Taarifa kwa Umma Kuhusu Mgomo wa Madaktari - CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa Umma Kuhusu Mgomo wa Madaktari - CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mike Mushi, Jan 30, 2012.

 1. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tangu kuanza kwa mgomo wa madaktari nchini, wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi wamekuwa wakitoa rai kwa viongozi mbalimbali wa Chama Cha Demokrasia CHADEMA (CHADEMA) kuingilia kati mgogoro unaoendelea baina ya madaktari na Serikali.
  Tarehe 25 Januari 2012 Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilitoa taarifa kwa umma kueleza kwamba chama kiliguswa na mgomo uliokuwa ukiendelea nchini na kueleza masikitiko kuhusu udhaifu wa serikali katika kushughulikia kwa wakati madai ya madaktari nchini.

  Katika taarifa hiyo tulieleza kwamba kwamba uzembe na ufisadi katika serikali kwenye sekta ya afya unaligharimu taifa na maisha ya wananchi. Hivyo, CHADEMA kikaitaka serikali kukamilisha kwa haraka majadiliano na madaktari ili kuepusha madhara zaidi kwa umma.

  Katika taarifa hiyo, CHADEMA iliwapa pole wananchi ambao wameathirika na migomo inayoendelea na kuzingatia kwamba mgomo huo umesababishwa na udhaifu katika serikali. Aidha, pamoja na migomo inayoendelea CHADEMA kilitoa rai kwa madaktari na watumishi wengine wa umma kuhakikisha maisha ya wagonjwa walio katika hali ya hatari yanaokolewa.

  CHADEMA ilieleza kuwa iwapo serikali haitachukua hatua za haraka kutatua mgogoro unaoendelea na kushughulikia madai ya wafanyakazi wa sekta ya afya, viongozi wakuu wa CHADEMA watatoa tamko kuhusu hatua za ziada ambazo chama kitachukua ili kuhakikisha kwamba umma hauendelei kupata madhara kutokana na udhaifu wa serikali.

  Pamoja na taarifa hiyo viongozi wakuu wa chama na kambi rasmi ya upinzani inayoongozwa na CHADEMA wamefanya mawasiliano kati ya tarehe 23 na 29 Januari 2012 na viongozi wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) na kamati ya mpito ya mgomo wa madaktari ili kupatiwa nakala ya madai ya madaktari na kuweza kutimiza wajibu wa chama na kambi rasmi ya upinzani bungeni katika kushughulikia vyanzo vya mgogoro huo.

  Mwenyekiti wa chama Mh. Freeman Mbowe kwa nafasi yake kama kiongozi wa upinzani bungeni tarehe 27 Januari 2012 aliwasiliana na viongozi wa kamati ya mpito ya madaktari ili kupokea madai yao kuweza kulinganisha na masuala ambayo tayari kambi rasmi ya upinzani iliyawasilisha bungeni kuhusu haja ya serikali kuboresha maslahi ya watumishi wa umma katika sekta ya afya.

  Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa kwa niaba ya chama aliwasiliana na viongozi wa Chama Cha Madaktari (MAT) kwa ajili ya kupatiwa nakala ya nyaraka za madai husika kwa nyakati mbalimbali.

  Kutokana na kusitasita kwa viongozi wa MAT na kamati ya mpito ya mgomo wa madaktari kutoa ushirikiano unaostahili ili chama na kambi rasmi ya upinzani, CHADEMA kilivuta subira ili kukamilisha mawasiliano husika kuweza kuisimamia serikali kuhusu mgogoro huu.

  CHADEMA kinatoa mwito kwa TUGHE, MAT na kamati ya mgomo wa madaktari kutoa ushirikiano unaostahili kwa chama, kambi rasmi ya upinzani na wadau wengine ili kuweza kuunganisha nguvu ya pamoja katika kushughulikia madai ya msingi ya madaktari yenye kuathiri sekta ya afya nchini na maisha ya wananchi kwa ujumla.

  Kwa upande mwingine, CHADEMA hakijaridhishwa na maelezo yaliyotolewa na serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu namna ambavyo imeshughulikia mgogoro huu na madai ya madaktari, watumishi wengine wa umma katika sekta ya afya nchini pamoja na uboreshaji wa huduma katika hospitali, zahanati na vituo vya afya nchini. Aidha, CHADEMA kinamtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na serikali kwa ujumla kuacha vitisho na matumizi makubwa ya vyombo vya dola kwa madaktari na makundi mengine katika jamii yanapotumia uhuru wa kikatiba kwa kukusanyika, kujadiliana na kuhoji kuhusu uwajibikaji wa serikali na viongozi wake kwa kuzingatia ibara za 8, 18 na 20 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  CHADEMA kinarudia kutoa rai kwa wananchi kuendelea kuunga mkono madai ya msingi ya madaktari ili kuhakikisha kwamba hospitali za umma nchini zinakuwa mahali salama kwenye huduma bora za kulinda maisha ya wananchi hususan wasio na uwezo wa kudumu gharama za matibabu katika hospitali binafsi za ndani na nje ya nchi. Pamoja na madai ya maslahi ya madaktari ambayo ni kwa maslahi ya umma, madaktari wanataka pia serikali ichukue hatua za kuboresha huduma za afya. Serikali inaingia gharama kubwa kupeleka baadhi ya watanzania wengi wao wakiwa viongozi kwenda kutibiwa nje ya nchi huduma katika hospitali za umma zinazidi kuzorota kutokana na ukosefu wa madawa, vifaa tiba na wataalamu wa kutosha katika hospitali za umma. Aidha, serikali inashindwa kuipa kipaumbele sekta ya afya kwa kisingizio cha kutokuwa na uwezo wakati ambapo inafanya matumizi mengine ya anasa kwa kiwango kikubwa kama ilivyokuwa katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru. Serikali inashindwa kushughulikia madai ya posho za madaktari kama nyongeza ya posho ya kulala kazini (on call allowance) na posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (risk allowance) wakati huo huo serikali hiyo hiyo inazungumzia nyongeza ya posho za vikao kwa wabunge.

  Chama kimewasiliana na kimeitaka kambi rasmi ya upinzani bungeni inayoongozwa na CHADEMA kufanya uchambuzi wa kina kuhusu maelezo hayo na kutumia njia za kibunge katika kuisimamia serikali kushughulikia migogoro kati yake na madaktari, maslahi ya watumishi wa umma katika sekta ya afya pamoja na uboreshaji wa huduma katika hospitali, zahanati na sekta ya afya nchini.

  Viongozi wakuu wa CHADEMA watatoa tamko kuhusu hatua za ziada ambazo chama kitachukua ili kuhakikisha kwamba umma hauendelei kupata madhara yatokanayo na udhaifu wa serikali katika sekta ya afya nchini iwapo serikali haitachukua hatua zinazostahili kuzingatia maoni yanayoendelea kutolewa na kambi ya upinzani katika nyakati mbalimbali.

  CHADEMA kinarudia tena kutoa mwito kwa serikali inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete kurejea mapendekezo yaliyotolewa na chama kupitia tamko la Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kuhusu mwelekeo wa taifa kwa mwaka 2012 kwamba Kipaumbele kikuu cha Kijamii kiwe kushughulikia vyanzo vya migogoro katika maeneo mbalimbali badala ya kukabiliana na matokeo.

  Iwapo serikali ingezingatia msingi wa tamko hilo ambalo linapatikana kupitia www.chadema.or.tz; mgogoro huu kuhusu madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya na serikali usingefikia hatua ya kuleta madhara kwa wananchi.

  Tunasisitiza umma uzingatie kwamba tangu Mwalimu Nyerere aondoke madarakani mwaka 1985, Serikali ya CCM imeongeza wingi wa majengo mbalimbali kwenye sekta ya afya hata hivyo imeshindwa kusimamia utoaji bora wa huduma za afya katika zahanati, hospitali na vituo vya afya. Kutokana na mfumo mbaya wa usimamizi wa sekta ya afya, misingi imara ya kuimarisha sekta ya afya iliyowekwa baada ya uhuru imevunjwa na kubomolewa ikiwemo katika masuala yanayohusu kujali maslahi ya watumishi wa umma katika sekta hii muhimu.

  Hali hii imefanya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwa na nakisi ya watumishi asilimia 48% na takwimu zinaonesha kuwa 18% ya wafamasia, 15% ya madaktari, 13% ya madaktari wasaidizi waliacha vituo vyao vya kazi na kwenda kutafuta kazi kwenye mashirika ambayo yanalipa mishahara mikubwa na mizuri. Nakisi hii itaongezeka zaidi iwapo madai ya msingi ya madaktari na watumishi wengine hayatashughulikiwa na serikali itaendelea kuchelewa kushughulikia migogoro na migomo mingine inayoendelea.

  Serikali ya CCM irejee ilani ya CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kifungu cha 3.3 ambapo chama kimeeleza bayana namna ambavyo serikali inaweza kuongeza mishahara kwa watumishi wa sekta ya afya ili kuweza kuwavutia wataalamu kubakia nchini badala ya kwenda kugoma au kwenda kutafuta kazi nje ya nchi kutokana na malipo mazuri huko.

  Aidha, katika ilani hiyo CHADEMA imeeleza bayana kwamba ipo haja ya malipo ya mazingira magumu kutolewa kwa watumishi wa afya wanaofanya kazi katika maeneo na kada maalum.

  Pia, serikali izingatie maoni yaliyotolewa na kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu sekta ya afya ili kuweza kuepusha migogoro na pia muendelezo wa upatikanaji wa huduma mbovu za afya katika hospitali, zahanati na vituo vya afya nchini kwa manufaa ya umma.

  Imetolewa tarehe 30 Januari 2012 kwa niaba ya CHADEMA na:

  John Mnyika (Mb)
  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Hakukuwa na kusitasita....bali MAT, Kamati ya kuratibu mgomo, pamoja na wagomaji wenyewe (maDaktari) hawakutaka mgomo huo uhusishwe na chama chochote cha siasa, bali mgomo huru wa wanataaluma ya afya usiofungamana na itikadi yoyote ya siasa wala imani yoyote ya kidini! Na kwa mafanikio ya mgomo huo, tunaomba iendelee hivyo...
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hivi hakuna namna nyingine ambayo Chadema wanaweza wakafanya zaidi ya kutoa tamko tu? I think there is another alternative.
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  nawashauri chadema wakae mbali kabisa na huu mgomo wa madaktari ili kukwepa lawama zisizo na ulazima
   
 5. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu nashukuru kwa kuliona hilo
   
 6. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Mimi nadhani MAT walifanya uamuzi wa busara kutojihusisha na chamba chochote. Mgomo huu ni wa wanataaluma, hauna itikadi yoyote..CHADEMA acheni ku-capitalize katika kila ishu.
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Well it is the issue that need scrutiny from more bodies, CDM being one of them. I am not sure which would have been a good approach, spreading these demand or enclosing the same.
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Give us your thought. The only way CDM can make Doctors back to work is to accept their demand. CHADEMA can accept Doctors demand if they have ability to Tax and use the tax to implement their policies. CHADEMA can only have ability to tax and use Tax if they form a government of Tanzania. For CHADEMA to form a Govt they sould first be given mandate to form a government by people. Lets Vote CHADEMA in 2015 and the we can find if they will be able to implement their policies. The Govt in power failed Tanzanians, we need to give them notice that if they are not going to change, 2015 will be hard for them to Chakachua as usual.

  For the time being the only thing CDM can do as a political party out of power is telling people what they would do if the run a government. The burden to prove them wrong relies on the party in power by doing the otherway round and make the health sector in Tanzania stronger than ever. I am afraid that the path they are now taking will lead into a decline of the sector.
   
 9. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #9
  Jan 30, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwanza ninashukuru Mnyika na Idara yake ya uenezi kwa kuwa very proactive.
  Pili, Chadema kutoa kauli ni muhimu sana, wengi wanataka kusikia maoni ya Chama. statement hii imekaa vizuri sana.
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Chadema sasa hivi mtalikoroga
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  kama kweli Chadema walikuwa na nia nzuri wangeanza kufutilia issue hii kabla ya madaktari hawajagoma, kuhijack hoja si vizuri. Kuna wengine wengi tu wana matatizo hayo, wawasemee basi, sio kusubiri mpaka wameamua kugoma. Siungu mkono kupoliticize mgogoro wa madaktari na serikali.
   
 12. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huna tofauti na mpishi wa makuli
   
 13. M

  Makupa JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Baada ya tamko kinachofuatia ni nini
   
 14. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #14
  Jan 30, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hakuna walichokosea.
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Jan 30, 2012
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  CHADEMA mmetoa tamko ni vema lakini tunataka hatua zaidi ambazo ni pamoja na kuishitaki serikali kwa mauaji ya wagonjwa wasio na hatia waliokufa wakiwa langoni mwa hospitali bila huduma.
   
 16. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hebu soma hapa vizuri
  them, Ukiangalia tamko, linasema CHADEMA walitaka kujua hasa tatizo ni nini na madai ni yepi iliwaweze ku-push bungeni kwa kupitia kambi rasmi ya upinzani bungeni. Kama wangeona madai yao hayana maana, wangejua la kufanya.

  Mkuu, watu wanataka CHADEMA ifanye mambo, wakati jamaa wanabwabwaja bungeni kuhusu haya mambo na potentiality ya eruption ya migogoro kutokana na mazingira duni na maslahi duni ya wafanyakazi, nobody listen to them.

  Sasa hivi walikuwa wanajaribu to get into the bottom of it, so that wajue jinsi ya kusaidia kutokea bungeni, watu wanalalama.

  Hatuwezi kuendelea kwa design hii, never.
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  meat head...........umeweza kusoma hilo tamko? au uvivu tu ndo unakusumbua.
   
 18. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #18
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hivi unajua maana ya chama kikuu cha upinzani au una payuka tu...
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Jan 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii statement ya CHADEMA inawakata miguu wale wote waliokuwa wanakimbilia kuunganisha huu mgomo na CHADEMA. Kumbe hawa wandugu wadunga sindamo vichwa vimepata moto. Crying wolf, not!
   
 20. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #20
  Jan 30, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  ni kwenda kwa wananchi na kuwajulisha kinachoendelea..watakacho kiamua wananchi ndicho tutakacho kifanya...Vipi Kikwete kasha rudi au bado ana kula bata
   
Loading...