mgulu
Member
- Feb 14, 2015
- 74
- 33
Wana Jf
Siku ya Jumamosi nilipigiwa simu na mtu akajitambulisha kwa jina la Daniel (0656438***) kutoka Access Bank, akaniambia nimechaguliwa kwenda kwenye training kutokana na Maombi yangu niliyotuma ya kazi.
Katika maongezi na yule jamaa alinipa options nichague niiende kuanza training lini maana wao wana uhitaji wa maafisa kwa haraka sana, option ya kwanza alinipa tar. 18/05 na ya pili ilikuwa mwezi wa sita. Akazidi kunisisitizia watanitumia forms za medical cherk up nizitume kabla ya siku husika.
Kilichonishtua ni kutaka ela kama laki tatu au mbili maana hr anahitaji kwa kukufanyia upendeleo, nikamjibu mimi sina kabisa hata 10, labda unisaidie nikifika huko nitakulipa kama fadhira, jamaa akasema Mimi sina shida ila Mzee ndio kila kitu labda nikaongee nayo then tuone nitakusaidiaje, poa poa tukamalizia Hapo.
Baadaye nampigia simu kumuulizia anasema ooh bado sijaongea nayo nikiongea nayo ntakujilisha siku ikaisha bila call yake. Nilishtuka sana hasa nikipiga ile simu haipokelewi mpaka Leo. Nikajua ndio walewale wanaowaibia watu kwa kutofahamu.
Naomba kuwasilisha