Taarifa kuhusu namna ya kujiunga na Ualimu baada ya kumaliza kidato cha 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kuhusu namna ya kujiunga na Ualimu baada ya kumaliza kidato cha 4

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by tata mvoni, Mar 28, 2012.

 1. tata mvoni

  tata mvoni JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  NAOMBA MWENYE TAARIFA KUHUSU NAFASI ZA KUSOMEA UALIMU KWA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE TUJUZANE. natanguliza shukrani
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Unatarajia chuo cha umma au binafsi?
   
 3. Ally chilima

  Ally chilima Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  jamani nisaidieni chuo ambacho kinaweza kumchukua aliyepata division 4 ya 28 ni msichana hata binafsi naomba msaada wenu
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Vyuo vingi vinachukua hadi div 4 ya 26 pts (nadhani hii ndio criteria ya NECTA), nadhani anaweza kuchukuliwa kwenye chuo ambako wana nafasi ya re-seat exams.
   
 5. DullyJr

  DullyJr JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,040
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Mdogo wang alipata three ya 23 lakini hakupata chuo cha ualimu,shenz zao
   
 6. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  [h=2]Tangazo kuhusu nafasi za mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na stashahada kwa mwaka wamasomo 2012/2013[/h]
  2. STASHAHADA YA UALIMU ELIMU MAALUM: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
  Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
  (a) Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi au Sayansi ya Jamii na uzoefu kazini usiopungua miaka miwili ;
  (b) Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua „Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari;
  (c) Mwalimu anayefundisha watoto wenye mahitaji maalumu (wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili nk) ni sifa ya nyongeza (vithibitisho viambatishwe).

  3. STASHAHADA YA UALIMU SAYANSI KIMU: MUDA WA MAFUNZO NI MIAKA 2
  Mwombaji awe na sifa zifuatazo:

  [FONT=&amp](a) [/FONT]Mwalimu mwenye Cheti cha Ualimu Daraja A;
  [FONT=&amp](b) [/FONT]Mwalimu mwenye Cheti cha ualimu Sayansi Kimu; na
  [FONT=&amp](c) [/FONT]Ufaulu wa mtihani wa Kidato cha 6 kwa kiwango kisichopungua 'Principal Pass‟ moja na „Subsidiary‟ moja za masomo ya ‘Biology, Chemistry and Nutrition'.

  VIAMBATISHO/ MAELEZO MUHIMU
  Waombaji wa mafunzo ya Ualimu waambatishe vielelezo vifuatavyo:
  (i) Nakala za vyeti vya ufaulu Kidato cha IV na cha VI;
  (ii) Nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti na Stahshahada (kwa Walimu kazini);
  (iii) Barua za Walimu kazini zilizopitishwa na Waajiri;
  (iv) Sifa zilizoelekezwa kwa kila kozi ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya ualimu katika vyuo vya ualimu vya Serikali na Vyuo Visivyo vya Serikali;
  (v) Wahitimu wa Kidato cha 4 mwaka 2011 na Kidato cha 6 mwaka 2012 walioomba kupitia „Sel forms‟ wanatakiwa kutuma maombi upya kwa barua;
  (vi) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya ualimu yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi;
  (vii) Barua za kujiunga na mafunzo zitatolewa na chuo atakakopangwa mwombaji kwa kutumia anuani ya yake; na
  (viii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara: WELCOME TO MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING OFFICIAL WEBSITE:::::::::, Ofisi za Makatibu Tawala (M) na Vyuo vya Ualimu.

  MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 30/04/2012.
  Maombi yatumwe kwa:
  KATIBU MKUU,
  WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
  S.L.P. 9121,
  DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)  source: WELCOME TO MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING OFFICIAL WEBSITE:::::::::
   
 7. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tafuta kazi ingine ukasomee ndugu yangu; Ualimu kwa hapa Bongo ni kutafutana lawama bure!!!
   
Loading...