Taarifa kwa umma: Atumia jina la Lukuvi kutapeli...

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,721
Imetolewa na Umoja Village

prince.jpg

WanaJF tunapenda kuleta kwenu taarifa zinazohusu mwenendo wenye kutia shaka wa kijana Prince Owden (PICHANI).

Kwa sasa taarifa hizi zinabaki kama tuhuma ambazo zimefanyiwa uchunguzi wa awali na wanakijiji kadhaa ambao wamethibitisha shaka yao kuhusu ndugu yetu Prince Owden. Hivyo tumeonelea ni vema kuleta kwenu ili kuweka tahadhari hasa kwa kuwa mwenendo huo unaelekea kuwa na nia yenye kuweza kuwaumiza wengine.

Ndugu Prince Owden alijitambulisha katika group la UV Whatsapp kwa jina hilo ambalo ndilo linalotumika mitandaoni akijieleza kuwa yeye ni daktari bingwa ‘neurosurgeon’ kama ambavyo wanakijiji kadhaa walivyoweza kujitambulisha. Mara zote Dr. Prince (kama ambavyo tutaendelea kutumia utambulisho kwa ‘taaluma’ yake ya udaktari) amesisitiza kwamba yeye ni mwajiriwa katika hospitali ya Hindu Mandal hapa Dar es Salaam. Halikadhalika kwa nyakati tofauti amejieleza yeye kama mtoto wa waziri wa nchi Ofisi ya waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Mh. William Vangimembe Lukuvi, japo baadaye amekwepa kututhibitishia hilo. Huenda hili si neno kwa sababu dhamira ya kufahamiana kwetu na kushirikiana haitokani na unasaba wa mtu yeyote na kiongozi wa nchi, ila tutaeleza huku mbele shaka zetu. Vilevile kwa maneno na matendo yake Dr. Prince amejaribu kuonyesha kwamba yeye ni afisa wa serikali katika kitengo ambacho hakiweki bayana, mtu mwenye kufahamiana na wakuu serikalini na katika siasa. Pia akijitambulisha kama mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa japokuwa makazi yake ni jijini Dar es Salaam jirani na hoteli ya Holiday Inn.

Pengine maisha yake binafsi si kitu kama sio mashaka aliyotujengea katika tuhuma hizi hapa chini.


  1. Mara kadhaa Dr. Prince amejaribu kujipatia pesa kwa njia za ulaghai kutoka kwa wana UV kwa kigezo cha kukopeshwa Tsh. 500,000/- ambazo mara zote anaahidi kurudisha ndani ya muda mfupi (bila kufafanua). Mara zote hizo akidai ama kadi yake ya benki Barclays imepotea, ama kaisahau mahali ama mtandao wa benki hauko vizuri hivyo hawezi kutoa pesa. Lakini uchunguzi ulionyesha kuwa katika muda aliodai hivyo Benki ya Barclays haikuwa na tatizo hilo.
  2. Mara nyingine amejaribu kutaka kupewa akaunti namba za wanakijiji lakini baada ya kufanya mawasiliano na wengine, wanakijiji hao wakatahadharishwa kutothubutu.
  3. Amekuwa pia akitoa ahadi za kusaidia wengine kuwawezesha kuagiza gari kutoka Japan kwa gharama ya Tsh. 3,000,000/-, ambazo yeye angepewa na kisha kumuunganisha mhusika na wauzaji magari wa nje.
  4. Amekuwa akiwaeleza wanakijiji hasa wakinadada kuwa atawasaidia kupata huduma za matibabu katika hospitali anazofanyia kazi hasa akihitaji kiasi cha pesa kushughulikia matatizo fulani ya kiafya. Mara zote amewasisitiza watu kutopeleka wagonjwa wao hospitali ya Mwananyamala kwa kuwa hapo ni mahali ambapo serikali hupeleka madaktari waliofeli.
  5. 5. Dr. Prince pia amejitaja kuwa ni mmoja kati ya madaktari kumi bingwa hapa Tanzania katika taaluma yake na kuwa kati ya hao ni watatu tu ambao wamebaki hapa nchi. Hii inampa yeye fursa ya kuwa miongoni mwa watanzania wachache sana ambao wamewahi na wanaendelea kuitumia ndege maalum ya raisi kutokana na uzito wa taaluma yake. Bila shaka akiwazidi hata mawaziri wengi ambao hawajawahi kupata nafasi hiyo.
  6. Dr. Prince amekuwa akijaribu kusambaza habari za kujieleza kuwa ana mahusiano na wakinadada kadhaa wa UV na wengine wenye nasaba na viongozi wa serikali na hata kusambaza picha zao mitandaoni bila kujali kama kufanya hivyo anawavunjia heshima na kuhatarisha maisha yao ya kindoa na kifamilia.
  7. katika kipindi kifupi amefanikiwa kujipenyeza mpaka kwenye sehemu za kazi za wana UV na huko akionyesha mienendo ya kitapeli jambo ambalo linazidi kutia hofu pia usalama wa wanakijiji.
  8. katika kipindi kati ya mwezi April na Mei mwaka huu, Dr. Prince amejaribu ‘kuua’ bibi zake wawili kwa lengo la kupata rambirambi. Tunadhani alipokosa rambirambi za bibi wa kwanza akaona ni vema kumuondoa na wa pili. Hata hivyo alikwepa wanakijiji wasiweze kuhudhuria mahali penye msiba na hata siku ya kuaga maiti ya bibi mdogo pale hospitali ya Muhimbili. Maiti ilisafirishwa kwenda Mbeya kwa ndege ya kukodi.

Tukiacha madai yake mengine kama kumiliki majumba, moja ikiwa na sebule tano, kufahamiana na viongozi wa serikali na kujisifu kuwa na uhusiano na wakinadada kadhaa, sasa tuangalie matokeo ya uchunguzi wetu.

Timu yetu ya UV ilifika katika hospitali ya Hindu Mandal ambapo uongozi ulikiri kutomtambua mtu mwenye jina hilo, mbaya zaidi hata picha yake haifahamiki sio tu kwa uongozi bali hata wafagizi wa hospitali.

Baada ya kufahamishwa hilo akaeleza kwamba yeye anafanya consultation Aga Khan ambapo timu yetu ilifika hapo na kuongea na uongozi ambao haukuweza kumtambua si tu kwa jina bali pia kwa sura baada ya kuonyeshwa picha yake. Kama hiyo haitoshi Dr. Prince akajisukumiza AAR ambapo pia tulithibitishiwa na afisa rasilimali watu (HR) kuwa mtu huyo hafahamiki na hata huduma anazodai kuwa anaendesha hospitalini hapo hazipatikani.

Baada ya kubanwa na wanakijiji hasa utata wa jina lake kutofahamika maeneo yote hayo, alibadili na kudai kwamba yeye anaitwa Dr. Vangenembe. Hivyo jina lake ni Dr. Prince Owden Vangenembe William Lukuvi (bila shaka sio Vangimembe). Tunajitahidi kupata mawasiliano na Mheshimiwa waziri ili kujiondolea shaka kuwa mhusika anatumia vibaya jina la kiongozi wa serikali.

Timu yetu haikuchoka na uchunguzi na badala yake tulimtumia mgonjwa ili kuweza kujua kama kweli ni mfanyakazi wa Hindu Mandal, hata hivyo alipoongozana na mgonjwa huyo hakuweza kuonyesha dalili hata moja kwamba anafahamika hospitalini hapo. Kifupi ni kuwa hakuwa hata na ofisi na hakuna mtu aliyemfahamu kama daktari wa hospitali hiyo. Kwa sasa amegeuza kibao kwamba yeye anafanya kazi Muhimbili.

Katika siku nne zilizopita timu yetu ilimbana Dr. Vangenembe Prince Owden William Lukuvi, ili aweze kujitetea kuhusu tuhuma za kutaka kuwatapeli wanakijiji, lakini matokeo yake aliishia kutoa kauli za vitisho na mwishowe kujiondoa kijijini UV Whatsapp.

Uchunguzi wetu ni kwamba Dr. Prince hana makazi maalum ya kuishi hasa baada ya kujaribu kuhamia kwa mwanakijiji mwenzetu bila mafanikio. Hafahamiki anafanya kazi gani na kama ana mtandao na wengine (syndicate) ama anaratibu shughuli zake peke yake.

Sababu ya kuandika haya yote ni kuwatahadharisha wanaJF ili msipatwe na madhara ambayo wengine wameelekea kuyapata. Vilevile ni kwamba ushahidi kuhusu matendo yake na mienendo yake unaendelea kukusanywa na tahadhari ya kuwalinda wanakijiji waliotishwa imechukuliwa kwa kutoa taarifa vyombo vya usalama.

Jambo hili linahusisha pia vyombo vya usalama.

Hatuwezi kupuuza kitisho ingawa hatuogopi vitisho.
 
Naona nyota tu hapa..UV ni kundi la chama au ni kitu gani?..anyway ntafatilia comment hapa
 
Duh! Mjini shule.
Na hiyo Kijijini UV Whatsapp ni nini? Au pia nayo mjini shule?
 
Huyu si owden lukuwi huyu nilisoma nae darasa la saba pale st.mary's ya Tabata huyu..!, kamaliza la saba 2002 huo udaktari bingwa ameutoa wapi..??!
By the way..., jina lake halisi ni 'LUKUWI' with a 'W' and NOT 'LUKUVI' with a 'V'
 
yaani mnapoteza muda kumtafuta Dr. Vangenembe Prince Owden William Lukuvi. By that name I just ignore his/her exstence.

Dactari bingwa anajiita Dr. Vangenembe Prince Owden William Lukuvi. Huo ubingwa sio wa kidactari ni wa uchenchede. just by the name.

Acheni kupoteza muda fanyeni kazi nyingine huyo ni tapeli. period.
 
halafu sio wenye magari hatupigi pichi tukiwa tumesimama kwenye magari yetu.

mara nyingi tuki pack tunakuta watu wamesimama wanaomba kupigwa picha
 
mjini hapa akina YAHAYA wapo kazini kila kukicha
Lady J dee alishasema na leo namuuliza Yahaya unaishi wapiiiiiii......?
 
Hilarious...
hivi watu wazima magrupu ya nini mi kwa mtazamo wangu naona kama mashudu tu, kupoteza muda kwenye magrupu na kupiga majungu unless group lina specific mission yenye tija
 
Nafikiri jamaa amei - copy toka jukwaa jingine ameileta huku akifikiri sisi ni wenzake ktk jukwaa hilo la uv, lakini inasaidia sana kwa taarifa tu
 
Hivi UV ni facebook group au ni whatsapp group? Kwenye bandiko lako nakumbuka kusoma kwamba ni whatapp group.

Tiba
Ni facebook group na ipo ktk whatsapp pia. inaitwa Umoja Village
 
Back
Top Bottom