Taarifa kutoka JWTZ kuhusu Jenerali Davis Mwamunyange

Ina maana mkuu wa jeshi la wananchi hajui kinachoendelea nchini?nadhani anatakiwa kujua habari kubwa zinazohusu nchi mf.uchaguzi,na kuzushiwa kifo kwake kama yuko popote duniani hapa.Kwa upeo wangu mdogo uchaguzi ukienda kombo, jeshi la wananchi chini yake ndo linaongoza sasa si aseme lolote kuhusu hili?
Labda yuko kwenye handaki anapata mazoezi ya hali ya juu huko Italy. Twende ubalozi wa Italy kupata taarifa za leo leo kuhusu mtu wetu.
 
Kwa yaliyokwisha kutokea sisi waoga a.k.a watz halisi tunaogopa hata kuchangia uzi huu.
Hivi kwa idadi ya tv stations zilizopo na radio ni kwa nini moja isiseme ...."sasa tunajiunga na reporter wetu aliyepo Milan tumsikie mhusika moja kwa moja ili kuondoa uvumi...."

kama yuko kwenye mahandaki anafanya mazoezi je?
 
hiv mwamnyange sio kiongozi wetu cc watanzani? Kwann msitwambie ukweli? Kama amedanja twambieni! kama mumemlisha sumu mtakuwa sio wastaarabu! Nawapa siku tatu msiponipa jibu naenda mahakani mara moja tena the Hague
 
Kwani bado yuko Milan?

Mimi najua basi, ila kwa wakazi wa miji kama Dar es Salaam wameshazoea kila siku asubuhi na jioni barabara zinafungwa ili kupisha misafara. Hivyo kama hawaoni hiyo misafara basi wanaweza kuhoji, na tutofautishe kufuatilia maisha ya watu binafsi na kuwafuatilia viongozi wetu.
Mtu binafsi hata akipatwa na lolote halitiliwi maanani sana lakini kiongozi wa kitaifa hata birthday yake inajulikana kwa umma.

Mkuu bado unaendelea tu wakati yamesema yaombwe radhi? Mimi sitaki nije nipigwe makofi humu JF kutokana na msako wa haya majamaa! Ha ha haaaaa, time will tell!

Acha woga, Tunahitaji kujua aliko? Mkuu wa Majeshi, sidhani kama ni dhambi kuomba kujua aliko,
na kama watanzania tuna wasiwasi, tunaomba watoe wasiwasi huo kwa kuonesha ukweli aliko na sio maneno.

na ikiwa kuna uwongo wowote wa kimaelezo, watoa maelezo mtakuwa mmepotezea sifa mamlaka mnazowakilisha.
 
kwa mujibu wa taarifa hii hapa siku 20 zimeshapita tangu Jenerali mwamnyange aanze ziara yake nchini Italy ; Je bado hajarudi tu? kwan ziara yake ilikua ya miezi mingapi?.anarudi lyn? there is something fishy...!!!hata waandishi wa habari wanaogopa kufuatilia hii habari Ngome..ajitokeze wanashi waondoe wasiwasi....
WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, imewataka watu waliosambaza uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, kuwa amelazwa nje ya nchi kwa ugonjwa, kuomba radhi mapema la sivyo watachukuliwa hatua.

Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali Juma Sipe, imeweka wazi kuwa Jeshi na Wizara kwa kushirikiana na mamlaka husika, wanachunguza watu hao na kuwataka waombe radhi mapema kabla ya hatua hizo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jenerali Mwamunyange ni mzima wa afya na aliondoka nchini Jumanne iliyopita Septemba 22, 2015, saa 10.45 jioni kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kwenda Rome, Italia kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Jenerali Claudio Graziano.

“Tunapenda kuwahakikishia wananchi kuwa Jenerali Mwamunyange pamoja na ujumbe wake wanaendelea na ziara hiyo kama ilivyopangwa na amesikitishwa na uvumi huo,” alisema Sipe.

Sipe alisema uvumi huo ni matumizi mabaya ya uhuru wa habari na kuupotosha umma na umeleta usumbufu kwa familia ya Jenerali Mwamunyange, Jeshi na Taifa kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa watu walisambaza uzushi huo kwamba Jenerali Mwamunyange amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya, huku wengine wakidai kuwa yuko nchini India kwa matibabu, kumuomba radhi kwa kutambua kuteleza kwao.

“Taarifa hizo ni uongo wenye kila dalili ya kutengenezwa kwa lengo la kuwatia hofu Watanzania juu ya usalama wa kiongozi huyu wa juu wa majeshi yetu, Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi, ni mzima wa afya na hayupo nchini Kenya wala sio India kama ilivyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari,” alisema Sipe.

Sipe alionya kwamba kuacha kuomba radhi, itatafsirika kuwa ni kukiri kueneza uzushi huo kwa makusudi na kwa dhamira fulani na hivyo kushawishi hatua zaidi kuchukuliwa. Alisema wizara hiyo imesikitishwa na tabia hiyo ya uzushi inayopingana na weledi na kanuni za uandishi wa habari.
 
Mambo mengine hayaeleweki hiyo ziara haina hata kavideo tumuone maana kama mzima ajisemee yeye sio mmusemee huu ni wakati wa digital aongee live na media sio picha siwezi kuamini
 
Back
Top Bottom