Taarifa kwa Umma Kuhusu Mgomo wa Madaktari - CHADEMA

Watu kukosa huduma, kupoteza maisha na kuwa bila tiba ndio mnaona mafanikio? Ingekuwa dini yangu inaniruhusu kuwalaani basi nisingesita kuwaaambia madaktari waliogoma wamelaaniwa. Mlitaka nini zaidi ya Waziri Mkuu kuwaita na kuwasikiliza? na mkamdharau? Kama si laana hiyo ni nini? kama si kufungamana na siasa chafu ni nini? msijidai kujivuwa lawama baada yakuona maji yako shingoni.

Hamna haya wala hamjui vibaya, akili na matumbo yenu yako kwenye kula tu, na mtakuwa na uchu na njaa maisha yenu hata muwe mmeshiba vipi, vile vihela mnavyolazimisha kuhongwa na wagonjwa haviwatoshi? kuachiwa kufanya kazi za binafsi kwenye mahospitali na vituo vya afya vya binafsi hakuwatoshi? Wacheni kuona Watanzania wote ni wajinga.

Nasema Serikali iwahukumu wote kwa makosa ya jinai kwa kukosa kuripoti na kutoa huduma. Msiokuwa na haya wala msiojuwa vibaya.

fikra za huyu mtu huwa za kipunguani daima, kwanini yeye Pinda asiafuate Madaktari kule walipo, kazi yake ni kukaa ofisini tu , nyie watu mmelogwa ama ? wao ndio wenye shughuli, wanamtaka aje awasikilize, anaanza yeye kupanga masharti tena, ukialikwa wewe ndio unapanga ukumbi, umesoma shule lakini kalunguyeye wa akili
 
Sasa viongozi wa Chadema nao mnataka kuingilia vitu hata msivyovijua. ktk taarifa yenu mnaonyesha wazi kwamba MAT na TUGHE wameshindwa au wamekataa kuwapa nakala ya madai yao ili mpate kuyasoma na kujiunga nao ktk kutafuta njia za kutatua mgogoro huu. Sasa nashangaa chama kinapowaunga mkono madai yao na kuyaita HALALI wakati chama hakiyajui zaidi ya fununu na maelezo ya baadhi ya watu ktk vyombo vya habari. Kama chama hakijapokea taarifa kimaandishi hakiwezi kuchua msimamo bila kujua kwa sababu tu kinapingana na serikali.

Chama kinapinga POSHO za vikao, na kama mnawaunga mkono ina maana mnakubaliana na posho hizi kama zitatolewa kwa wote kama walivyopewa wabunge.. Jamani msimamo wa kiitikadi haubadiliki kama upepo Kama chama kinapinga matumizi mabaya ya serikali hakiwezi kwa njia moja kukubaliana na hoja ya kuongeza matumizi yasiyokubalika kitikadi kama Posho za vikao. Mwalimu anayewafundisha watoto chini ya mwembe, kusema kweli binafsi ndio namwita shujaa na Mzalendo wa kweli pamoja na kwamba Ufisadi umeshindikana.. Huu ndio moyo ninaoutafuta kutoka kwa wananchi na kama swala ni la kisiasa zipo njia ambazo CDM na vyama vya Upinzani wanaweza kabisa kuwakilisha bungeni na kujenga Upinzani wa kweli.

Kinachonishangaza ni kwamba wahudumu wa Hospital na wanesi ambao wanapata mshahara mdogo sana na wapo ktk mazingira mabaya zaidi ya madaktari wapo kazini na hakuna mtu anayewatetea. Na hali mbaya ya AFYA na ELIMU nchini inahusiana na vitengo ambavyo serikali imevikabidhi kazi hii, sasa ikiwa kweli chama kinataka kuona hali nzuri ya AFYA kwa nini kisitangulie na kupiga vita muafaka wa MoU.. hawa ndio wanahusika na mipango yote ya kiafya nchini na Artical 1 inajieleza wazi.. Kwa nini chama na wananchi wanamlalamikia JK wakati wanajua wazi kina nani wahusika..Hakuna hata mtu mmoja aliyeinua kidole na kuwanyooshea CSSC kwa sababu gani wakati mnakubaliana na madai ya Madaktari na walimu?..

Hapa ndipo tunapokutana na unafiki wa wananchi, wanajua kwamba mhusika ni ndani ya imani zao, lakini hawataki kukubali hivyo atafutwe bangusilo mwingine kulaumiwa. Ni wazi kabisa mfumo mzima wa ELIMU na AFYA unatakiwa kubomolewa bila kujali wahusika ni kina nani hasa ikiwa madai makubwa ya hawa madaktari ni mazingira mabaya ya kufanyia kazi. Na hakuna Mtanzania hata mmoja anakubaliana na mfumo wa Elimu na Afya nchini leo. Hali ni mbaya kupita maelezo na wapo wahusika ambao tunatakiwa kuwashambulia. Chombo kinachohusika na swala hiki ndicho kinatakiwa kutoa majibu na sio kila mtu kuogopa kukigusa chombo hiki kwa sababu ya imani zetu. Najua kwa nini JK analikimbia swala hili na viongozi wengi wanalitazama kwa jicho la woga lakini ifike mahala tufanye uchunguzi na tufahamu who is responsible na tuwatake wawe accountable kwa matatizo ya elimu na Afya nchini.

Kwa wana JF, Mtanichukia sana mwaka huu lakini imefika mahala tunataka Mabadiliko ktk Tanzania yetu. mfumo wa kiutawala uliotuongoza kwa miaka 50 haufai tumeshindwa na tukubali kushindwa hvyo tutafute mwanzo mpya toka hapa tulipo. Nchi inaonekana haina utawala, haina kiongozi wala system ya kiutawala ambayo makundi ya watu wanajichukulia mamlaka ya kuunda makundi sijui Boyz to Men na kadhalika..Nimechoka kuetetea makundi, nimechoka kuwa mshabiki wa vyama pasipo kuona ama kujua msimamo wa chama ktk maswala nyeti kama ELIMU, AFYA, UMEME, MAJI, USAFIRI na MAWASILIANO.. vyombo hivi ndivyo kati ya Commanding heights za uchumi wa nchi yoyote ktk maendeleo na hakuna nchi yoyote iliyoendelea ambayo imepwaya ktk mambo hayo. Huu ndio msingi na tusipoweza kuujenga vizuri na kuulinda bado tutaendelea kukwama hapa karne na karne.

For Change Tanzania...Nawaomba sana wana JF hasa wale Think tank au Great thinker kujiunga na - Change Tanzania ktk FB na Tweet...Tuondokane na mawazo ya mgando kufungiwa ktk makabati ya Udini na Ukabila..
 
Chadema acheni ushamba na ulimbukeni wenu wa kutaka kila hoja muigeuze kuwa ya kisiasa kumbukeni "Trade Unionism" huwa haingiliwi na Siasa!
 
Tunasubiri Madaktari wakimalizana na serikali. waje wengine, bila migomo mambo hayaendi kabisa.
 
Tukishaanza kuingiza uchama katika hii issue tumekwisha. Madai ya madaktari na maslahi ya watanzania yanayohusiana na afya yako hayaangalii itikadi za chama wala dini. Tukishaanza kuelekea huko basi tunaiua nguvu ya pamoja, kwa kuwa itaanza ile ya kwa kuwa mimi ni CHADEMA siko tayari kushare na CCM, au kwa kuwa mimi ni CCM siko tayari kuungana na CHADEMA katika kuicondemn serikali ambayo inaongozwa na Chana changu.
Guys are we not liquidifying the issue hapa?

Hebu tusimame kwa jina la Watanzania na si waCHADEMA, CUF wala CCM. After all wote tunategemea huduma sawa maana hakuna hospitali au madaktari wa wananchi walio CHADEMA, CCM au CUF ilmradi tu wa hali ya kawa basi wote tunatibiwa na hawa hawa waliogoma. Unless uko kwenye first class mnaopelekwa Apollo hata mkiumwa mafua.
 
Chadema nanyi hampitwi mshaanza kutafuta maujiko uchwara msisahau na masahani na mabakuli!!!
 
Serikali through statement ya jana kwenye TBC iliyotolewa na PM Pinda ilibadilisha swala lote hili kuwa la kisiasa. Kwanza PM Pinda alipoviagiza vyombo vya Dola viwazuie hawa madaktari wasikutane ni kuvunja haki za raia za kimsingi na katiba ya nchi. Pili Waziri Mkuu alipoanza kum- attack personally na professionally kiongozi wa Kamati ya Madaktari [Dr. Ulimboka] aliviolate fundamental rights za huyu jamaa. The Primeminister is a very senior official of the Government and when he embarks on a personal attack against an individual citizen using the massive powers of state [e.g. TBC] without following the due process then the opposition parties have to intervene. CHADEMA is therefore right in intervening in this saga at this point in time. The Government has goofed and turned a simple labour dispute into a political issue!
 
ukiona mtu anaanza viroja ujuwe hana hoja!

kwetu iringa fox ni mnyama ambaye anapenda sana kupandwa na madume mengi na hata hivyo huwa haridhiki. Sasa wewe faiza fox unawalaani madr. Umesahau kuwa kuna watu wanaiba sana hela ambazo zingesaidia kuwalipa madr. Na kuwahudumia wagonjwa si ndio hao walaaniwe ?
 
Sasa viongozi wa Chadema nao mnataka kuingilia vitu hata msivyovijua. ktk taarifa yenu mnaonyesha wazi kwamba MAT na TUGHE wameshindwa au wamekataa kuwapa nakala ya madai yao ili mpate kuyasoma na kujiunga nao ktk kutafuta njia za kutatua mgogoro huu. Sasa nashangaa chama kinapowaunga mkono madai yao na kuyaita HALALI wakati chama hakiyajui zaidi ya fununu na maelezo ya baadhi ya watu ktk vyombo vya habari. Kama chama hakijapokea taarifa kimaandishi hakiwezi kuchua msimamo bila kujua kwa sababu tu kinapingana na serikali.

Chama kinapinga POSHO za vikao, na kama mnawaunga mkono ina maana mnakubaliana na posho hizi kama zitatolewa kwa wote kama walivyopewa wabunge.. Jamani msimamo wa kiitikadi haubadiliki kama upepo Kama chama kinapinga matumizi mabaya ya serikali hakiwezi kwa njia moja kukubaliana na hoja ya kuongeza matumizi yasiyokubalika kitikadi kama Posho za vikao. Mwalimu anayewafundisha watoto chini ya mwembe, kusema kweli binafsi ndio namwita shujaa na Mzalendo wa kweli pamoja na kwamba Ufisadi umeshindikana.. Huu ndio moyo ninaoutafuta kutoka kwa wananchi na kama swala ni la kisiasa zipo njia ambazo CDM na vyama vya Upinzani wanaweza kabisa kuwakilisha bungeni na kujenga Upinzani wa kweli.

Kinachonishangaza ni kwamba wahudumu wa Hospital na wanesi ambao wanapata mshahara mdogo sana na wapo ktk mazingira mabaya zaidi ya madaktari wapo kazini na hakuna mtu anayewatetea. Na hali mbaya ya AFYA na ELIMU nchini inahusiana na vitengo ambavyo serikali imevikabidhi kazi hii, sasa ikiwa kweli chama kinataka kuona hali nzuri ya AFYA kwa nini kisitangulie na kupiga vita muafaka wa MoU.. hawa ndio wanahusika na mipango yote ya kiafya nchini na Artical 1 inajieleza wazi.. Kwa nini chama na wananchi wanamlalamikia JK wakati wanajua wazi kina nani wahusika..Hakuna hata mtu mmoja aliyeinua kidole na kuwanyooshea CSSC kwa sababu gani wakati mnakubaliana na madai ya Madaktari na walimu?..

Hapa ndipo tunapokutana na unafiki wa wananchi, wanajua kwamba mhusika ni ndani ya imani zao, lakini hawataki kukubali hivyo atafutwe bangusilo mwingine kulaumiwa. Ni wazi kabisa mfumo mzima wa ELIMU na AFYA unatakiwa kubomolewa bila kujali wahusika ni kina nani hasa ikiwa madai makubwa ya hawa madaktari ni mazingira mabaya ya kufanyia kazi. Na hakuna Mtanzania hata mmoja anakubaliana na mfumo wa Elimu na Afya nchini leo. Hali ni mbaya kupita maelezo na wapo wahusika ambao tunatakiwa kuwashambulia. Chombo kinachohusika na swala hiki ndicho kinatakiwa kutoa majibu na sio kila mtu kuogopa kukigusa chombo hiki kwa sababu ya imani zetu. Najua kwa nini JK analikimbia swala hili na viongozi wengi wanalitazama kwa jicho la woga lakini ifike mahala tufanye uchunguzi na tufahamu who is responsible na tuwatake wawe accountable kwa matatizo ya elimu na Afya nchini.

Kwa wana JF, Mtanichukia sana mwaka huu lakini imefika mahala tunataka Mabadiliko ktk Tanzania yetu. mfumo wa kiutawala uliotuongoza kwa miaka 50 haufai tumeshindwa na tukubali kushindwa hvyo tutafute mwanzo mpya toka hapa tulipo. Nchi inaonekana haina utawala, haina kiongozi wala system ya kiutawala ambayo makundi ya watu wanajichukulia mamlaka ya kuunda makundi sijui Boyz to Men na kadhalika..Nimechoka kuetetea makundi, nimechoka kuwa mshabiki wa vyama pasipo kuona ama kujua msimamo wa chama ktk maswala nyeti kama ELIMU, AFYA, UMEME, MAJI, USAFIRI na MAWASILIANO.. vyombo hivi ndivyo kati ya Commanding heights za uchumi wa nchi yoyote ktk maendeleo na hakuna nchi yoyote iliyoendelea ambayo imepwaya ktk mambo hayo. Huu ndio msingi na tusipoweza kuujenga vizuri na kuulinda bado tutaendelea kukwama hapa karne na karne.

For Change Tanzania...Nawaomba sana wana JF hasa wale Think tank au Great thinker kujiunga na - Change Tanzania ktk FB na Tweet...Tuondokane na mawazo ya mgando kufungiwa ktk makabati ya Udini na Ukabila..

Change Tanzania ni ya watoto wa wakubwa akina Maria sarungi na Mike Bomani ambao kwanza hamuijui Tanzania vizuri zaidi ya kukaa Ulaya hata ukiangalia FB na Twitter mnaweka vitu vya kitoto zaidi
 
Change Tanzania ni ya watoto wa wakubwa akina Maria sarungi na Mike Bomani ambao kwanza hamuijui Tanzania vizuri zaidi ya kukaa Ulaya hata ukiangalia FB na Twitter mnaweka vitu vya kitoto zaidi
Haya ndio mawazo mgando, sasa ikiwa watoto wa wakubwa ndio unashindwa kuchangia. Wewe mwenye mawazo ya kikubwa huoni kama unatakiwa zaidi kuonyesha ukubwa wako?.. Changia mawazo mbona utoto upo sana hapa JF...hata mimi sijachangia lakini nimewasoma watu wengi sana wakielezea matatizo yetu na nakusanya mawazo mazuri kuielewa Tanzania yangu. Kuishi Dar au Mwanza pekee huwezi kufahamu matatizo ya Kitaifa na nini maendeleo zaidi ya yale uloyaona ama kuyasikia. Ni sawa na kipofu anayetaka kujua ukubwa wa Tembo.

Mkuu, tumetawaliwa kwa miaka 50 wananchi hatujawahi kupewa nafasi ya kuchangia mawazo yao na chombo kidogo kama hiki kinaweza kabisa kuunda kundi lenye nia ya kupata mabadiliko wakati hapa JF tunakusanya Ushabiki na unazi zaidi. Binafsi siwezi kuwaunga mkono madaktari kwa hoja ambazo sizifahamu vizuri na nyingine sikubaliani nazo.. Mwana Chadema anayeunga mkono posho za madaktari kwa sababu tu wabunge wamepewa ni mnafiki wa nafsi yake mwenyewe. - Pinga Posho hadi kieleweke!..
 
Ni karibu wiki sasa toka sakata la mgomo wa madaktari na serikali lishike kasi. Tumesikia jinsi pande mbili hizi zilivyojibishana na hatimaye jana PM Pinda akahitimisha kwa agizo alilolitoa akitaka madaktari walitekeleze. Kinachonisikitisha sijasikia vyama vya upinzani vyote tulivyonavyo vinasema nini juu ya hili suala wakati wapiga kura wao wakiteseka kwa kukosa matibabu. Au ni katika kuhofia kupoteza ongezeko la posho ya kikao?? Jamani wabunge kama kweli mpo hapo kutokana na kura zetu, basi naomba muilazimishe serikali kuumaliza mgogoro huu ndani ya masaa 12 tu kuanzia kesho saaa moja asubuhi.
 
Hakukuwa na kusitasita....bali MAT, Kamati ya kuratibu mgomo, pamoja na wagomaji wenyewe (maDaktari) hawakutaka mgomo huo uhusishwe na chama chochote cha siasa, bali mgomo huru wa wanataaluma ya afya usiofungamana na itikadi yoyote ya siasa wala imani yoyote ya kidini! Na kwa mafanikio ya mgomo huo, tunaomba iendelee hivyo...

mkuu hii ni kweli kabisa
 
Kuna watu hawapendi kuona mazuri ya CDm kwanza niwapongeze madaktari kwa kugoma
pili niwapongeze cdm kwani walitoa onyo mapema kabla hata madaktari kugoma
Tatu WATANZANIA BADILIKENI SISIEM inatupeleka pabaya!
 
fikra za huyu mtu huwa za kipunguani daima, kwanini yeye Pinda asiafuate Madaktari kule walipo, kazi yake ni kukaa ofisini tu , nyie watu mmelogwa ama ? wao ndio wenye shughuli, wanamtaka aje awasikilize, anaanza yeye kupanga masharti tena, ukialikwa wewe ndio unapanga ukumbi, umesoma shule lakini kalunguyeye wa akili

haaah haaaah mkuu huyu bibi atakua na taaluma ya uchawi!
 
Tunasisitiza umma uzingatie kwamba tangu Mwalimu Nyerere aondoke madarakani mwaka 1985, Serikali ya CCM imeongeza wingi wa majengo mbalimbali kwenye sekta ya afya hata hivyo imeshindwa kusimamia utoaji bora wa huduma za afya katika zahanati, hospitali na vituo vya afya. Kutokana na mfumo mbaya wa usimamizi wa sekta ya afya, misingi imara ya kuimarisha sekta ya afya iliyowekwa baada ya uhuru imevunjwa na kubomolewa ikiwemo katika masuala yanayohusu kujali maslahi ya watumishi wa umma katika sekta hii muhimu.

Hali hii imefanya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa na nakisi ya watumishi asilimia 48% na takwimu zinaonesha kuwa 18% ya wafamasia, 15% ya madaktari, 13% ya madaktari wasaidizi waliacha vituo vyao vya kazi na kwenda kutafuta kazi kwenye mashirika ambayo yanalipa mishahara mikubwa na mizuri. Nakisi hii itaongezeka zaidi iwapo madai ya msingi ya madaktari na watumishi wengine hayatashughulikiwa na serikali itaendelea kuchelewa kushughulikia migogoro na migomo mingine inayoendelea
Lengo la mfumo uliopo ni kuua serikali kuendesha Elimu na AFYA ili ku - privatize AFYA na ELIMU na ndio maana tumefikia matatizo haya. hayakutokea kwa bahati mbaya bali yamepimwa na kupangwa hadi tumefika hapa tulipo..Maswala ya Umeme mbali na rais au wizara huwa tunawalalamikia Tanesco, Maji - Dawaso... Je Afya na Elimu tuwalalamikie nani?.
 
Back
Top Bottom