Taarifa hizi za mauaji zinafichwa kwa manufaa ya nani?

Duh mbaya sana! Hiyo si Tafrani kama ulivyoiita. Hiyo ni A DISASTER,MAYHEM,DOOM,etc. Usishushe viwango vyake. Yaani hii inanikumbusha Tunisia kipindi cha Ben Ali! Aliwatumia vibaya polisi kulinda maslahi yake. Na waliogopeka hakuna mfano wake! Lakini huwa yana mwisho.
 
Ndugu wanajamvi.

juzi mjini dodoma katika jitongoji cha njendengwa kuna vurugu zilijitokeza wakati wananchi zaidi ya 2000 (nyumba)500 walipobomolewa nyumba zao na tinga tinga kumpisha mwekezaji....

katika tafrani hilo ambapo polisi walichukuliwa nje ya mkoa (inasemekana morogoro) walipambana na raia wakazi wa pahala pale tangu uciku wa manane kukataa kubomolewa makazi yao......polisi wa dodoma walikuwa bize kujionyesha mtaani na yebo yebo zao kuwa hawahusiki....

ilikuwa ni tafrani la mwaka, ambapo hata kwenye magazeti risasi za moto zilitumika, japo hazijaripoti waliouwawa....

jumamosi hiyo mbaya nilikuwa mjini dodoma mishale ya saa 5 nilipopata taarifa kuwa teyari raia 6 na askari 3 wameishauwawa. hadi jioni nilipata taarifa kuwa ni watu 16 wamefariki....japo zinahitaji kuhakikiwa......

it has been shame. baadhi ya masimulizi niliyoyapata toka kwa wakazi wa eneo hilo

1. mama amepigwa risasi na polisi, kaanguka kifo, mtoto kapanick, kampiga jiwe polisi, polisi kamshoot mtoto to death, mtu katokea nyuma kampiga bisu polisi to death.............

2. polisi kapigwa mshale kwa nyuma tokea chooni, kaanguka kafa.....

3. baba kawakumbatia watoto wake ndani ya nyumba ili wafe pamoja, wakabomolewa na kuuwawa na tingatinga......

4. kulikuwa na babu kilema mguu mmoja kagoma kutoka, wakampiga risasi mguu wa pili ulio mzima.....

(inahitajika wanaharakati kama amnesty international na NGO nyengine kuja dodoma kupata taarifa halisi za tafrani hili linaloonekana kama la mchezo lakini ni massacre..)

maswali magumu

1. how comes habari hizi hazijasomwa hata kwenye gazeti moja? kumbe ni wengi wanaouliwa na taarifa zao kuishia hewani?

2. kwa nini serekali isikiri kwamba kuna udhaifu katika kugawa viwanja hadi kuwalazimu watu kuhamia maeneo bado wazi? na hilo linapotokea, je inahitaji PhD ya sociology kukiri kosa na kumrealocate mwekezaji?

3. je kwani mwekezaji alinunua eneo liwe mgodi kiasi hakuweza kuhama?

4. je is it health KWA TAIFA kwa taarifa za mauaji katika kugombea ardhi kuwa EMBARGO?





i

Ingekuwa ni kweli gazeti la CDM Tanzania Daima wangeandika, huu ni uzushi na habari za umbeya humu JF tuliisha zipiga marufuku. CRaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap
 
Uwezekano wa taarifa kutoandikwa au kutangazwa ni mkubwa. Binafsi,nimewahiona na kusikia kwa macho na masikio yangu'waandishi wa habari wakipigwa mkwara na polisi wasiandike mwenendo wa kesi fulani vinginevyo watakuwa hawapati taarifa. Taarifa mbaya kwa polisi zinakatazwa kutangazwa ila zilizo nzuri (kwao polisi) ndio huziitia waandishi kuzisikia na kkuzitangaza.

Na kama mfumo huo hutumika Dar es Salaam kwa mji mdogo kama Dodoma linawezekana vsana. Amini kuwa watu wameuawa kwa kuwa wananchi toka awali walionekana kusimamia haki yao. WATU WAMEUAWA KWELI.

Kama polisi hao wanauwa mara kwa mara, mfano, Nyamongo-Tarime zaidi yatu 7, Ubaruku Meya watu wawili, Arusha watu watatu, Misitu ya pande-DSM watu watatu na kadharika na kadharika. JE POLISI HAO HAO, MAKAMANDA WAO WALE WALE, MAFUNZO YAO YALE YALE, NA ZAIDI WATAWALA WAO WALE WALE KWANIINI NA KWAVIPI WASIUWE DODOMA? Dodoma watu wameuawa KABSAAAAAAAAAAAAAAA!

Nakubali kuwa kuna uwezekano kwa waandishi wasiandike habari fulani lakini sio kuficha maafa/vifo. Wanaotakiwa kuthibitisha taarifa za vifo ni polisi na madfakitari, hata kunapotokea ajali, ukashuhudia miili inapandishwa kwenye magari, anayethibitisha vifo ni daktari.

Hivyo kwenye kadhia hiyo ya Dodoma, inaweza uliowashuhudia ukidhani wamekufa, kiukweli, hawakufa bali wamejeruhiwa tuu!.

Magazeti yanasubiri taarifa rasmi ndipo yaandike.
 
Nakubali kuwa kuna uwezekano kwa waandishi wasiandike habari fulani lakini sio kuficha maafa/vifo. Wanaotakiwa kuthibitisha taarifa za vifo ni polisi na madfakitari, hata kunapotokea ajali, ukashuhudia miili inapandishwa kwenye magari, anayethibitisha vifo ni daktari.

Hivyo kwenye kadhia hiyo ya Dodoma, inaweza uliowashuhudia ukidhani wamekufa, kiukweli, hawakufa bali wamejeruhiwa tuu!.

Magazeti yanasubiri taarifa rasmi ndipo yaandike.

Bulldozer usiku wa manane,Risasi za moto, mabomu, mishale, mapanga na mikuki halafu eti uliowaona ni wanaweza kuwa majeruhi dah! muuaji yyt lzm aapuuzie hili!
 
ndugu yangu mmoja alikuwa na kiwanja huko na alifika pale.....jirani na kiwanja chake kulikuwana nyumba na ndani ya nyumba kulikuwa na mama mjamzito...yule mama alitka nje na alipoona tinga ntina linakuja kubomoa nyumba yake alipaza sauti akasema basi na mimi mniue tu.....akarudi ndani ...tinga tinga likaja moja kwa moja likabomoa nyumba na yule mama akafia ndani ......

hii nimeambiwa jana na jamaa yangu nae anashangaa kuona hakuna hatua yoyote wala taarifa yoyote iliyoandikwa na vyombo vya hbari wala hatua zozote kuchukuliwa
Mgetuwekea angalau kapicha yaani ingekuwa vizuri sana maana hawa jamaa hawachelewi kukanusha maana hata JF sielewi inakuwaje kuna baadhi ya thread zinapotea kimya kimya tu na mara nyingi ni sile zinazo ichoma serikali kwenye kidonda...
 
JF tuweni watu ambao tunachukua wajibu wakufatilia habari tunayoiripoti na kuleta kitu kilichokamilika. Tusipofanya hivyo kwa kupost na kusubiri watu wengine wafatilie tutakuwa tunaishia hivihivi.

Lazima tubadilike kama tunataka na wengine wabadilike na watu wajue kuwa habari inayowekwa JF imekamilika na siyo udaku.

Tunaomba mleta habari achukuwe jukumu la kutafuta ukweli wa habari hizi zikiwemo picha na shuhuda za waathirika.
 
Mkuu Charity inaanzia nyumbani.. Kama ulivoweza kuweka hii thread hapa, pia weka kwa social networks zote maarufu hapa nchini na nje, kila mmoja asome, mwisho wake wataona aibu watajibu tu. Ikiwezekana kwa kutumia kamera ya simu yako chukua video clips ukiwahoji wahanga baadhi then zipost youtube watanzania wengi ndani na nje wataona na dunia itaona pia.... Naamini tutafika mahali.

Roho zao marehemu zipumzike kwa amani

Mkuu nimeipenda sana hii, hapa JF tumekuwa mabingwa sana wa kusikitika, kulia, kushangaa, kucheka na hata wakati mwingine kutukana kwa hasira. Ni mara chache kukuta mtu hapa JF akitoa ushauri nini kifanyike ili kutatua tatizo husika, asante sana kwa ushauri wako Mkuu.
 
Mgetuwekea angalau kapicha yaani ingekuwa vizuri sana maana hawa jamaa hawachelewi kukanusha maana hata JF sielewi inakuwaje kuna baadhi ya thread zinapotea kimya kimya tu na mara nyingi ni sile zinazo ichoma serikali kwenye kidonda...

Tujaribu kufuatilia, hii thread ikipotea humu jamvini tuulizane hapa JF nini kinaendelea...
 
kwa kweli naogopa kusema nimeanza kukata tamaa kabisa na nashindwa kuelewa vizuri mbaya mno! hata vyombo vya habari vimetusaliti achilia mbali daktari tuliyemsomesha kwa fedha ningi asimamie afya zetu ameshindwa kusema ukweli? hii imekaa vibaya sana rpc yeye yuko bize na mwenge!
lakini cha kujiuliza je ni kweli dodoma tumefikia kugombea ardhi kiasi hiki?
lakini linalosikitisha ni kwa nini wanaotajwa kwenye migogoro ni wale wale kila siku?
ni kweli tumefika mahali serikali haioni umuhimu wa kutoa tamko la maana kuhusu hili? mbaya zaidi nasikia kuna ulinzi mkali kuhusu maiti za tukio hilo
hivi ni kweli tukae kwa habari za kubahatisha tukisikiliza ukweli ukishindwa kukanushwa kuwa ni uzushi?
naogopa lakini lijalo ni kubwa mno na siku sinahesabika
wasijione wamefanikiwa damu ya mtu haipotei bure ipo siku kwa uwezo wa mungu tutaujua ukweli lakin hata tusipo jua mkono wa mungu hautawaacha.
 
Hakuna alie fariki waliumia tu. ITV,TBC,Star tv na magazeti mwananchi,Tanzania Daima,Majira walifika eneo la tukioa hakukuwa na mtu aliepoteza maisha
 
Hakuna alie fariki waliumia tu. ITV,TBC,Star tv na magazeti mwananchi,Tanzania Daima,Majira walifika eneo la tukioa hakukuwa na mtu aliepoteza maisha
 
kaka naomba nikushauri kitu... hii ni story kubwa sana na inaweza kuleta msisimko mkubwa kwa wananchi! ungejaribu kwenda au kupiga simu hata dodoma mjini na kutafuta mwandishi mmoja akaenda ku-cover hiyo stori....hivyo ndio watu hufanya siku hizi tena kama upo sharp na unauhakika nilo jambo unaweza hata kuwatumia sms BBC na wakatuma mwandishi wao huko (pengine unaweza kuwa hauna namba yao but si mbaya kama simu yako ina mtandao then namba unaipata fasta tu through searching)
Haya ni moja kati ya mambo yanayoleta vurugu na kutukosesha amani kabisa katika nchi yetu
 
Kama ni kweli au uongo tutajua baadae....lakini tunachojua kwa uhakika ni kuwa vyombo vyetu vya habari vingi ni legelege kwenye kutoa taarifa. Yaani ni kama wanaombaga ruhusa kutoa au kutotoa habari. Mfano tukumbuke ilivyokua majuzi kwenye ajali ya boti Unguja...ilichukua masaa mangapi kuanza kuona habari kwny vyombo vyetu...ingawa CNN,BBC walikua wameshatangaza..
RIP wote na pole kwa familia zilizopoteza makazi
 
Back
Top Bottom