Taarifa Kwa Fundis

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
TAARIFA KWA MAFUNDI WA COMPUTER

Kama unavyojua , mafundi wa computer Hapa Tanzania hawana chama chao , ambacho mtu anaweza kwenda kueleza matatizo yake yakasikilizwa , hakuna chama cha kusaidiana na kushirikiana katika mambo mengi zaidi kila mtu yuko na lake lakini hapa kati kati ya mji mafundi wengi tunajuana na tunasaidia kwa hili na lile .

Wiki iliyopita nilipigiwa simu na mtu jina lake siwezi kulitaja kwa ajili ya kulinda usalama wangu na wengine zaidi , huyu mtu akaniambia anataka kununua laptop , mimi nikaenda dukani nikanunua laptop nikampelekea ili aweze kunirudishia pesa zangu .

Nilipomkaribia nimemkabidhi laptop , akasema anaenda kuchukuwa pesa benki , ghafla akabadilika akanifungia milango ya gari yake na kunipeleka kituo cha polisi , bila maelezo yoyote yale na laptop yangu akaichukuwa akaiweka katika gari lake binafsi , lakini akajitambulisha kwamba yeye ni polisi .

Tulisumbuana huko polisi sana tu kwa sababu alikuwa anataka rushwa ili tumalizane nje ya polisi , kwa kweli nilisita kutoa pesa yangu nimkabidhi yeye , lakini watu wengine waliokuja pale ndio wakanisihi nitoe kitu kidogo ndio nitoke yote haya nikakataa .

Ikabidi nimwombe polisi hiyo kesi aifikishe mahakamani kule ndio nitaweza kwenda kuongea na kuelewana nae kwa sababu pale nilipo nisingeweza kuongea chochote na sikuwa na maelezo ya ziada kuhusu malalamiko hayo

Huku polisi nikakutana na kesi nyingi nyingi tu zingine za mwaka 2002 , mwaka huo hata secondary nilikuwa sijamaliza , na zingine zinafurahisha zaidi siwezi kuzitaja hapa haya ni maelezo mafupi .

Kwa ufupi ni kwamba kuna polisi anayepewa namba za Mfundi wa computer au watu wanaouza Computer na watu wengine , labda ni rafiki zetu , ndugu zetu , wafanyakazi wenzetu au washirika wengine katika biashara na hao watu wanajitungia visa vya uwongo kule polisi .

Halafu polisi huyo anaanza kukupigia anakuomba umpelekee laptop anataka kununua au computer anataka kununua au kifaa Fulani anataka kununua ukifika pale anakushikilia mpaka utoe kitu kidogo ndio mumalizane .

Mfano mimi nilipomwambia awalete hao watu waliokuja kushitaki akashindwa kusema chochote , na nimekaa mpaka nimetoka pale kituoni sijapewa nafasi yoyote ya mimi kuweza kuandika maelezo yangu au vielelezo vyovyote vile .

Huu ni zaidi ya uhuni , kwahiyo kama wewe unashiriki katika kuuza computer na vifaa vyake au laptops na vifaa vyake angalia sana watu unaowauzia au kushirikiana nao katika biashara hii , wengine ndio hao polisi ambao wanatumia vyeo vyao dhidi ya watu wengine wasio na hatia .

Haiwezekani mtu utishiwe usalama wako , na uhuru wako wa mambo mengine nchini mwako tena na mtu ambaye anatakiwa atetee usalama wako na uhuru wako wakati wowote anapotakiwa kufanya hivyo .

Ndio hivyo mafundi tumeingiliwa , sasa kuna umuhimu wa kuwa na chama chetu ambacho kitatetea masilahi yetu popote na kuweza kushiriki katika mambo mengine zaidi ya kujenga taifa letu tukufu la Tanzania , hicho ni kisa kimoja kimetokea kisa hichi tungekuwa na chama tungeweza kuleta mapinduzi katika jamii yetu ila ndio hivyo

Kama watu hawataki kushirikiana na kuweza kuondoa polisi wa hivi basi kuna umuhimu wa kuchukuwa hatua zaidi dhidi ya polisi wenye tabia hizi ili kukomesha aina hii ya utafutaji .

Wako katika ujenzi wa Taifa
 
...mzee we huwa unauza pc za deal?

...maana hiyo inaweza kuwa sababu na utapata usumbufu hata baadae!

...wanasema ukipenda boga,na ua lake pia lipende!

...anyways,pole kwa yaliyokupata!
 
Mkuu pole sana kwa mkasa huo.

Lakini utaratibu unaotumia kuuza hizo laptop ni mbovu, ulio na hatari kwa maisha yako na pia unaonekana hulipi kodi ama kwa kuuza laptops za wizi au njia zingine za vichochoroni.

Unatakiwa uwe na duka linalojulikana kwamba linauza laptops za "range" zote na unakuwa na "decriptions" zote kuhusu hizo laptops na wateja wote watarajiwa ni budi watembelee hapo dukani kwako au uwe na "website" ili wanunue kwa "paypal" na wanunue na uwape recepts za mauzo na VAT halafu uwe registered na revenue (kama inawezekana au uko "willing")

Haya ni mambo ambayo ndugu yangu unatakiwa uyajue kwani wewe ni mtaalam wa mambo haya. Sasa utanunuaje laptop kwa fwedha yako halafu ndio ulipwe fwedha na teja umeona wapi biashara hio.

Hata hapa majuu kama ukihitaji machine hizo kama unataka iwe "personalised" basi wanakufanyia "special order" kutoka kwa "manufacturer" na unalipa sehemu ya fwedha iwe dukani au "online" halafu kifaa kinapoletwa basi wewe hutaarifiwa na kwenda kumaliza malipo kwa kadi au fwedha taslim na si vinginevo.

Sasa mkuu jaribu kuingia bank na "business plan" yako, mwone bank manager na eleza unahitaji kiasi gani cha fwedha kuanzisha duka la maana linalouza laptops,PC na vikorokoro vingine, liwe na bora kuliko yote hapo ulipo.

Mimi siko TZ kwa muda sasa lakini bado nakumbuka jinsi polisi wanavyotumia mbinu(hasa detectives) mbalimbali za kukandamiza wale wamoonekana wana-make kwa michoro.

Achana na mambo ya kizamani ya kufanya biashara za mikononi na matokeo yake iko siku utaitwa mwizi na kupigwa mpaka ufe(sikuombei hivo mkuu).
 
Huyu polisi nimeshampa hela za moto na amekamatwa sasa hivi kwa sababu mchezo huu anaufanya kwa watu wengi sio mimi peke yangu na wengi tumeshamjua sasa hivi lakini ndio hivyo sasa yuko nae kitanzini tungoje tuone sheria inavyochukuwa mkondo wake lakini nimepigiwa simu na jamaa zake wanasema niachane na mambo hayo tumalizane
 
uliona iwe kama mbwai mbwai tuu
 
Back
Top Bottom