. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 764
  Trophy Points: 280
  Wafukuzeni ndio mtajua kama mtaweza kutetea.
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Bora kutokuwa na madiwani kabisa kuliko kuwa na wasaliti....
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  watimuliwe tn haraka sn sbb ni wasaliti tn hawafai kwenye harakati za ukombozi wa nchi hii, nia yao c nzuri kwa wana arusha wafukuzwe cdm na wakabidhiwe kadi za ccm fasta
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  njaa kwakweli ndo inadumaza demokrasia hapa nchini, inawezekana kabisa hao madiwani 7 wamepewa mabahasha, ila bado hili sijalipa kipaombele kwa leo, bado akili zangu zipo kwa shimbo na trillion zaidi ya 3.
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  safi sana, muafaka gani hauna hata sharti moja. fukuza wote ngoma ianze upya, ni heri kutokuwa na madiwani kabisa kwa jinsi walivyo walafi hawa. wanageuza udiwani kama sehemu ya ajira hawafai kabisa
   
 13. F

  FUSO JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  Mimi naona ni sawa kwa CHADEMA wilaya nao kuja na maoni yako kwa ujumla - hatutaki kesho na keshokutwa watu wakahisi kwamba CC ya CDM imewaonea hawa madiwani.

  Lazima tuwe na kauli moja kwa pamoja, Tukiwashirikisha CDM Wilaya as well. Na pia ilikuwa vizuri hawa Madiwani wapewe haki ya kujitetea ndiyo sababu tukaunda Tume ya Marando.
   
 14. L

  Lua JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hakuna tamu lisilo na machungu, na hakuna mtu maarufu kwenye chama zaidi ya chadema kwa sasa. piga chini tusonge mbele c wakati wa kulambana miguu.
   
 15. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  haya ndiyo tuliokuwa tukiyasubiri,haiwezi kuwa na kugawana vyeo kirahisi rahisi tu.
   
 16. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hao madiwani kama wanashindwa kuheshimu viongozi wao fukuza tu.ni kweli wametupa wakati mgumu lakini potelea mbali.wacha wahamie ccm wapate utajiri.hao hawafai kuongoza uma.fukuzaaa!!
   
 17. Baba Collin

  Baba Collin JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  <br />
  <br />
  tunawafukuza muwachukue nyie magamba
   
 18. N

  Ngoks Member

  #18
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fukuza bila ya kukawia, fukuza haraka, tena haraka sana.
   
 19. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #19
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Wakuu,hili ni tamko baada ya mkutano mkuu wa wilaya,ambao ni viongozi wa kata zote,uliokuwa na ajenda ya kuridhia kujiuzulu kwa viongozi wa wilaya,na viongozi wa kata zote za Arusha mjini,wakaazimia kwa kauli moja kuwa madiwani wasaliti hawafai tena,na kamwe wasisamehewe tena,hii ni baada ya hawa madiwani wasaliti kutafuta wazee maarufu ili kwenda nao dodoma kwenye kikao cha kamati kuu kitakachofanyika jumamosi hii.Baada ya hali kuwa mbaya na shinikizo la nguvu ya umma kuwa kubwa wanaomba msamaha kwa chama
   
 20. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa madiwani kuwaamini tena ni ngumu maana wameonyesha usaliti mkubwa japokuwa walijitetea kuwa mwafaka ulikuwa wa halali pia waliipinga kamati je wataaminika katika chama na kwa nguvu ya uma?

  <br />
  <br />
   
Loading...