Elections 2010 Taarifa: Kesi kati ya ya Mpendazoe na Mahanga ni February 3, 2011

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
kwa wale wafuatiliaji na ambao wangependa kujua kuhusu hii kesi, Itaanza kusikilizwa february 3, 2011 katika mahakama kuu hapa Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ilitolewa jana katika viwanja vya Segerea stendi jana siku ya Jumamosi ambapo Mpendazoe aliongea na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza. Aliwaeleza kuwa wapiga kura wote wa Segerea na wapenda haki wengine wafike mahakamani ili kuonesha mshikamano na itakuwa ni ishara ya kuonesha kuwa wanasikitishwa na kitendo cha mahanga kuchakachua kura zao.

Taarifa zitaendelea kutolewa kadiri zinavyopatikana.
 
Ikiwa maoni ya watu wa kawaida yataendana na maamuzi ya mahakama basi ni wazi Mahanga yuko katika hali mbaya maana killa ninayekutana naye anamponda.
 
Kutokana na mfumo wa uendeshwaji kesi bongo, inaweza kuchukua miaka mi5 kutoa uwamuzi! Kama haki ipo ipo tu. Wanazidi kilimbikiza hasira za wananchi, siku ikilipuka hawataweza kuizuia.
 
Back
Top Bottom