Taarifa kwa makamanda na wadau wote wa mabadiliko chini ya UKAWA

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Ndugu zangu poleni na mapambano,

Kwa muda wa mwezi mmoja na nusu sasa nilipotea mitandaoni na katika majukumu mengine ya kimageuzi.

Laa hasha, sikupotea kwa maana ya kuyasaliti mapambano ya ukombozi wa Tanzania, mimi ni mtu huru sawa na matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uhuru wangu huu unaotambuliwa na katiba ya nchi, umepokwa na maadui wa ukombozi waliochini ya mwavuli wa kisiasa.

Ndugu Watanzania, Taifa linaingia katika uchaguzi mkuu siku tatu zijazo yaani jumapili, Kwaajili ya kulinda Amani na Umoja wetu unaopita kwenye jiwe la moto, nisieleze UNDANI wa yaliyonisibu na WASIBUAJI katika siku 45 ngumu kabisa tangu niwepo duniani, nikipindi ambacho nilikuwa naupigania UHAI wangu pande zote yaani angani, majini na nchi kavu.

Nawaomba watanzania msiogope, kuweni majasiri wakulinda haki zenu za kikatiba na kutii sheria za nchini na sio vinywa vya kisiasa, kwa umoja wetu, tujitokeze kupiga kura kwa wingi na kura hiyo tumpigie Mh Edward Ngoyayi Lowassa aongoze mabadiliko kutoka kuwa taifa la kikundi kidogo cha kihalifu kiitwacho ccm kinachoendesha uhalifu nchini kwakulindwa na baadhi ya vyombo vya dola.

Ndugu zangu, nataka mfahamu kuwa ccm imehama kutoka kuwa chama cha siasa na kuwa genge la uhalifu nchini linalobaka matakwa ya umma kwamsaada wa vyombo vya dola, hakuna njia ya mkato ya kuitoa ccm madarakani bali ni kupiga kura kwa wingi na KUZILINDA kura hizo kwamjibu kwa katiba na sheria za tume ya uchaguzi na sio huruma ya wahalifu hawa wanaowalazimisha tukalale baada ya kupiga kura.

Dhambi kubwa ambayo hata Mungu hatatusamehe ni kitendo cha sisi kupiga kura na kurudi majumbani mwetu kulala na kuacha wahalifu hawa watuhesabie kura.

Sisi wanaukombozi tuliombele ya mstari wa vita hii tumeshamaliza kazi kwa asilimia miamoja, hatua iliyosalia ni ya watanzania wote kulinda kura zetu mpaka Mh Lowassa na wabunge na madiwani wa UKAWA watangazwe wameshinda ndipo tutembee vifua mbele maatako nyuma tukiusherekea uhuru wetu wa pili.

Niwahakikishie mimi nipo nimzima wa afya, Mungu hakutaka yatokee waliyokusudia watesi na wanyang' anyi wetu.

Natumia fursa hii kuwakumbusha ccm, jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, UHAI wa binadamu hauishii kulindwa na katiba ya Tanzania wanayoifinyanga tu bali Uhai wa binadamu unalindwa na Katiba ya ULIMWENGU! Tanzania ni yawatanzania, matakwa ya umma yaheshimiwe, Wasiipendelee UKAWA wala wasiipendelee ccm, Bali wawapendelee Watanzania tu.

Sisi wanaukombozi tunaipigania Tanzania ambayo nyinyi vyombo vya usalama mtaiishi kesho, tunapigania ili kuboresha maslahi ya askari wa Tanzania, Tunapigania ili mtoto wa askari huyu asome bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu, tunapigania ili familia za askari hawa zitibiwe bure na huduma nyinginezo nyingi. Hatupiganii matumbo yetu bali ndoto za Watanzania wote.

Natoa shukrani za pekee kwa Mwenyekiti wa Chadema Mh Mbowe na Familia ya Mheshimiwa Lowassa ambao wamesimama nami katika kipindi chote kigumu, pia niwashukuru makamanda na marafiki zangu mitandaoni ambao kwahakika ninalo deni kubwa la kuwalipa kuanzia jumapili.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UKAWA.
 
Wewe tu ndio hupiganii tumbo lako wenzako wameshafanya miamala ya kuhamisha hela akaunti za nje ya nchi
 
Kwendraaaaa wewe hutakii nchi yetu memaaa unachochea machafuko we are not sillyyy...tunajua nani tunamtaka wala hatuna haja ya kukaa kulinda kura kama wakala tuliowaweka hatuwaamini kura zitaibiwa tuuu...
 
we wee,yericko unaposema mpaka lowassa na wabunge watangazwe washindi,unamaanisha nini?je wasipotangazwa kuwa washindi kwa kuwa kura hazikutosha?
 
we wee,yericko mwana wa nyerere,unaposema ni dhambi kuacha kura zihesabiwe na hawa wahalifu,according to you ni ccm but in fact ukawa ndio wahalifu,maswali:
je,hujui kuwa mawakala wenu pia watahusika katika uhesabuji wa hizo kura?
je mawakala wenu pia ni wahalifu?
je,kama ni wahalifu mnawaweka wa nini?
je,kuna umuhimu gani wa kuwa na mawakala kama hamuwaamini?
 
pole mkuu.najua kuna watu kama wewe ambao mmelipa bei kubwa kwa mabadiliko ya nchi hii.

wewe na Ben Saanane ni role models kwa vijana wengi.

Wameninyima haki yangu ya kupiga kura kwa Kukata jina langu pasipo sababu.

Ila najua.AND I will live to fight to see my descendants enjoy the fruits of their mother country
 
Last edited by a moderator:
we wee,yericko mwana wa nyerere,unaposema ni dhambi kuacha kura zihesabiwe na hawa wahalifu,according to you ni ccm but in fact ukawa ndio wahalifu,maswali:
je,hujui kuwa mawakala wenu pia watahusika katika uhesabuji wa hizo kura?
je mawakala wenu pia ni wahalifu?
je,kama ni wahalifu mnawaweka wa nini?
je,kuna umuhimu gani wa kuwa na mawakala kama hamuwaamini?
hujui ukisemacho.

This time system tumeishika
 
Yericko Nyerere
Pole sana mkuu kwa yaliyokukuta lakini nina uhakika hakuna amfanyiaye ubaya mtu atabaki salama duniani bila Mungu kufanya malipo yake hapa hapa duniani, ingawa haujaweka wazi yaliyokusibu lakini ni wazi tunajua nini kimekusibu, narudia tena kukupa pole sana.
 
Last edited by a moderator:
tokea upotee wamendelea kutumia zile bilioni 150 mpaka wamebakiza 10 kwa ajili ya siku tatu
 
Back
Top Bottom