Taarifa:Aliyegushi vyeti ili kupta ajira hana haki ya kiinuamgongo au malipo ya aina yoyote ile.

moma2k

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
1,091
1,404
Kisheria kugushi vyeti ni kosa la jinai kwa mujibu wa S.120 Penal Code, akitiwa hatiani na mahakama yenye mamlaka(A court with competent jurisdiction), adhabu yake ni miaka 7 jela.

Binadamu aliyegushi vyeti huku akijua, ili ajipatie ajira kwa udanganyifu, huyu ni criminal. Hastahili kupata malipo ya aina yoyote ya kiajira hata kama alikuwa ktk ajira hiyo kwa miaka 20.

Hoja ya msingi ni kwamba hakuwemo kwenye ajira hiyo kihalali na kisheria.Hivyo hana kinga ya aina yoyote ya kisheria kuhusu malipo hayo.

Kilicho halali kwake ni kukamatwa na polisi, kupelekwa mahakamani kwa kosa la jinai la kugushi vyeti, ili haki ikatendeka huko.Huu ndo ukweli wa kisheria.No more no less.
 
Mkuu, umemaliza? Utapata faida gani wewe?
Atakuwa hana ajira huyo. Anategemea kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wahanga. Hivyo kwake ni sherehe lakini hajui kama upande wa pili kuna tatizo la kijamii limejitengeneza hapo.
 
Hawa enye vyeti feki waiiba fursa za watanzania maskini wenye vyeti safi. Hawa ni watoto wa matajiri,lazima waburuzwe mahakani. We want justice to prevail as well as the rule of law. Wanatibu watu kumbe ni mdaktari feki.Hii ni hatari sana kwa afya za watanzania.
 
pole sana. Nipo kwenye ajira tangu 2003. Mwanasheria na mtetezi wa walalahoi wenzangu.
 
Unasema kweli vipi mkurugenzi na afisa utumishi siwalishirikiana kumpatia ajira mwenye cheti bandia wataunganishwa kwenye kesi.
 
Hapa serikali ishitakiwe kwa kuhatarisha maisha ya watu kwa kuajiri watu wasiokuwa na sifa.
 
Serikali kama mwajiri ilikuwa na wajibu wa kujiridhisha na vigezo vya inayemwajiri.

Mathalani serikali ilishaweka mifumo ya kuangalia ufanisi wa watendaji mfano kupitia OPRAS. Kama mtu amevuka vyote hivi miaka yote nadhani hatuna budi kukubaliana kimsingi kwamba pande zote zimekuwa na dosari.

Amefanya kazi, amechangia mifuko ya pensheni acheni udhalimu mpeni mafao yake baada ya kumwachisha kazi kisheria baada ya kuthibitisha kwamba anakosa vigezo!
 
Kisheria kugushi ni kosa la jinai kwa mujibu wa S.120 Penal Code, akitiwa hatiani na mahakama yenye mamlaka(A court with competent jurisdiction), adhabu yake ni miaka 7 jela.

Binadamu aliyegushi vyeti huku akijua, ili ajipatie ajira kwa udanganyifu, huyu ni criminal. Hastahili kupata malipo ya aina yoyote ya kiajira hata kama alikuwa ktk ajira hiyo kwa miaka 20.

Hoja ya msingi ni kwamba hakuwemo kwenye ajira hiyo kihalali na kisheria.Hivyo hana kinga ya aina yoyote ya kisheria kuhusu malipo hayo.

Kilicho halali kwake ni kukamatwa na polisi, kupelekwa mahakamani ili haki ikatendeka huko.Huu ndo ukweli wa kisheria.No more no less.
Naona marinjirinji ipi bora kukaa na kupewa stahiki then kuadhibiwa au kusepa kimya kimya?
 
Kisheria kugushi ni kosa la jinai kwa mujibu wa S.120 Penal Code, akitiwa hatiani na mahakama yenye mamlaka(A court with competent jurisdiction), adhabu yake ni miaka 7 jela.

Binadamu aliyegushi vyeti huku akijua, ili ajipatie ajira kwa udanganyifu, huyu ni criminal. Hastahili kupata malipo ya aina yoyote ya kiajira hata kama alikuwa ktk ajira hiyo kwa miaka 20.

Hoja ya msingi ni kwamba hakuwemo kwenye ajira hiyo kihalali na kisheria.Hivyo hana kinga ya aina yoyote ya kisheria kuhusu malipo hayo.

Kilicho halali kwake ni kukamatwa na polisi, kupelekwa mahakamani ili haki ikatendeka huko.Huu ndo ukweli wa kisheria.No more no less.

Jambazi hana haki akikamatwa, na waliogushi vyeti ni majambazi ya ajira, hivyo hawana haki hata kidogo. Ulipwe kiinua mgongo kwa kazi ipi uliyo ifanya wakati uliajiriwa ila kazi hujuwi?
 
Akina Lissu wanawadanganya na kuwapa matumaini feki. Kama KWELI una vyeti feki, basi ukweli wa kisheria ndo huo. Asikudanganye mtu.
 
Hawa enye vyeti feki waiiba fursa za watanzania maskini wenye vyeti safi. Hawa ni watoto wa matajiri,lazima waburuzwe mahakani. We want justice to prevail as well as the rule of law. Wanatibu watu kumbe ni mdaktari feki.Hii ni hatari sana kwa afya za watanzania.
Haha haha Eti "Hawa ni Watoto wa matajiri" acha kujidanganya.

Nakuhakikishia 95% ya Waliomo kwenye Orodha ile ni watoto wa masikini mno na wengine ni wazazi ambao walikuwa wanakaribia kustaafu ili wapate viinua mgongo angalau wajenge nyumba za kuishi. (HILO NINAKUHAKIKISHIA).
 
Back
Top Bottom