TAARIFA juu ya maombi ya CCM kuwa Dkt. Willibrod Slaa awanie ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAARIFA juu ya maombi ya CCM kuwa Dkt. Willibrod Slaa awanie ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Tumaini Makene, Feb 19, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]

  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]KURUGENZI ya Habari na Uenezi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inapenda kutoa taarifa kuhusu habari zilizoripotiwa kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, juu ya maombi ambayo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinafanya usiku na mchana ili eti Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, agombee ubunge, kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Jimbo la Arumeru Mashariki, Aprili 1, 2012.[/FONT]
  [FONT=&amp][/FONT]
  [FONT=&amp]Ingawa haijajulikana maombi hayo yanafanyika msikiti upi au kanisa lipi au sehemu ipi yoyote ile nyingine ya kufanyia maombi, Kurugenzi imeshangazwa sana na mantiki ya kuwepo kwa maombi hayo ya CCM yakionesha upendo wa kutiliwa mashaka kuwa chama hicho kimefikia mahali kinaweza kufanyia maombi vyama vingine ili vipate wagombea makini wa kukibwaga vibaya sana katika uchaguzi.[/FONT]
  [FONT=&amp][/FONT]
  [FONT=&amp]Kurugenzi inapenda kusema yafuatayo juu ya maombi hayo ya CCM, ambayo kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, kama ilivyoripotiwa katika njia mbalimbali za upashanaji habari, imedhihirika dhahiri kuwa ni maombi yanayoongozwa zaidi na hila, husuda kwa CHADEMA na Katibu Mkuu wake, Dkt. Slaa;[/FONT]
  [FONT=&amp][/FONT]
  [FONT=&amp]Tunapenda CCM wajue kuwa CHADEMA na viongozi wake makini, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Slaa, si watu wa kurudi nyuma. Chama hiki daima muda wote kinapanga mikakati na mipango ya kusonga mbele, kikionesha utawala mbadala, kikijiandaa kushika dola na kutekeleza malengo ya Watanzania![/FONT]
  [FONT=&amp][/FONT]
  [FONT=&amp]Kwa mantiki hiyo, chama hiki hakiwezi kurudi nyuma, hakiwezi kumrudisha nyuma Katibu Mkuu wake, Dkt. Slaa kuwania ubunge. Kiongozi huyu makini, ambaye umma wa Watanzania una imani kubwa naye, ameshavuka viwango vya ubunge, si mtu wa kuwania nafasi ya ubunge tena, (is not parliamentary material).
  [/FONT][FONT=&amp][/FONT]
  [FONT=&amp]Kwa nafasi yake ndani ya CHADEMA, anao wajibu mkubwa kujenga chama. Kwa kutimiza wajibu huo, Dkt. Slaa anafanya kazi ya kutengeneza na kuivisha watu wengine makini zaidi, kuweza kuwa viongozi ndani ya chama, nafasi za udiwani na ubunge, ili kuendeleza umakini na uimara wa chama hiki ambacho dhahiri ni tumaini jipya la Watanzania katika kutoa uongozi mbadala wa nchi.[/FONT]

  [FONT=&amp][/FONT][FONT=&amp]Kwa umakini wa CHADEMA, uwezo wa Dkt. Slaa na matumaini makubwa ya Watanzania, ambayo wameendelea kuyaonesha kwa chama hiki tangu mwaka 2007, kilipoanzisha rasmi mapambano dhidi ya ufisadi na mafisadi, kisha kudhihirika wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, nafasi pekee inayomstahili Dkt. Slaa ni urais kwa maana ya kuwa ni ‘presidential material', si ubunge.[/FONT]
  [FONT=&amp][/FONT]
  [FONT=&amp]Lakini pia, tunatambua kuwa CCM, wameweza kutoa kauli hiyo ya kukurupuka baada ya Dkt. Slaa kuwa tayari ametamka wazi tangu awali na kurudia kauli yake thabiti mara kadhaa kuwa hana nia wala mpango wa kuwania ubunge mahali popote pale nchini. Hawezi kufanya hivyo kwani hata ubunge wa Karatu hakushindwa bali aliacha mwenyewe kwa hiari yake, ili kutekeleza mahitaji ya umma wa Watanzania.[/FONT]

  [FONT=&amp][/FONT][FONT=&amp]Kurugenzi ya Habari na Uenezi inatumia nafasi hii kuwaambia CCM kuwa watambue CHADEMA ni chama makini. Kimedhihirisha hivyo mara kadhaa katika masuala makubwa kwa maslahi ya Watanzania. Kitaendelea kudhihirisha hivyo pia katika uchaguzi wa Arumeru kwani kina utaratibu wa kuwapata wagombea wake, kutokana na maamuzi ya wanachama wake.[/FONT]
  [FONT=&amp][/FONT]
  [FONT=&amp]Tunatambua kuwa kauli hiyo ya CCM pia ni sehemu ya mkakati wa makusudi kuwakatisha tamaa baadhi ya watu wanaotaka kugombea jimbo hilo kupitia CHADEMA. Kurugenzi ya Habari na Uenezi inapenda kusisitiza taarifa ya awali, kuwataka wanachama wetu wajitokeze kwa wingi kuwania uteuzi wa kugombea ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki.[/FONT]

  [FONT=&amp][/FONT][FONT=&amp]Tunataka CCM wajue kuwa suala la kuteua mgombea wa CHADEMA ni la CHADEMA yenyewe, kwa kutumia utaratibu wake, ikiongozwa na katiba, kanuni na mahitaji ya umma, wala hatuhitaji ushauri wa chama ambacho kadri siku zinavyokwenda, kinadhihirisha kila dalili ya kuchoka kujisimamia chenyewe, kusimamia wanachama wake, kusimamia serikali na maendeleo ya watu, hivyo kupoteza kabisa ushawishi kwa wananchi. Wala hatujawahi kuomba ushauri kutoka kwao hata siku moja.[/FONT]

  [FONT=&amp][/FONT][FONT=&amp]Lakini maombi hayo ya CCM, kama ambavyo Nape amenukuliwa katika vyombo vya habari akisema, yamedhihirisha namna ambavyo chama hicho bado kinaandamwa na mzimu wa CHADEMA na Dkt. Slaa tangu baada ya uchaguzi mkuu, kwa kuiba kura na kuvuruga matokeo ya uchaguzi huo.[/FONT]

  [FONT=&amp][/FONT][FONT=&amp]Kauli ya Nape kuwa iwapo maombi yao yatafanikiwa na Dkt. Slaa akawania ubunge, CCM watakuwa wamemaliza kazi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, inathibitisha tuhuma hizo na namna ambavyo CCM hakikushinda kwa haki uchaguzi huo.[/FONT]

  [FONT=&amp][/FONT][FONT=&amp]Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya pia inataka CCM waelewe kuwa umaarufu wa CHADEMA hautokani na umaarufu wa mtu mmoja mmoja wala hausubiri matukio pekee, bali unatokana na uongozi makini, kuanzia ngazi ya taifa hadi ya msingi, kikijikita katika kusimamia masuala yenye maslahi kwa Watanzania na nchi yao muda wote! [/FONT]


  [FONT=&amp]Imetolewa leo Februari 18, 2012, Dar es Salaam na [/FONT]


  [FONT=&amp]Tumaini Makene[/FONT]
  [FONT=&amp]Afisa Habari wa CHADEMA[/FONT]
   
 2. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kweli inaonyesha hamna cha kufanya.
   
 3. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  he!.....................kumbe Dr. slaa alishakuwa mgombea urais wa kudumu wa chadema??.................. mie sikulijua hili!!.................. mnarudia yaleyaleee...................

  halafu si vyema chama kuwa na dharau namna hii..................... nani kasema ubunge ni kazi ndogo na duni sana kiasi ambacho ni aibu mtu kama slaa kuifanya??................... kwa hiyo slaa sasa ni superior kwa wabunge wote?................. hivi mnajua kuwa hata rais kibaki na odinga wa kenya ni wabunge mpaka sasa?................ so slaa yuko kwenye viwango vya juu hata ya kibaki na raila??................... hebu acheni kudharau kazi ya ubunge na wabunge wetu................. tumhwshimu kila mtu na kazi aifanyayo kwa maslahi ya taifa tafadhari...............

  mtaharibu chama chenu sasa na hii kasi ya kumjibu kila mtu chochote asemacho....................... mingine ni mitego tu, msiwe mnajibu.................. ni ushauri tu wakuu.......................
   
 4. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mmeanza kupoteza mwelekeo... maana hata Lipumba na Sharif walijiona ni presidential materials, wakaishia kuwa madikteta wa vyeo! Siku yaja mtakula haya maneno, or die trying kulazimisha udikteta wa Dr. Slaa!
   
 5. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  hapa lazima mtu aangalie wakati.si kwamba ubunge kazi ndogo ila kwa sasa katibu mkuu huyu hawezi tena kurudi kuchukua ubunge.kuna hoja ya umri kwa sasa.dr slaa ana umri ambao kama tungetaka kuainisha ukomo basi watu wote wenye umri huo hawapaswi kugombea ubunge.mbowe aligombea urais na baadae akaja kugombea ubunge.ukitazama hilo utakuta umri wake unamruhusu kufanya hivo.wakati anagombea urais mbowe alikuwa na 44 years.hivyo,taarifa ya makene ni sahihi.dr slaa kwa sasa ni mtu wa kujenga na kuandaa vijana kushika hatamu. Na haijaelezwa kuwa atagombea urais ila ikionekana anafaa tutamuunga mkono agombee tena kwa mara ya mwisho.kwa sasa cdm haijaamua na wala haijatangaza hilo.mnaopinga pinga humu.tafakarini kwanza.
   
 6. T

  Twaa Member

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ndio msimamo wa mambo, ubunge sii kitu! Kama ubunge ungekua na maana Kwanini Tanzania tuna sheria mbovu? Na hizo sheria mbovu zimetungwa na bunge? Ubunge sii kitu kama bunge linalotokana na ubunge linashindwa kuiwajibisha serikali hilo ni bunge? Kazi ya bunge nini? Kwanini bunge linaitetea serikali ilehali bunge linapaswa kuiwajibisha serikali? Kwanini Sisi watanzania tunakua maskini wa fikra(poverty mentality)? Unahitaji kwenda shule ili ujue ubora wa bunge letu? Je kama wabunge wangekua wanalipwa mishahara kutokana na taaluma zao watu wangekimbilia kuwania ubunge? Umaskini na uroho /uchu wa pesa ndio unaomfanya mtu akimbilie kuwania ubunge kanakwamba ubunge ndio solution ya umaskini! Na pia Dkt Slaa hatagombea ubunge kwa kigezo eti yeye ni mgombea wa kudumu wa urais hapana Dkt yupo kwa ajili ya kuwafunda vijana ndani ya chama wawe kama yeye, watambue u muhimu wa maslahi ya taifa kwanza na pia umuhimu wa kutoa haki kwa mtanzania wa leo na kesho! Dkt yupo ajili ya CHADEMA na watanzania kwa ujumla na sio kwa ajili ya urais!
   
 7. k

  kibunda JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tumaini uwe makini unapoandika statement zako. Epuka kuweka maneno yenye utata, majivuno, dharau ama kujidai. Be straight and to the point. Hata mimi sikupenda baadhi ya maneno uliyotumia. Aidha, sidhani kama ni msimamo wa chama kudharau nafasi ya ubunge. Hali kadhalika, sidhani kama ni msimamo wa chama kuonyesha mwelekeo wa mgombea urais wa 2015. Bado naamini CDM ni chama makini. Mnaweza kuliweka vizuri suala hili.
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ndio nini hiki?
   
 9. k

  kibunda JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ikumbukwe kuwa Mbowe alisema ni Ruksa Dokta Slaa kungombea kama akiamua. Lakini taarifa hii ya Tumaini inapingana na statement ya M/kiti. Tafadhali CDM msituchanganye!
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Sikuona umuhimu wa CDM kumjibu Nepi. Haina maana,wangempotezea.
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Walistahili kumjibu ajue Dr. Slaa is Presidential Material. Nape anawaza 2015 tu utafikiri anatumia makalio kuwaza
   
 12. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  yes 100%
   
 13. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #13
  Feb 19, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,779
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mshauri W. Mkama katibu wa CCM akagombee ubunge Arumeru!......... Kwani yeye hapendi kuingia mjengoni?!................. Au hata wewe hupendi kuingia mjengoni?............... Nakushauri kama CCM wakikubania jiunge na CCK au CCJ si ndo pacha wenu najua watakukubali ili ulikomboe jimbo la Arumeru na kukufanya uingie mjengoni!............
   
 14. M

  Molemo JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Habari nzuri sana hii.Imetulia..
   
 15. M

  Mkolakumwezi Member

  #15
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa maelezo haya ccm kazi mnayo hyo 2015.
   
 16. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,322
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri kuihabarisha jamii juu ya taarifa zilizozagaa za dr Slaa kugombea ubunge Arumeru.

  Magamba fanyeni yanayowahusu ya cdm waachieni wao.
   
 17. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  JF imekuharibu wewe kijana Tumaini Makene! ****** unaongelewa kwenye jukwaa hili si wa kupelekwa nje officially! Yaani taarifa yako imekuwa kama MCHANGO kwenye THREAD ya JF!
   
 18. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #18
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Huyu ndiyo mrithi wa Regia Mtema?
   
 19. Mr.mzumbe

  Mr.mzumbe JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 803
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 60
  Kiongozi huyu nae ni wale wale kasoro tarehe tu.Alikuwa na hamu ya kuuza sura huyo,sasa ndio kasema kinini hapo!!!utapia-mlo mtupu.
   
 20. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #20
  Feb 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Asante kwa kusema ni ushauri tu. CHADEMA kwa maana ya chama kizima, iwe makao makuu, ngazi ya mkoa, wilaya, jimbo au mabaraza yake au kiongozi mmoja mmoja, hakijawahi kumjibu "kila mtu chochote asemacho". Mitego inafahamika na namna ya kuitegua pia. Kauli ya Nape haikuwa mtego.

  Haijasemwa kuwa Slaa ni superior, wala hakuna mahali imeoneshwa kuwa ubunge ni kazi duni, kwani haiwezi kuwa duni, bali kuna wabunge ni duni, bila shaka hata wewe unawafahamu. Bila shaka unajua hata ni wa chama gani. Wamekuwa wakijidhihirisha hivyo pasi na shaka yoyote! Walio na uwezo, bila hata kujali party affiliation, wanaheshimiwa sana na jamii nzima ya Watanzania!

  Hakuna mahali kabisa imeelezwa kuwa Dkt. Slaa ni mgombea urais wa kudumu wa CHADEMA, hakuna!
   
Loading...