Taarifa kwa Umma kuhusu upotoshwaji wa ugonjwa wa homa ya Dengue

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UPOTOSHWAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE

Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa mbalimbali za upotoshaji unaofanywa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii, simu za mikononi na mikusanyiko ya watu kuwa ugonjwa wa Dengue haupo nchini Tanzania.

Wizara inapenda kusisitiza kwamba, ugonjwa huo upo nchini na serikali kwa kushirikiana na wananchi inaendelea kutekeleza hatua mbalimbali za kukabiliana nao. Ikumbukwe ugonjwa huu unapatikana pia katika nchi nyingi duniani zilizoko katika ukanda wa joto na unaathiri takribani asilimia 40 ya watu duniani.Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinathibitisha kuwa takribani watu milioni 5 wanaripotiwa kuugua ugonjwa wa kila mwaka.

Wizara inasisitiza na kuikumbusha jamii kwamba hakuna dawa maalumu ya ugonjwa wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili zitakazo ambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengue


  • Kuangamiza mazalio ya mbu
    • Fukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia viuatilifu vya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
    • Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile: vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
    • Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
    • Hakikisha maua yanayo pandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
    • Funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara
    • Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama


  • Kujikinga na kuumwa na mbu
    • Tumia viuatilifu vya kufukuza mbu “mosquito repellants”
    • Vaa nguo ndefu kujikinga na kuumwa na mbu
    • Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (kwa wale wanaolala majira ya mchana na hasa kwa watoto)
    • Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi

Wizara inawakumbusha wananchi wa Tanzania kuwa, huu ni muda muafaka wa kuzingatia utunzaji bora wa mazingira yetu. Tukitunza mazingira yetu, nayo yatatutunza na kutuepusha na maradhi yanayoambatana na mazingira machafu.

Nsachris Mwamwaja
Msemaji wa wizara
23 mei 2014

 
Mbona kama Dengue ipo mbona kinga yake inatofautiana na maelezo ya awali. Kwanza taarifa zilisema mbu wa Dengue a.k.a Masharobalo hupenda maji masafi, sasa wizara inasema tufukie maji yaliyotuama. Pili Masharobalo hao huuma mchana, wizara inasema tutumie vyandarua au wataleta vya muundo wa miamvuli?

Kifupi hapa ni kupiga deal kwa kwenda mbele kama kikombe cha babu.
 
Serikali iache mzaa ifanye kazi ya kupulizia nchi mzima bil3 walizotumia kuondoa machinga Zingetumika kuua wadudu hawa masharobaro.
 
Dengue sio..? nyie tengeni fedha za kupambana na ugonjwa hatari dengue.. mjini mipango bana
 
Aliyesema haupo nani? hoja ni kwamba kama issue ni nguo fupi vipi watoto wa shule wanaovaa nguo fupi?
 
Haya ndiyo matatizo ya serikali kujiingiza kwenye mambo ya propaganda, sasa wananchi tumeshapoteza nao imani. Hata kama wakiwa serious tunajua ni propaganda tu hizo.
 
Our gvt has been corapted there is no serious issue let's people believe what their know
 
Hapa lengo wala si kutoa taarifa kwa umma,ni mpango wa kupiga hela siku chache zijazo. Hii ndo Tanzania bhaana!
 
TUMESHITUKA!!!! Mnataka kutusahaulisha tu kuhusu Katiba Mpya. NO WAY!!!! Kwanza, Katiba Mpya; Pili, Katiba Mpya; Tatu, Katiba Mpya; Nne, Katiba Mpya; Tano, Katiba Mpya; Sita, Katiba Mpya; Saba, Katiba Mpyaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!
 
Hapa ndipo sasa wananchi wajue jinsi serikali isivyilowajali wananchi wake.Serikali ipo tayari kutenga fedha kwa mambo yadiyokuwa na maana ili mradi yanawspa ulaji wa kifisadi,lakini hili ka ugonjwa hawapo tayari kabisa kutenga fedha za kununulia dawa za kuua hao wadudu kwenye majimaji nchi nzima,hawajali kabisa,mfe msife shauri yenu,kazi yao nikusema watanzania chukueni tahadhari!wao hamna kabisa kwani wanajua wskiugua na familia zao wao ni nje ya nchi.
Nikifikaga hapa huwa naumia sana,ninapoona watanzania wanakufa kwakukosa matibabu huku wakubwa wakila anasa bila kumjali mlipa kodi!Mungu na awalaani kabisa
 
Pamoja na kupiga noti mnakopiga ila waelimisheni watu watambue, na hiyo miavuli mtagawa bure au nayo Ni sili? Tuwekeni waxing basi
 
Ugonjwa unapatikana kwenye nchi za ukanda wa joto, na WHO imesema asilimia arobaini (40%) wanaathirika dunia nzima sasa hao watu milioni tano ndiyo asilimia arobaini ya world population au asilimia arobaini ya wanaoishi kwenye ukanda wa joto (NCHI KADHAA) ambako dengue inapatikana? Msemaji wa Wizara kajipange upya!
 

Attachments

  • 1400864178305.jpg
    1400864178305.jpg
    28.7 KB · Views: 520
Nimefukuzia ishu ya kuchapa tshirt na mabango nimeambiwa mambo itakuwa Ok!! Hebu punguzeni midomo kwanza kidogo tupige hela, kwani vyandarua si mlishagawiwa?? Mnataka nini tena? Ebo! Kesho semina ya kupambana na dengu, kesho kutwa warsha, next day kongamano!!!! Sitting allowance 50000 kwa siku, heheeeeee Idumu dengue
 
Nimefukuzia ishu ya kuchapa tshirt na mabango nimeambiwa mambo itakuwa Ok!! Hebu punguzeni midomo kwanza kidogo tupige hela, kwani vyandarua si mlishagawiwa?? Mnataka nini tena? Ebo! Kesho semina ya kupambana na dengu, kesho kutwa warsha, next day kongamano!!!! Sitting allowance 50000 kwa siku, heheeeeee Idumu dengue

idumu kwako pekee
 
Hawa Wapuuzi Tu Badala Ya Kuwajali Ma-Public Pealth Practitioners Waliosoma Prevention n Control Wanakomaa Na Madaktari!
 
Back
Top Bottom