Taarab ZIMEPOTOSHWA au kulikoni?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Sehemu kuwa ya nyimbo za Taarabu siku hizi zimetawaliwa na KUSEMANA, KUGOMBANA, KUSUTANA, na MAJIGAMBO.
Hivi kweli hilo ndilo kusudi haswa la taarabu au fani hii inapotoshwa?
 
Sehemu kuwa ya nyimbo za Taarabu siku hizi zimetawaliwa na KUSEMANA, KUGOMBANA, KUSUTANA, na MAJIGAMBO.
Hivi kweli hilo ndilo kusudi haswa la taarabu au fani hii inapotoshwa?

Taarabu siku zote ni MATUSI mtindo mmoja.
Hata mwanajamii Star analijua hilo.
 
Taarabu ni aina ya ngonjera iliyo katika nyimbo. Ndo maana unakuta vikundi mbalimbali vikijibizana katika mada mbalimbali tena kwa lugha ya kimafumbo. Kumbe taarabu kwa yenyewe ilipaswa kuwa na mada mbalimbali kama tulizonazo hapa JF (uchumi, siasa, elimu, lugha, mapenzi, nk). Lakini kwa bahati mbaya watunzi wa nyimbo hizo wamejikita zaidi katika uwanja mmoja: wa mapenzi. Hawana habari na mada zingine.
Kumbe kama ni kuharibu ni hapo kwenye mada. Lingine ni lugha. Wakati mwingine wanatumia lugha kali mno, lugha ya matusi.

Kumbe watunzi wakiweza kupanua wigo wa mada na kutumia lugha ya mafumbo lakini isiyo na ukakasi, naamini muziki huu utakuwa na manufaa makubwa kwa jamii yetu. Sikiliza kwa mfano nyimbo za bibi Kidude ni nzuri sana.
 
ni kawaida ya sanaa yoyote kuburudisha,kukosoa na kufundisha,taarabu iwe ya kisasa au ile ya zamani ni sanaa inyofanya hivyo ila taadhira ndyo inayoharibu ujumbe na maudhui yaliyomo kwenye nyimbo za taarabu,kwa mfano haya yanapotoshwa mno sehemu za uswazi kwani ni vigumu mno kwao kutafsiri mashairi ya wimbo husika,mbona hata muziki wa dansi kama vile msondo na sikinde walikuwa hivyo hivyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom