Taarifa kwa umma:dawa bandia ya malaria iitwayo eloquine

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
wakuu tuwe waangalifu na tutoe taarifa kwa mamlaka husika....
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KUHUSU UWEPO WA DAWA BANDIA YA KUTIBU UGONJWA WA MALARIA IITWAYO ELOQUINE (Quinine Sulphate 300mg USP)

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni wakala wa Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti ubora, ufanisi na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii.
TFDA inapenda kuutaarifu umma kuwa imebaini kuwepo kwa dawa bandia ya kutibu ugonjwa wa Malaria katika soko. Dawa hiyo inaitwa Eloquine (Quinine Sulphate 300mg U.S.P) na ipo katika makopo ya vidonge 1000 (elfu moja) kila moja. Maelezo yaliyopo katika lebo yanaonesha kuwa dawa hiyo imetengenezwa na kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd cha nchini Kenya.
Hata hivyo, TFDA imebaini kuwa kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd hakitengenezi dawa yenye jina la biashara la ‘ELOQUINE’. Kiwanda hicho kimesajili Tanzania Quinine Sulphate 300mg B.P isiyo na jina la kibiashara. Aidha, kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd kimebainisha tofauti mbalimbali zilizopo katika lebo ya dawa bandia ikilinganishwa na dawa halisi inayotengenezwa na kiwanda hicho iliyosajiliwa na TFDA na hivyo kuthibitisha kuwa kiwanda hicho hakitengenezi dawa hiyo.
Katika kudhibiti usambazaji wa dawa hiyo hapa nchini, hadi sasa TFDA imekamata jumla ya makopo 155 ya dawa hiyo bandia ya Eloquine jijini Dar Es Salaam yaliyokuwa yakisubiri kusambazwa. Aidha, kopo moja lenye vidonge 115 limekamatwa Moshi, Kilimanjaro. Tayari mtuhumiwa mmoja amekwishafikishwa mahakamani na upelelezi wa chanzo na wasambazaji wa dawa hii unaendelea kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Uchunguzi wa dawa bandia katika maabara umebaini kuwa vidonge hivyo havina kiambato hai (active ingredient) cha Quinine Sulphate kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Malaria na hivyo matumizi yake ni hatari kwa afya ya binadamu.
Maelezo ya kina yanayotofautisha dawa halisi iliyosajiliwa na dawa bandia ni kama yalivyoainishwa katika jedwali hapa chini.
Dawa halisi iliyosajiliwa

Maelezo ya dawa bandia
Jina la dawa: Quinine Sulphate 300mg B.P
Jina la biashara: Haina jina la biashara
Mtengenezaji: Elys Chemical Industries Ltd, Road B, Off Enterprise Road, P.O Box 40411, 00100 Nairobi, Kenya
Rangi ya Lebo: Nyeupe na kahawia (Brown)
Namba ya toleo: Huanzia na namba na siyo herufi. Kwa mfano: 2167E
Muda wa matumizi (Shelf life): Miaka 4
Jina la dawa: Quinine Sulphate 300mg U.S.P
Jina la biashara: ELOQUINE
Mtengenezaji: Elys Chemical Industries Ltd, Road B, Off Enterpises Road, P.O Box 4011 00100 Nairobi, Kenya
Rangi la Lebo: Njano na Nyekundu
Namba ya toleo: GE410
Tarehe ya kutengenezwa: 04/2009
Tarehe ya mwisho wa matumizi: 4/2014 (Miaka 5)

Wafanyabiashara wote wa dawa na wananchi wanatahadharishwa kutozitumia dawa hizi na wale wote waliouziwa dawa hizi wanaelekezwa kuzirudisha dawa hizo katika ofisi za TFDA, vituo vya afya vya Serikali au vituo vya polisi vilivyo jirani nao.
TFDA inapenda pia kuwakumbusha wafanyabiashara wa dawa, wasafirishaji wa vifurushi na wananchi kutoa taarifa haraka iwezekanavyo pale wanapohisi kuuziwa dawa duni, bandia au zilizoisha muda wa matumizi. Taarifa zitolewe ofisi za TFDA makao makuu zilizopo Barabara ya Mandela, EPI Mabibo External, Dar es Salaam na Ofisi za Kanda zilizopo mtaa wa Nkurumah, Mwanza, Mtaa wa Sakina – Arusha, Hosptali ya mkoa ya Dodoma na Jengo la Ofisi ya Mifugo Mkoa wa Mbeya.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:-

MKURUGENZI MKUU

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA

EPI MABIBO EXTERNAL,

S.L.P 77150, DAR ES SALAAM

Simu: + 255 222 450512/450751/452108

Nukushi: + 255 222 450793

Barua pepe: info@tfda.
 
Asante kwa taarifa lakini nadhani imefika wakati sasa tasisi husika ziwe serious kwenye kushughulika na masuala haya. Suala la sawa bandia halijaanza leo, lakini sijawahi kusikia hata mtu mmoja akiewa adhabu kali kutokana na kuchezea maisha ya watu kwa kutengeneza au kuuza dawa bandia. Kwangu mimi, mtu anapokamatwa na dawa hizo bandia, sidhani kama unahitajika ushahidi mwingine tena kumfanya mtu huyo awe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo. lakini kisl siku wanakamatwa na wala sijui wanaishia wapi!
 
sijui kama muhindi hatahusika hapa.india ni baba wa counterfeit drugs
 
TFDA wanafanya nini? kazi yao ni nini mpaka vitu vya aina hii viingie sokoni? au wamekaa tuu kama wenzao TBS, aagrrrrrrrrr hivi mamlaka zishanichosha, wamejaa uzembe sana.
 
TFDA wanafanya nini? kazi yao ni nini mpaka vitu vya aina hii viingie sokoni? au wamekaa tuu kama wenzao TBS, aagrrrrrrrrr hivi mamlaka zishanichosha, wamejaa uzembe sana.
mkuu umeisoma hii taarifa au unalaumu tu?!
 
TFDA wanafanya nini? kazi yao ni nini mpaka vitu vya aina hii viingie sokoni? au wamekaa tuu kama wenzao TBS, aagrrrrrrrrr hivi mamlaka zishanichosha, wamejaa uzembe sana.

Sijaona mamlaka yeyote iliyoundwa nchi hii ambayo ipo serious, chunguza SUMATRA, TCRA, FAIR COMPETITION, TBS,
TRA, nk
Lakini wanaotutia hasara zaidi ni TFDA kwani watu tunaugua malaria zisizopona kila siku hazisikii dawa...ipo siku daktari mmoja pale hospitali ya Mnazi-1 aliniambia hapa TZ 40% - 60% ya dawa zote zinazoingizwa TZ ni feki...Tafakari vifo!!!
 
TFDA wanafanya nini? kazi yao ni nini mpaka vitu vya aina hii viingie sokoni? au wamekaa tuu kama wenzao TBS, aagrrrrrrrrr hivi mamlaka zishanichosha, wamejaa uzembe sana.

Mkuu wanatudhihirishia wapo pale kwaajili ya kula kilaini laini kodi zetu walala hoi
 
Suala hilo lithibitiwe haraka lisije kuleta madhara na wahusika wachukuliwa hatua za kisheria.
 
hv hao TFDA n washenzi pamoja na bi nyoni na mponda inakuwaje mpk hii kitu inaingia kwnye mzunguko kwel serikal yet n ya kisee.. Na hakuna action zaid ya kutuambia turudishe shamba la bibi limekuwa rotten.
 
Back
Top Bottom