Taarifa juu ya zawadi za washindi wa shindano la #ChinaMade (NEW)

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,270
<<Update: 19 July, 2016>>

Habari za wakati huu Ndugu WanaJF,

Kama ilivyotangazwa awali, kwamba zawadi za simu zitakuwa zimefika Ofisi za Jamii Media, Mikocheni-Dar, kufikia Jumatatu ya tarehe 11 July, 2016 na washindi watapewa maelekezo namna ya kufika na kukabidhiwa zawadi zao.

Tunathibitisha kwamba zawadi hizo zipo tayari na kilichobaki ilikuwa ni kuandaa utaratibu mzuri wa kuzikabidhi kwa washindi.

Kwa wale washindi ambao tumewasiliana PM; tungependa muzingatie maelekezo haya upya ili kuweza kuja kuchukua zawadi;

1. Tutumie PM namba yako ya simu unayotumia
2. Tutumie copy ya kitambulisho halali chenye jina lako halisi

Zingatia

  • Utaulizwa jina lako halisi na litalinganishwa na lililopo kwenye kitambulisho
  • Namba ya simu utakayotupatia itajaribiwa ili kuhakiki.
  • Haitokubalika kutuma mtu akuchukulie zawadi, ni lazima ufike mwenyewe.
  • Kama haupo Dar na umekosa nafasi ya kuja kuchukua, zawadi yako itahifadhiwa mpaka pale utakapokuwa tayari.
Kwa maelekezo zaidi, tafadhali mawasiliano yafanyike PM.
======

{UPDATE}

Washindi waliokabidhiwa zawadi zao tayari ni;

Nifah, Tanki cognition, @Plusbee na winchester

JamiiForums inatoa pongezi nyingi kwa washindi na asanteni kwa ushirikiano wenu.

=======

Ndugu WanaJF,

Leo tunapenda kuwapa taarifa kuhusu maamuzi tuliyoyafikia kwenye utoaji wa zawadi kwa washindi wa Shindano la [HASHTAG]#ChinaMade[/HASHTAG].

UFAFANUZI KUHUSU ZOEZI ZIMA

AWALI

Itakumbukwa kuwa, mwishoni mwa mwaka jana (Nov 30, 2015), Jamii Media ilishirikiana na China Radio International kuandaa Shindano la China Made ambapo washiriki walitakiwa kutoa ushuhuda kuhusu ubora wa bidhaa na huduma kutoka China. Zoezi lilienda vizuri na tulipata washindi kama ilivyotarajiwa.

Uzi wake unapatikana hapa: Shiriki shindano la ChinaMade ushinde Simu aina ya Huawei au Xiaomi Arm Band

KILICHOTOKEA

Washindi waliopatikana walitangazwa na kuahidiwa kupatiwa zawadi zao kama inavyoonekana kwenye uzi huu: Majina ya washindi wa shindano la [HASHTAG]#ChinaMade[/HASHTAG] kutoka JamiiForums

HALI HALISI

Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, simu hizo zilichelewa kutufikia (kutoka kwa wenzetu wa CRI) na hadi sasa hazikufika kwetu. Hivyo sisi kama Jamii Media, tulikuwa tunavuta muda kuhakikisha tusinunue halafu zikawasili.

Hata hivyo, ili kulinda uaminifu na kutowaudhi wanachama wetu, na ikizingatiwa kuwa ni muda mrefu sasa umepita, Menejimenti ya Jamii Media imeshaamua kununua simu hizo na hivyo zitawasilishwa wakati wowote.

AHADI YA UHAKIKA

Kwa vile maamuzi yameshafikiwa, taarifa hii iwe rasmi kwa washiriki na washindi wote kwamba simu hizo zitakuwa tayari Makao Makuu (Ofisi za Jamii Media, Mikocheni-Dar) kufikia Jumatatu ya tarehe 11 July, 2016 na washindi watapewa maelekezo namna ya kufika na kukabidhiwa zawadi zao.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika zoezi hili.

CC: Nifah Tanki cognition @plusbee winchester
 
Ni simu aina Gani vile? Na je,kwa sababu gani mmeamua kununua nyie badala ya wadhamini wa shindano walioamua? Je,ikitokea China Radio International ikawaletea simu kipindi ambacho tayari zimeshuka bei,mtawajibika kuingia gharama?

Anyway,hongereni kwa kudhubutu kufanya hayo yote. Kila La kheri.
 
Jamiiforums Imefanya Vema Kununua Zawadi Halafu Wao Wataendelea Na CRI Wao Kwa Wao
 
Duuuuuh!Tarehe 11 si kesho jamani?
Nasubiri maelekezo ya namna ya kuifuata hiyo simu.
Hadi nilishasahau...
Asante cognition kwa taarifa.
 
@JamiiForuma ZINGATIEBI HILI. Kwa muda mliouchukua ambapo ni tangu mwaka jana wa shindano. Mimi nitashamgaa sana kama hizo simu zitakuwa ni huawei za kitoto au za kawaida tu. Inabidi mjipinde mtoe simu za maana. Na naomba washindi walete mrejesho tujue simu gani mlizowapa.
 
Back
Top Bottom