Taarifa kwa Umma: Kanusho la Taarifa za uzushi kuhusu afya ya Mzee Mwinyi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
TAARIFA KWA UMMA KUKANUSHA TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU AFYA YA MZEE MWINYI

Dar es Salaam,

Ijumaa, Februari 24, 2017:

Kumekuwa na habari zinazoenea na kujirudia sana katika mitandao ya kijamii kuhusu hali ya afya ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi. Taarifa hizo ambazo hazieleweki lengo lake, zimekuwa zikidai kuwa Mzee Mwinyi amefariki dunia.

Tutautaarifu umma kuwa habari hizo si za kweli, ni za kupuuzwa. Mzee Mwinyi ni mzima wa afya, anaendelea na majukumu yake kama kawaida ambapo jana Alhamisi amehudhuria chakula cha jioni kuadhimisha siku ya Taifa la Kuwait na leo mchana alitarajiwa kwenda kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya.

Natumia fursa hii kuendelea kuwakumbusha watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa waliobuni teknolojia hii walikuwa na malengo adhimu ya kumpatia mwanadamu uwanja na uwanda mpana wa mawasiliano tusiwachezee wabunifu hao kwa kuitumia kinyume cha malengo.

Aidha, jamii ifahamu kuwa ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni, 2015, kwa mtu yeyote kutangaza, kuchapisha na kueneza habari za uongo au uzushi katika mitandao.

Kwa niaba ya Serikali nachukua fursa hii kuwapa pole familia ya Mzee Mwinyi na watanzania wengine kwa mshtuko walioupata kutokana na uzushi huu. Katika hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhusika na uhalifu huu.

Imetolewa na:
Dkt. Hassan Abbasi
Mkurugenzi, Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali

mwinyi.jpeg
 
Naona watu bado hawajaelewa sheria ya makosa ya Mtandao inavyofanya kazi. Inakuwaje mtu mzima na akili yako uanzishe uzushi kama huo? Kwa faida gani hasa? Ni ajabu kabisa1
 
Naona watu bado hawajaelewa sheria ya makosa ya Mtandao inavyofanya kazi. Inakuwaje mtu mzima na akili yako uanzishe uzushi kama huo? Kwa faida gani hasa? Ni ajabu kabisa1
na mtu kama huyo alichukuliwa hatua za kisheria analalama kuwa serikali inaonea kumbe vitu vingine tunatafuta wenyewe!!!
 
Ni mzima wa afya anaendelea na majukumu take kama kawaida ambapo jana Alhamisi amehudhuria chakula cha jioni kuadhimisha siku ya taifa la Kuweit.
 
Badala ya kukanusha mngempa airtime hata ya kupanda basi la mwendokasi akashuke ubungo bus terminal ashuhudie ukaguzi wa magari ukiongozwa na kamanda Mpinga kisha alishukuru jeshi la polisi kwa kusimamia sheria ya udhibiti wa mwendo kasi wa magari.

HII HABARI YA KUTUKUMBUSHIA SHERIA YA MAKOSA YA KWENYE MITANDAO HAIJAKAA VIZURI SANA.
KWA MAANA INAFANANA MTU AZUIE MATUMIZI YA VISU KWA KUWA KUNA MJINGA MMOJA KAMUUA MWENZIE KWA KUMCHOMA KISU.
 
Yaani watu wengine sijui ni wa aina gani..!? Uzushi wa kifo kwa mzee huyu maana yake nini.?
 
ndio kwanza nazisikia kwako, hivi kuna mtandao mwingine zaidi ya huu wa jamii forum??
 
kila nikiangalia kwenye mitandao ya kijamii kuwa mzee mwinyi ameaga dunia... nimesoma magazeti sioni. mwenye nchi hakutangaza taarifa hizo.hivi ni kweli naomba kujuzwa kama ni kweli
 
Siyo jambo dogo hili ndugu, hii ni hazina iliyobakia kwa Taifa letu, ingawa yapo mengi wameshindwa ama kuogopa kukemea.
 
Back
Top Bottom