Taarifa full-operesheni tokomeza

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,534
12,375
Katika pita pita huku na kule nimefanikiwa kupata hii taarifa iliyoleta kiza zaa Bungeni leo na kusababisha Waziri Balozi Kagasheki kujiuzuru, na wengine nafasi zao kutenguliwa na mh rais.

MY TAKE:
Lengo la hii operesheni halikuwa baya hata kidogo, Mh. Kagasheki amewajibika kwa sababu tatizo limetokea ndani ya wizara yake.

Ukweli ambao mimi nauona hapa kwa (mtazamo wangu) ni kwamba kuna syndicate fulani hapa imefanya jambo hili lionekane kubwa zaidi ya madhara ya ujangili na hivyo kufanya baadhi ya wahusika wakubwa kwenye hili wasibainike kitu ambacho hadi kwa hatua hii wameweza.

USHAURI:
Hata kama Kagasheki hatarudi kwenye cabnet, Operesheni hii isiwe mwisho, itafutwe namna nzuri ambayo haitaleta madhara kwa jamii ikiwa ni pamoja na majeshi kuelimishwa kuwa siyo vita lakini pia jamii kuelimishwa kutokuwa wakaidi wanapoobwa ushirikiano kwenye ufanikishaji wa kutokomeza ujangili.

Nasisitiza Kujiuzuru kwa Balozi Kagasheki ni auheni kwa majangili ambao wengi wao wapo kwenye mfumo wa sasa wa utawala!
 

Attachments

  • TAARIFA- OPERESHENI TOKOMEZA.pdf
    115.5 KB · Views: 1,171
Mkuu asante..ilitaka kufichwa hii.hadivijitabu havikutolewa kwa wabunge ndipo Mh TL akaomba bunge liahirishwe..vichapishwe na wabunge wagawiwe wapitie ripoti hii ya UCHUNGUZI kabla ya kuchangia.
Yaani kazi ya TISS inafanywa na wabunge?
 
Acha awajibike, operesheni ya nini wakati majangili wanafahamika? Ile ilikuwa zuga tu.
 
Majangili sasa wamepata Kichwa sijui kama atakayechukua wizara ataweza kufanya crean up
 
Wakati wa operesheni hii mimi nilikuwa kwenye kijiji kimoja kule Ulanga watu walikuwa wanapigwa bila sababu wakiwa majumbani na hata njiani au shambani nilishangaa siku moja kuona akina mama wakikimbia na matenga ya mboga vichwani wakidai wemzao wanabakwa oh so bad
 
Too bad! Nimeisoma na kustushwa sana. Tanzania imefika mahali pabaya mno as far as human rights record is concerned. Ubaya mwingine ni kwamba katika pangua pangua hiyo manaibu mawaziru wabaya kuliko kawaida watapanda kuwa mawaziri kamili na hali itakuwa mbaya zaidi.
 
Wengi wetu tunashabikia tu bila kufikiri kwa kina maana ya operation na hasa zile zinazojumuisha majeshi. Madhara ya aina yoyote ile na hata mabaya kuliko hayo hutarajiwa kwani walengwa hujiingiza na kujifanya sehemu ya operators kwa kuwaweka watu wao ili kuleta madhara kwa makusudi na hivyo kukwamisha nia njema iliyokusudiwa.
Ni kweli majangili wameshinda kwa kupitia bunge kwani katika bunge wapo wahusika waliotuhumiwa. Rai yangu kwa Kagasheki awataje kwa majina yao wote ambao anawajua wanafanya biashara ya vipusa bila kuogopa ili wananchi tuwafahamu. Asiogope kwani hana cha kupoteza.
 
Nafikiri sasa imefikia hatua nzuri na tamu maana hawa wanaojiuzulu na wale ambao uteuzi wao umetenguliwa zamu yenu kujibu mapigo PIGA NIKUPIGE wamemwaga mboga mnaangalia ugali wa nn sasa? Mwagaaaa tulale njaa wote :israel::halafu sisi watazamaji tu shangilie kihivi lock1::lock1: wakati mkulu anakuna:crazy::der: wananchi amkeni mjue haki zenu
 
Nafikiri operation ilitakiwa ifanywe kimya kimya bila hata kupiga watu, sio rahisi kukamata majangiri kwa kupiga piga wananchi, kupiga watu ni mbinu dhaifu sana na ya watu wasiotaka kutumia vichwa kufikiri.
 
Kuna wakati nikiwa Karagwe nilisikia kupitia redio FADECO mambo yaliyozungumzwa katika mkutano wa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa (CHAWAKAZI) uliofanyika Biharamulo; hakika utajua kuwa wafugaji wanatamba kwamba wao ndio waliochochea suala hili na hata serikali ingeweza kuanguka. Ni mengi yalizungumzwa na mzungumzaji alitamba kwelikweli ma kusema wafugaji ndio walichochea suala hili baada ya kupandikiza wabunge wao. Kwa namna anavyozungumza unaweza kuhisi kuwa kuna wabunge walipewa kitu kidogo ili mpango mzima ukamilike.
Siwezi kuelewa kwa nini watanmbe hivyo, ni fedha ya ng'ombe au kuna fedha za ziada?
Hakika tutakuja kujua zaidi baadae.
Kama JK hakujua kilichozungumzwa katika mkutano huo basi anaweza kupata toka redio fadeco.
Sishabikii mabaya yaliyotokea, nayachukia sana, ila kwa namna mkutano ilivyokuwa mtu unaweza kushawishika kuwa hao waliotenda mabaya yawezekana walikuwa wamepandiklizwa ili operesheni ichukiwe. Of course, unapandikiza wachache na wengine wengi wanawaiga hao bila kujua mkakati
 
Back
Top Bottom