Taarifa: Chadema ihamasishe uandikishaji wapiga kura wapya:

YAGHAMBA

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
545
147
Napenda kuipongeza Chadema kwa kazi kubwa waliyokwisha kuifanya hadi sasa ktk kutoa elimu ya uraia ambayo watawala wa mabavu (CCM) hawataki iwafikie watanzania walio wengi na wanafanya kila njia kuhakikisha wanazizima juhudi hizo, msirudi nyuma. Naiomba CHADEMA ukifika wakati wa kuiboresha daftari la kudumu la wapiga kura wafanye oparesheni maalumu nchi nzima ya kuhamasisha vijana kujiandikisha kwa wingi na kuzitunza shahada zao hadi wakati wa kupiga kura, hili litasaidia sana kuwaondoa CCM 2015 kwani watashindwa kuwahonga na kuzinunua shahada sababu zitakuwa nyingi sana.
 
Ni ushauri mzuri naamini wakuu wanapita sana hapa na hope watafanyia kazi.
Na kwa kweli kwa wasiojua ni kuwa bado watz hawajapata nafasi nyingine ya kujiandikisha ili kuwa na wigo mpana wa kutumia ipasavyo uhuru wao wa kuchagua,nakumbuka mara ya mwisho ni kabla ya uchaguzi mkuu 2010 na ninaamini huko tuendako watz wakipata fursa ya kujiandikisha basi 2015 msiba mzito ccm.
 
Baada ya hii M4C, hilo la vijana kujiandikisha litakuwa zoezi jepesi sana. Kuna wapiga kura wapya yapata milioni 4 ambao kati yao CCM ina chini ya 28% (According to an independent research) 2014 uchaguzi wa mitaa baada ya regista ya wapigakura kuboreshwa itakuwa kiama kwa magamba. Wacha wajiliwaze kwa kata walizoshinda.
 
Back
Top Bottom