Taarifa hizi za uhakiki wa majina ya mshahara zina ukweli?

Lundavi

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
327
323
Jamani kuna taarifa zinaenea juu ya kuhakiki majina yanayotumika kwenye Account ya mshara na Yale yanayooneka kwenye salary slip ni kweli? Yaani wanataka jina linaloonekana kwenye salary slip yafanane na yanayoonekana kwenye ATM.
 
Mbona halmashauri nyingine watumishi hawana taarifa yoyote?
 
Kama account yako ya bank ina majina matatu na kitambulisho chako cha kazi kina majina mawili, rekebisha jina la kitambulisho kwa mwanasheria au mahakamani haraka kabla ya mwaka mpya wa serikali kuanza kwani jina lako litaondolewa kwenye mishahara
 
Kuna halmashauri mpaka Leo watumishi wake hawajapewa vitambulisho vya kazi, wakifanya hivyo utakua ni uonevu.
 
Namna nyingine ya kupiga chenga kale ka increment alikoahidi wakati WA may mosi.....hatutaweza kutoa increment kwani inaelekea kuna watu wanatumia account hewa !!!
 
Ni kweli mkuu,mfumo wa ulipwaji mishahara unabadilika kutoka hazina kwenda BOT to benki kuanzia july (kwa mujibu wa taarifa tuliyopewa) ndio mana kuna huo uhakiki,ni vema ufatilie mkuu usijekosa mpunga mnono july,.
 
Poa bhana ngoja tuendelee kuhangaikia maana tuliipenda wenyewe.
 
Back
Top Bottom