Taarifa Kwa Umma Kutoka Benki Kuu Ya Tanzania kuhusu NBC

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=1][/h]

Katika Gazeti la Business Times toleo nambari 1248 la Ijumaa, tarehe 10 Agosti 2012, ziliandikwa habari zenye kichwa cha habari chenye maana kuwa “Operesheni za NBC zawekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu”.

Katika habari hiyo ilielezwa kuwa Benki Kuu imechukua hatua hiyo kufuatia ripoti za tuhuma kadhaa zihusuzo udhaifu katika uendeshaji wa benki na utawala bora.

Benki Kuu inapenda kuchukua fursa hii kuueleza umma kuwa haijaweka operesheni/shughuli za NBC chini yake. Benki hiyo inajiendesha yenyewe kwa kufuata utaratibu wa Sheria za Makampuni, 2002, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha 2006 na miongozo itolewayo na Benki Kuu kama zilivyo benki zingine. Wateja wa NBC na Umma kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufanya biashara na benki hii kama kawaida.

IMETOLEWA NA BENKI KUU YA TANZANIA11AUGUST 2012
 
Inasikitisha Mkurungenzi Mkuu Mzalendo alifanya nini?
 
Ebwana ebu nifumbueni macho,ukiacha kufukuzwa kazi mafuru kuna nini kinaendelea hapo NBC?
 
Sasa tunaomba list ya management ya bot tafadhali

kwa nini bot wanafanya hii info siri kubwa?

Kwasababu labda hawataki kuichukuwa wataipa BAILOUT ili isife... kwahiyo ndio Maana wametangaza hawajaichukua

Sijui kaka yetu alizoa kiasi gani huko...
 
Nimekosa Imani na Serikali yangu kabisa na hivi ndivyo walivyokanusha kuwa Ebola haikufika TZ na sasa wanaumbuka mtu aliyepatikana MWZ na huo ugonjwa mkubwa wa mlipuko.
 
Magazeti ya kibongo bwana, aghhhh, sijui huwa yanapataga wapi habari zao
 
Huenda kuna shida huko NBC. Masuala ya kibenki ni very sensitive hivyo BOT wanakanusha hata kama kutakuwa na shida iwe kimya kimya kuepuka piblic punic.Nadhani wangetuambia sababu ya Mafuru kusimamishwa na ni nani anaongoza NBC. Uongozi katika masuala ya kibenki ni muhimu sana hivyo kuondolewa kwa CEO kunaashiria kuwa mambo si shwari hapo NBC.
 
My sentiments exactly.

Ila kama NBC haipo chini ya BOT (kama ilivyothibitishwa na BOT) hawawezi kuongelea sana mambo ya NBC with specifics.

Tunahitaji gazeti ama liombe radhi ama kuelezea zaidi chanzo cha habari zake na mfululizo mzima kwa kufuatisha tamko la BOT.
 
HATA MIMi nilishanga. Hii ni bank kubwa sana. Naina pesa zakutosha, acha azina ya dolari ina akiba kubwa sana ya fedha. Huyu mwandish lazima aombe radhi
 
My sentiments exactly.

Ila kama NBC haipo chini ya BOT (kama ilivyothibitishwa na BOT) hawawezi kuongelea sana mambo ya NBC with specifics.

Tunahitaji gazeti ama liombe radhi ama kuelezea zaidi chanzo cha habari zake na mfululizo mzima kwa kufuatisha tamko la BOT.

Wamelifungia gazeti la Mwanahalisi,nani mwingine atakayeweza kutupa ukweli bila kona kona?
 
Back
Top Bottom