Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
250
583
TAARIFA KWA UMMA



Treni.jpg
TRENI YA ABIRIA KUTOKA KIGOMA YAPATA AJALI TABORA

Shirika la Reli Tanzania (TRC) linautaarifu umma kuwa Treni ya abiria namba Y14 yenye injini namba 9019, iliyokuwa ikisafiri kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam, imepata ajali majira ya saa 5:00 asubuhi eneo la Malolo Mkoani Tabora Juni, 22,2022.

Treni iliondoka Stesheni ya Kigoma majira ya saa 2 usiku, siku ya Jumanne tarehe 21 Juni 2022, kuelekea Dar es Salaam ikiwa na behewa 8 zilizobeba abiria 930. Ilipofika eneo la Malolo (Km 10

kutoka stesheni ya Tabora) behewa 5 za abiria daraja la tatu, behewa 1 la vifurushi, behewa 1 la huduma ya chakula na vinywaji na behewa la breki zilianguka na kusababisha ajali.

Majeruhi 132 tayari wamepelekwa katika hospitali ya Mkoa, Kitete Tabora, kwaajili ya matibabu na wanaendelea vizuri. Ajali imesababisha jumla ya Vifo 4 wakiwemo watoto 2, wakike mwenye umri wa miaka 5 na wakiume miezi 4 na watu wazima wawili, mwanaume na mwanamke.

Shirika linaendelea na zoezi la kuwasafirisha manusura wa ajali kutoka Tabora ili kuendelea na safari ya kuelekea Dar es Salaam. Shirika la Reli linaendelea kufuatilia kwa karibu, kufahamu chanzo cha ajali ili kuchukua hatua.

TRC inatoa pole kwa familia za marehemu na linawaombea majeruhi wa ajali wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.

TRC itaendelea kuutaarifu umma endapo kutakuwa na taarifa nyingine zitakazojitokeza katika eneo la ajali.

FV2Y4uTXEAA0eAL.jpg

FV2Y4uXWYAAvXyd.jpg


0d9dde19-2ed0-4590-88a5-834ed23af327.jpg


fd4d5e31-5d09-4325-8b92-718f6ed61fd3.jpg


d6258d62-7802-4183-b8a6-6f8475aa18ee.jpg

treni 1.JPG
 
Ajali ya treni imetokea Tabora eneo la Malolo. Inahofiwa watu kadhaa wamefariki na wengine kujeruhiwa vibaya. Kazi ya uokoaji unaendelea.

IMG_20220622_122219.jpg
IMG_20220622_122219.jpg
 
Hii ndio Taarifa iliyotufikia hivi punde kutoka Tabora, Kwamba Treni hiyo iliyobeba Abiria kutoka Kigoma ikielekea Dar es salaam imeanguka kwenye vijiji vya Tabora na kusababisha Majeruhi kadhaa.

Tatendelea kuleta taarifa zaidi kwa kadri zinavyotufikia.

Chanzo: Muungwana Blog
 
Kipande cha Kigoma Tabora Nikipande kibaya sana
Reli imechoka Treni Inadunda Kama Kuna Magogo yanagongana
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom