Taarifa kutoka TRA kuhusu kodi ya majengo

Heee!!kwani hii kodi ya majengo ni mpya?au ulikuwa hujafikiwa , kwani wengi hamkuwa mnailipa, sasa hapa hakuna ujanja, labda uamue kutoa umeme kabisa, na luku warudishie tanesco kabisa!!!kidogo hapo utaweza ikwepa japo kwa muda fulani tu, lakini kwa tuliokuwa tukiilipa miaka yote hakuna jipya
kwa nini wasiweke na option kwa mtu anaye taka kulipa yote alipe aachane na taratibu za kulipia kwenye luku!
 
kwa nini wasiweke na option kwa mtu anaye taka kulipa yote alipe aachane na taratibu za kulipia kwenye luku!
Tatizo hiyo kodi, imekuwa na ugumu sana kwenye kuikusanya, mala ya kwanza ilikuwa inakusanywa na halimshauri, wakashindwa, ikapelekwa TRA, wameshindwa, ikarudishwa halimashauri, sasa ndio wameona bora iwe hivi, kuikwepa ni ngumu!!!kwani inshu ni kulipa yote kwa mpigo, au wao wanataka kwa mwaka ulipe 12, 000?huko mbeleni hiyo option wanaweza iweka tu.
 
Kwa mfano Mimi nataka niwalipe Elfu 12 yao yote Mara 1 sitaki kukatwa bukubuku inakuwaje ?
Swali zuri .... Au kwa mtu aliyekwisha lipia kodi ya majengo kwa utaratibu wa zamani, akinunua umeme leo anakatwa tena.... Huu si wizi tu kama ule wa vibaka?
 
Kwanini Serikali ilishindwa kufanya reserch ikajua luku furan ndiyo mmliki akatwe na sio kubebesha mzigo wote alafu muanze kupanga foren?
nimwendelezo wa uwizi wa serikali ya ccm sasa atakatwa kila anayetumia luku kila mwezi hata kama ni wapangaji na baada ya muda utawasikia kama kunautata ukawasiliane na TRA na huko utapigwa danadana siku,miezi zinakwenda na wakati huo tunaendelea kukatwa tu na mwisho wa siku waziri wa nishati/ardhi atakuja na takwimu kama madulu wa fedha kwamba tumekusanya mabilioni kadhaa kutoka kwenye kodi ya majengo wananchi tuendelee kuwa wazalendo tujengo nchi yetu
 
Wabongo wengi wanapenda yale majina ya wanyonge na masikini hivyo hawastahili kulipa kodi yoyote halafu wanafurahi wakisikia mtu fulani katumbuliwa au kafilisiwa akidaiwa ni mkwepa kodi.
 
Na kuna tangazo wanadai watawaondoa wazee wa zaidi ya miaka 60 wasikatwe , nimejiuliza hizo LUKU zenye uwezo hadi wa kujua umri wa watu sijapata majibu hadi sasa, mambo ya kukurupuka ni mabaya sana, yaani wewe haya mambo hayakugusi huwezi kuelewa kabisaaaa uko ndani ya V8 unalipiwa kila kitu na kodi za hao hao walalahoi na bado unapanua mdomomwako eti sijui chama gani kinaleta maendeleo Stupid kabisa, kipindi hiki sijaona hata Kiumbe yeyote awe mwana siasa awe wa dini anakemea hili wooote wamepigwa ganzi. Wanyonge ndio mtajua kama hamjui
 
Swali zuri .... Au kwa mtu aliyekwisha lipia kodi ya majengo kwa utaratibu wa zamani, akinunua umeme leo anakatwa tena.... Huu si wizi tu kama ule wa vibaka?
Yani Bora vibaka huwa hawajui Sheria.. serikali wanaijua Sheria vizuri Tu ilitakiwa wao wawe mfano wa kuigwa yani
 
Waafrica ni uzembe ndo unatusumbua ,ili tufanye mambo kwa njia zisizo na hesabu..kodi ya nyumba/majengo inapaswa kulipwa kwa kuangalia size ya nyumba au jengo...TRA / TBA /municipal s au districts council,wanajukumu la kufanya kazi pamoja kupata details za nyumba/majengo pia,yanayotokea kwenye tozo ni uzembe na udhaifu mkubwa.
HAWANA CAPACITY HIYO..NADHANI YAKUTUMIA LUKU NI BORA INGAWA SI SAWA WATU WA VIJIJINI KULIPA SAWA NA MWENYE BANAGALOW LA WAZIRI JIJININ
 
Ni njia nzuri ya kulipa jengo
Kuliko kwenda kupanga foleni mara
Mtandao unambiwa uko chini
Mwishowe inakula na kupoteza muda

Ova
 
Serikali waache wizi kupitia mifumo yao,iweje elfu moja ya kodi ya jengo ikatwe tena 2%? Kwa mfano leo inatakiwa ununue umeme wa zaidi ya elfu mbili ikiwa elfu moja ya jengo na iliyobaki ni umeme.

Sasa wizi wa serikali ukiweka lets say elfu 5 basi makato yatakuja 5100 yaani wana assume hadi buku ya pango nayo unanunua umeme,wajaribu kuprogram upya kwamba kwa wanaokatwa elfu 1000 waiset 980 ili Tsh 20 inayozidi kwenye makato iwe replaced kwenye 1000 na kuwa 980.
 
Hatukushauri hivi, tunataka kodi itozwe kwa asilimia, mwenye nyumba kubwa atatumia umeme mwingi na atalipa zaidi, sio kiweka fixed amaount kiasi hata mwenye chumba kimoja alipe sawa na mwenye bungalow lisilo la ghorofa

Acha wivu wewe tulizana matako hayo....
 
Yaani hii nchi ni ya ajabu sana!!wananchi hao waoitwa wanyonge hawataki kabisa kusikia suala la kulipa kodi!!wanadhania kodi zote za kuendesha nchi ni tajiri tu ndio anatakiwa kumlipia!!!suala la tozo hiyo ya majengo wala sio mbaya/kiasi kikubwa bali tatizo ni utaratibu tu wa ukusanyaji wake!!tozo inayoumiza ni ile ya miamala, sasa watu wameisahau ile wanaanza kurukia hii, ya majengo!!mbona mwanachama wa simba/yanga kwa mwaka anachangia 12, 000 kwenye timu zao,?na wanyonge ndio wanufaikaji wakubwa sana wa kodi, hizo!!kuputia elimu, afya.kuliko hata tajiri.
Tena waweke Tozo katika kila unaponunua Luku kuna asilimia unaacha! Ili tukome kabisa....***** miti yenyewe tumekata
 
Back
Top Bottom