Taarifa kwa umma: Atumia jina la Lukuvi kutapeli...

Imetolewa na Umoja Village

View attachment 160858

WanaJF tunapenda kuleta kwenu taarifa zinazohusu mwenendo wenye kutia shaka wa kijana Prince Owden (PICHANI).

Kwa sasa taarifa hizi zinabaki kama tuhuma ambazo zimefanyiwa uchunguzi wa awali na wanakijiji kadhaa ambao wamethibitisha shaka yao kuhusu ndugu yetu Prince Owden. Hivyo tumeonelea ni vema kuleta kwenu ili kuweka tahadhari hasa kwa kuwa mwenendo huo unaelekea kuwa na nia yenye kuweza kuwaumiza wengine.

Ndugu Prince Owden alijitambulisha katika group la UV Whatsapp kwa jina hilo ambalo ndilo linalotumika mitandaoni akijieleza kuwa yeye ni daktari bingwa ‘neurosurgeon' kama ambavyo wanakijiji kadhaa walivyoweza kujitambulisha. Mara zote Dr. Prince (kama ambavyo tutaendelea kutumia utambulisho kwa ‘taaluma' yake ya udaktari) amesisitiza kwamba yeye ni mwajiriwa katika hospitali ya Hindu Mandal hapa Dar es Salaam. Halikadhalika kwa nyakati tofauti amejieleza yeye kama mtoto wa waziri wa nchi Ofisi ya waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Mh. William Vangimembe Lukuvi, japo baadaye amekwepa kututhibitishia hilo. Huenda hili si neno kwa sababu dhamira ya kufahamiana kwetu na kushirikiana haitokani na unasaba wa mtu yeyote na kiongozi wa nchi, ila tutaeleza huku mbele shaka zetu. Vilevile kwa maneno na matendo yake Dr. Prince amejaribu kuonyesha kwamba yeye ni afisa wa serikali katika kitengo ambacho hakiweki bayana, mtu mwenye kufahamiana na wakuu serikalini na katika siasa. Pia akijitambulisha kama mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa japokuwa makazi yake ni jijini Dar es Salaam jirani na hoteli ya Holiday Inn.

Pengine maisha yake binafsi si kitu kama sio mashaka aliyotujengea katika tuhuma hizi hapa chini.


  1. Mara kadhaa Dr. Prince amejaribu kujipatia pesa kwa njia za ulaghai kutoka kwa wana UV kwa kigezo cha kukopeshwa Tsh. 500,000/- ambazo mara zote anaahidi kurudisha ndani ya muda mfupi (bila kufafanua). Mara zote hizo akidai ama kadi yake ya benki Barclays imepotea, ama kaisahau mahali ama mtandao wa benki hauko vizuri hivyo hawezi kutoa pesa. Lakini uchunguzi ulionyesha kuwa katika muda aliodai hivyo Benki ya Barclays haikuwa na tatizo hilo.
  2. Mara nyingine amejaribu kutaka kupewa akaunti namba za wanakijiji lakini baada ya kufanya mawasiliano na wengine, wanakijiji hao wakatahadharishwa kutothubutu.
  3. Amekuwa pia akitoa ahadi za kusaidia wengine kuwawezesha kuagiza gari kutoka Japan kwa gharama ya Tsh. 3,000,000/-, ambazo yeye angepewa na kisha kumuunganisha mhusika na wauzaji magari wa nje.
  4. Amekuwa akiwaeleza wanakijiji hasa wakinadada kuwa atawasaidia kupata huduma za matibabu katika hospitali anazofanyia kazi hasa akihitaji kiasi cha pesa kushughulikia matatizo fulani ya kiafya. Mara zote amewasisitiza watu kutopeleka wagonjwa wao hospitali ya Mwananyamala kwa kuwa hapo ni mahali ambapo serikali hupeleka madaktari waliofeli.
  5. 5. Dr. Prince pia amejitaja kuwa ni mmoja kati ya madaktari kumi bingwa hapa Tanzania katika taaluma yake na kuwa kati ya hao ni watatu tu ambao wamebaki hapa nchi. Hii inampa yeye fursa ya kuwa miongoni mwa watanzania wachache sana ambao wamewahi na wanaendelea kuitumia ndege maalum ya raisi kutokana na uzito wa taaluma yake. Bila shaka akiwazidi hata mawaziri wengi ambao hawajawahi kupata nafasi hiyo.
  6. Dr. Prince amekuwa akijaribu kusambaza habari za kujieleza kuwa ana mahusiano na wakinadada kadhaa wa UV na wengine wenye nasaba na viongozi wa serikali na hata kusambaza picha zao mitandaoni bila kujali kama kufanya hivyo anawavunjia heshima na kuhatarisha maisha yao ya kindoa na kifamilia.
  7. katika kipindi kifupi amefanikiwa kujipenyeza mpaka kwenye sehemu za kazi za wana UV na huko akionyesha mienendo ya kitapeli jambo ambalo linazidi kutia hofu pia usalama wa wanakijiji.
  8. katika kipindi kati ya mwezi April na Mei mwaka huu, Dr. Prince amejaribu ‘kuua' bibi zake wawili kwa lengo la kupata rambirambi. Tunadhani alipokosa rambirambi za bibi wa kwanza akaona ni vema kumuondoa na wa pili. Hata hivyo alikwepa wanakijiji wasiweze kuhudhuria mahali penye msiba na hata siku ya kuaga maiti ya bibi mdogo pale hospitali ya Muhimbili. Maiti ilisafirishwa kwenda Mbeya kwa ndege ya kukodi.

Tukiacha madai yake mengine kama kumiliki majumba, moja ikiwa na sebule tano, kufahamiana na viongozi wa serikali na kujisifu kuwa na uhusiano na wakinadada kadhaa, sasa tuangalie matokeo ya uchunguzi wetu.

Timu yetu ya UV ilifika katika hospitali ya Hindu Mandal ambapo uongozi ulikiri kutomtambua mtu mwenye jina hilo, mbaya zaidi hata picha yake haifahamiki sio tu kwa uongozi bali hata wafagizi wa hospitali.

Baada ya kufahamishwa hilo akaeleza kwamba yeye anafanya consultation Aga Khan ambapo timu yetu ilifika hapo na kuongea na uongozi ambao haukuweza kumtambua si tu kwa jina bali pia kwa sura baada ya kuonyeshwa picha yake. Kama hiyo haitoshi Dr. Prince akajisukumiza AAR ambapo pia tulithibitishiwa na afisa rasilimali watu (HR) kuwa mtu huyo hafahamiki na hata huduma anazodai kuwa anaendesha hospitalini hapo hazipatikani.

Baada ya kubanwa na wanakijiji hasa utata wa jina lake kutofahamika maeneo yote hayo, alibadili na kudai kwamba yeye anaitwa Dr. Vangenembe. Hivyo jina lake ni Dr. Prince Owden Vangenembe William Lukuvi (bila shaka sio Vangimembe). Tunajitahidi kupata mawasiliano na Mheshimiwa waziri ili kujiondolea shaka kuwa mhusika anatumia vibaya jina la kiongozi wa serikali.

Timu yetu haikuchoka na uchunguzi na badala yake tulimtumia mgonjwa ili kuweza kujua kama kweli ni mfanyakazi wa Hindu Mandal, hata hivyo alipoongozana na mgonjwa huyo hakuweza kuonyesha dalili hata moja kwamba anafahamika hospitalini hapo. Kifupi ni kuwa hakuwa hata na ofisi na hakuna mtu aliyemfahamu kama daktari wa hospitali hiyo. Kwa sasa amegeuza kibao kwamba yeye anafanya kazi Muhimbili.

Katika siku nne zilizopita timu yetu ilimbana Dr. Vangenembe Prince Owden William Lukuvi, ili aweze kujitetea kuhusu tuhuma za kutaka kuwatapeli wanakijiji, lakini matokeo yake aliishia kutoa kauli za vitisho na mwishowe kujiondoa kijijini UV Whatsapp.

Uchunguzi wetu ni kwamba Dr. Prince hana makazi maalum ya kuishi hasa baada ya kujaribu kuhamia kwa mwanakijiji mwenzetu bila mafanikio. Hafahamiki anafanya kazi gani na kama ana mtandao na wengine (syndicate) ama anaratibu shughuli zake peke yake.

Sababu ya kuandika haya yote ni kuwatahadharisha wanaJF ili msipatwe na madhara ambayo wengine wameelekea kuyapata. Vilevile ni kwamba ushahidi kuhusu matendo yake na mienendo yake unaendelea kukusanywa na tahadhari ya kuwalinda wanakijiji waliotishwa imechukuliwa kwa kutoa taarifa vyombo vya usalama.

Jambo hili linahusisha pia vyombo vya usalama.

Hatuwezi kupuuza kitisho ingawa hatuogopi vitisho.

????? amamkweli watu hamna cha kufanya....yaani we unakaa unachunguza mburura kama huyo wkaati kila kitu kiko wazi ....pls avoid conman wa mtindo kama huu.
 
Hamuoni hilo shati la kijani na nembo ya magamba? Sasa kama ni mtoto wa Lukuvi mnaona ajabu gani huyu mtoto kuwa tapeli? Kama baba yake ni jangili aliyemaliza tembo huko Ruaha mtoto atakosaje kuwa kama baba?
 
Naona nyota tu hapa..UV ni kundi la chama au ni kitu gani?..anyway ntafatilia comment hapa

UV Whatsap Ni Kundi katika mtandao wa kijamii wa whatsap (Umoja Village) Kama yalivyo makundi mengine mengi katika mitandao mbali mbali ya kijamii
 
Hivi sasa ameshaifunga acount yake ya facebook (Prince Owden) tangu alivyostukiwa na anatumia akaunti nyingine (nimeshaifahamu).

kwa wengi wenu hamuamini ID yangu basi endeleeni hivyo hivyo mtakujalizwa na kunikumbuka...
 
Na taarifa hii imeletwa na Msanii tia akili

Mkuu hii ni Tahadhari inatolewa mtajwa Huyo ni Mtanzania anafanya utapeli, Leo kafanya huko Kesho anaweza akafanya au akajaribu kukufanyia utapeli hata wewe.

Kikubwa tuzingatie Tahadhari hiyo na tuichukue Kama kinga ili Kesho ukikutana nae mtaani umfahamu kwa kazi yake hiyo ya utapeli.
 
Last edited by a moderator:
umoja wa vijana CCM UVCCM ni matapeli kweli angari sasa.maccm uvccm.
 
yaani mnapoteza muda kumtafuta Dr. Vangenembe Prince Owden William Lukuvi. By that name I just ignore his/her exstence.

Dactari bingwa anajiita Dr. Vangenembe Prince Owden William Lukuvi. Huo ubingwa sio wa kidactari ni wa uchenchede. just by the name.

Acheni kupoteza muda fanyeni kazi nyingine huyo ni tapeli. period.


Nakubaliana na wewe Kuwa Huyu ni tapeli kwa majina yake au kwa matendo yake.
Nafikiri tumepewa Kama Tahadhari na taarifa ili Kesho akitokea anga zako ufahamu Kuwa Yahaya Yuko mbele yako
 
halafu sio wenye magari hatupigi pichi tukiwa tumesimama kwenye magari yetu.

mara nyingi tuki pack tunakuta watu wamesimama wanaomba kupigwa picha
Wakati mwingine huwa wanasaidia kufuta vumbi kwa nguo zao...
Nilikuwa pale Soccer City Pub napata maji ya Ilala, wakati naondoka kuna jamaa mmoja alinidai fidia eti gari langu limechafua nguo yake. Nikamuuliza kivipi akasema aliligusa kwa bahati mbaya, na ukweli lilikuwa chafu maana ndiyo nilikuwa nimetoka safari na nilifika pale kwa ajili ya kupata chakula pamoja na kuliosha
 
Hii habari nahisi hapa si mahala pake inawahusu zaidi watu wa uv umoja village na wala sio wana jf
 
Hilarious...
hivi watu wazima magrupu ya nini mi kwa mtazamo wangu naona kama mashudu tu, kupoteza muda kwenye magrupu na kupiga majungu unless group lina specific mission yenye tija


Hivi watu wazima ni kuanzia miaka mingapi?
By the way umewezaje kujua umri ea hao walio katika Hilo group? Hadi ukaja na hitimisho Kuwa "watu wazima magrupu ya nini?"

Tapeli anaweza ibukia hata kanisani/Msikitini sio lazima iwe huko kwenye magrupu.

JIHADHARI NA TAPELI HUYO HAPO PICHANI.
 
Hivi UV ni facebook group au ni whatsapp group? Kwenye bandiko lako nakumbuka kusoma kwamba ni whatapp group.

Tiba

Kuna Umoja Village facebook group ambalo ndani yake kuna Umoja Village WhatsAp group, ambayo member wake ni wana UVFB Wanao share common interest.
 
Kuna Umoja Village facebook group ambalo ndani yake kuna Umoja Village WhatsAp group, ambayo member wake ni wana UVFB Wanao share common interest.

Sasa nyie mnashare interest gani na huyo Doctor fake?

Tiba
 
Hivi sasa ameshaifunga acount yake ya facebook (Prince Owden) tangu alivyostukiwa na anatumia akaunti nyingine (nimeshaifahamu).

kwa wengi wenu hamuamini ID yangu basi endeleeni hivyo hivyo mtakujalizwa na kunikumbuka...

Mkuu tupo tulioichukulia kwa uzito taarifa ya tapeli Huyo,
Lakini pia wapo waliojikita katika kina la mtoa taarifa "Msanii"
Hii isikupe shida tumeathiwa na majina ya kikoloni ndio mana.
 
Sasa nyie mnashare interest gani na huyo Doctor fake?

Tiba
Mwizi anapokuja kukuibia huwa unashare naye interest gani?

Ninamashaka labda habari imekugusa na kukuumiza kiasi fulani....
 
Hii habari nahisi hapa si mahala pake inawahusu zaidi watu wa uv umoja village na wala sio wana jf

Tapeli Huyo amefanya matendo hayo ya kitapeli huko UV whatsAp lakini pia anaweza kufanya matendo hayo hayo hata humu Jf kwa Kuwa Naye ni mwanachama humu.
Hivyo hii ni Tahadhari.

Ni sawa na jamaa afanye ujambazi na utapeli huko Kigoma alafu akakimbia sasa ikatolewa taarifa pamoja na Tahadhari hata mikoa mingine mfano Mwanza alafu tukasema "taarifa hii haituhusu inawahusu wakazi wa Kigoma Pekee"
 
Mkuu hii ni Tahadhari inatolewa mtajwa Huyo ni Mtanzania anafanya utapeli, Leo kafanya huko Kesho anaweza akafanya au akajaribu kukufanyia utapeli hata wewe.

Kikubwa tuzingatie Tahadhari hiyo na tuichukue Kama kinga ili Kesho ukikutana nae mtaani umfahamu kwa kazi yake hiyo ya utapeli.

Wanatapeliwa haohao wanaolewa na majina ya watu! Eti Lukuvi.... wa kazi gani na kwa mpango upi. Ujinga tu.
 
Mkuu hii ni Tahadhari inatolewa mtajwa Huyo ni Mtanzania anafanya utapeli, Leo kafanya huko Kesho anaweza akafanya au akajaribu kukufanyia utapeli hata wewe.

Kikubwa tuzingatie Tahadhari hiyo na tuichukue Kama kinga ili Kesho ukikutana nae mtaani umfahamu kwa kazi yake hiyo ya utapeli.

Wanatapeliwa haohao wanaolewa na majina ya watu! Eti Lukuvi.... wa kazi gani na kwa mpango upi. Ujinga tu.

Ngoja na mimi nijiunge na ilo group lenu then nijiite Mwakibete Mrisho Kikwete, si mnalewa majina.
 
Hivi sasa ameshaifunga acount yake ya facebook (Prince Owden) tangu alivyostukiwa na anatumia akaunti nyingine (nimeshaifahamu).

kwa wengi wenu hamuamini ID yangu basi endeleeni hivyo hivyo mtakujalizwa na kunikumbuka...

Msanii hiki kitendo kitendo cha kufunga accoun tosha kuwa huyu ni tapeli!!! Kama madai yalikuwa ni ya uongo angekuja hapa kupinga au kutumia FB kupinga. Wezi tu hawa. Tunashukuru kwa taarifa maana JF ina watu wengi angalao atakayepata habari atajulisha na wengine.
 
Sasa nyie mnashare interest gani na huyo Doctor fake?

Tiba

Mkuu lengo la group ni kufahamiana kiuhalisia, kuelimishana kuhusu mambo mbali mbali yahusuyo Maisha. Hizo ndio common interest tulizokuwa Nazo na doctor Huyo fake Kabla ya kumbaini ufake wake. Mtajwa alijitambulisha kazi yake Kuwa ni Daktari, lakini amefanya matendo ya utapeli. Kama ambavyo taarifa Ina jieleza
 
Back
Top Bottom