Kama tunavyofahamu, nchi yetu ina aina mbalimbali za nyoka ambao pindi wakimuuma mtu huleta madhara mbalimbali ya kiafya. Aidha tunafahamu kwamba tatizo hili lipo zaidi katika maeneo ya vijijini ambako uwezo wa wananchi kumudu gharama za matibabu ni mdogo.
Dawa za kutibu sumu ya nyoka huagizwa kutoka nje ya nchi. Dawa hizo siyo tu hazipatikani kwa urahisi, bali pia zinapatikana kwa gharama kubwa. Bei ya kununulia dawa hizi ni kati ya dola za kimarekani 55 hadi 85 (yaani shilingi za kiTanzania 118,250 hadi 182,750) kwa kichupa kidogo (vial) kimoja. Kichupa hicho huweza kutumika kwa wagonjwa wanne, lakini mara tu baada ya kufunguliwa dawa hiyo huwa haifai tena kutumika ndani ya mwezi mmoja tu
Kwa uzoefu wangu wa miaka mingi kudeal na masuala haya ya kuumwa na nyoka wenye sumu tatizo kuu ni muda, muda mala zote hautoshi kukabiliana na adha hii hasa kwa nyoka wenye sumu, muda ni kidogo mno. Kwa wahanga wakubwa kwa kuumwa na nyoka wenye sumu ambao ni:-
1. Wakata mbao za mininga mapoli ya Tabora
2. Wawindaji hasa wawindaji wa nungunungu
3. Wakata kuni
4. Wakulima wa jembe la mkono
Watu hawa kutoka eneo walilopatia dhahama mpaka kufika kwenye matibabu muda huwa hauwatoshi mala zote hufia njiani.
Mfano Bibi harusi wa kijiji kimoja wilaya ya Sikonge alikuwa amepakiwa na baiskeli na bwana harusi nyoka akatoka kwenye mti akamgonga alikufa baada ya dakika 10, wahusika wa sherehe wakitokea nyuma kufika eneo la tukio bibi harusi aliisha kufa zamani.
My take:
Hospitali za wilaya na mikoa na sehemu zingine kama huwa wanaagiza dawa kwa kutumia kanuni ya VIN ( Vital,Impontant,Non impontant) ASV waiweke kwenye gurupu la Non important kwa sababu nyoka wengi maeneo ya majumbani hawana sumu utakuta nyuki wana sumu zaidi kulika nyoka kwa hiyo mtu kama huyo kumpa ASV ni kupata gharama za bure tu, halafu watu kama hao ni hasara kuwapa ASV kuliko faida.
Kwa wenye kuhitaji ASV kiukweli they don't have a chance labda washauriwe waweze kuzinunua na kwenda nazo porini halafu wafundishwe na namna ya kuzitumia ambapo ni rahisi sana .