Elections 2015 Taarifa kuwa Kikwete hamuungi mkono tena zamchanganya Membe

M-bongo

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
338
71
Katika kuelekea kinyanganyiro cha URAIS 2015, AFISA wa usalama wa siku nyingi Mhe Membe inasemekana amekasirishwa sana na habari za kusemekana kwamba familia ya Rais Kikwete haina mpango naye tena kwenye urais na wamehamishia Nguvu kwa Mwigulu.

Kwasababu hizo ameamua kumvuruga Rais kupitia Usalama wa TAIFA kwa kuwatisha viongozi wa usalama wa zamani na sasa, kama ilivyoonekana hapa jamvini kuhusu habari za Mzee Mwangonda ambaye alifanya kazi kubwa sana kuboresha maslahi ya wana usalama nchi nzima.

Mzee Mwangonda ambaye ni mkulima wa Kawawa huko Mbozi siku hizi ametukanwa akihusishwa na UKAWA na lowassa kwa makusudi kabisa ili wafarakane na Mkurugenzi wa sasa Othman na yeye Membe afanikiwe kumfukuza Othman , mpango wake wa miaka mingi.

Jamani mgombane kwa URAIS lakini msiguse idara muhimu ya usalama wa TAIFA , mtatuua. Nawasilisha
 
Membe? atapiga propaganda lakini kitengo kiko imara sana... Nchi hii imebarikiwa kuwa na watu wenye weledi mkubwa sana kwenye medani ya Usalama...
 
Membe alikuwa msaidizi wa Apson mwang'onda huko usalama wa taifa na sidhani kama walikuwa na maelewano mazuri ; Othmana ambae ndio mkuu wa Usalama wa taifa sasa alifanya kazi na wote wawili hawa ; kitu kinachowatenganisha ni makundi ya kuwania URAIS kupitia chama cha magamba!! Apson yuko kundi la Lowassa na Membe ndio huyo anauzengea URAIS na Othman ndio huyo mwenye mtihani mkubwa kujiunga kundi la bosi wake wa sasa akijua wazi iwapo kundi la mahasimu wao wakishinda ndio hana kazi!!
 
Katika kuelekea kinyanganyiro cha URAIS 2015, AFISA wa usalama wa siku nyingi Mhe Membe inasemekana amekasirishwa sana na habari za kusemekana kwamba familia ya Rais Kikwete haina mpango naye tena kwenye urais na wamehamishia Nguvu kwa Mwigulu. Kwasababu hizo ameamua kumvuruga Rais kupitia Usalama wa TAIFA kwa kuwatisha viongozi wa usalama wa zamani na sasa, kama ilivyoonekana hapa jamvini kuhusu habari za Mzee Mwangonda ambaye alifanya kazi kubwa sana kuboresha maslahi ya wana usalama nchi nzima. Mzee Mwangonda ambaye ni mkulima wa Kawawa huko Mbozi siku hizi ametukanwa akihusishwa na UKAWA na lowassa kwa makusudi kabisa ili wafarakane na Mkurugenzi wa sasa Othman na yeye Membe afanikiwe kumfukuza Othman , mpango wake wa miaka mingi. Jamani mgombane kwa URAIS lakini msiguse idara muhimu ya usalama wa TAIFA , mtatuua. Nawasilisha

Utauliwa peke yako wengine hatumtumainii mwanadamu.
 
Ahsante usalama wa taifa a.k.a usalama Ccm kwa kusahaulisha UKAW ndani ya majukwaa na mitandao kwa kupandikiza hili. CCM hoye!
 
Mtapiga mayowe mwisho kabisa Mgombea anakuwa Mizengo Pinda na wassira waziri mkuu, huo ndo mpango mahususi
 
Wassira anarudi Bunda kugombea ubunge ili awe waziri mkuu Wa Pinda, hii nchi full vichekesho
 
Laiti watanzania tungetumia nguvu hii kwenye maendeleo na kuacha majungu na speculations tungekua another level
 
Ukiungwa mkono na kiongozi ambaye au hapendwi au hakufanya vizuri katika uongozi wake, nadhani ni sifa tosha ya wewe unayegombea kutostahili kuchaguliwa. Mimi nadhani mgombea akiungwa mkono na Kikwete, kutokana na utendaji wa Kikwete ambao haukuwaridhisha Watanzania walio wengi, itakuwa tayari ni disqualification ya kutokuchaguliwa. Kwa sasa wagombea wahangaike kuungwa mkono na Warioba, siyo Kikwete.
 
warioba mwenyewe umri ushasonga jioni na taa nyekundu nayo kwa pamoja,hata akikuunga mkono naye ni majanga tu kama yalivyo majanga mengine duniani
 
Mbona idara yenyewe unayozungumzia imeshakuwa corrupt. Siku hizi hakuna usalama wa taifa. Ni usalama wa maslahi.
Mwang'onda ndiye Apson? Alimsaliti Mkapa.

Alimsariti vipi Mkapa acha Uongo wako ww ni jasusi gani hata hujui kuchambua data !
 
Membe alikuwa msaidizi wa Apson mwang'onda huko usalama wa taifa na sidhani kama walikuwa na maelewano mazuri ; Othmana ambae ndio mkuu wa Usalama wa taifa sasa alifanya kazi na wote wawili hawa ; kitu kinachowatenganisha ni makundi ya kuwania URAIS kupitia chama cha magamba!! Apson yuko kundi la Lowassa na Membe ndio huyo anauzengea URAIS na Othman ndio huyo mwenye mtihani mkubwa kujiunga kundi la bosi wake wa sasa akijua wazi iwapo kundi la mahasimu wao wakishinda ndio hana kazi!!

Membe Hana nafasi ya Urais asome alama za nyakati mapema ajiunge kwa Lowasa ili aje aukwae uwaziri wa Utawala bora pindi lowasa Akiwa Rais
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom