Taaluma za kuheshimika na muhimu ni hizi sita (6) tu

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Si zaidi ya hapo; ni kama ifuatavyo:-

1. Mwalimu

Waelimishaji waliohitimu kwa viwango stahiki wanahitajika sana, na ikiwa utahitaji kujenga jamii imara walimu ni kundi muhimu na la lazima.

Ili vijana waweze kubadilisha ulimwengu na taifa, basi hii ndiyo taaluma ya muhimu na ya lazima popote pale duniani.

Taaluma hii ni kongwe na ya kuheshimika tangu dahari...kwenye dini zote walimu wanatajwa sana kwa sababu mchango wao uko dhahiri kwenye elimu ya kiroho na dunia.

2. Wanasheria

Wataalamu wa sheria husaidia kuhifadhi na kuzingatia utawala wa sheria. Hii ni taaluma adhimu na ya kuvutia, lakini yenye majukumu machache na muhimu mnoo.

Hawa huamua taabu ya jamii na raha ya jamii.

Fikiria unakabiliwa na kesi nzito na mwanasheria ndiye mtu pekee unaemtegemea kukubeba, utanielewa nasema nini.

3. Maafisa wa Polisi na Wanajeshi

Jukumu la usalama wa raia ni wito wa heshima. Maafisa wa polisi na jeshi daima wanapaswa kuwa tayari na kutarajia yasiyotarajiwa. Wanapaswa kuwa tayari kiakili, kihisia na kimwili kuwatumikia na kuwalinda wananchi dhidi ya wahalifu waovu, mara nyingi wakiweka maisha yao kwenye mstari mdogo sana unaotenganisha salama na hatari.

Kazi wanayofanya inahusisha ujuzi mkubwa. Iwe wanashika doria mitaani au wanafanya kazi ofisini, kazi wanayofanya ni muhimu sana kwa jamii. Wanalinda uhuru na kuzingatia sheria, wanahakikisha haki na kulinda maisha huku wakiweka amani na kuweka usalama wako mbele/ mfikirie mjeda aliepo DRC kulinda usalama wa ukanda huu wote, mfikirie polisi aliepo lindo.

4. Wahandisi

Katika msingi wake, uhandisi ni sayansi katika huduma ya ubunifu. Wataalamu hawa ni watu wenye tija na wa vitendo ambao hutatua shida muhimu kwa jamii.

Mhandisi hawezi kufukia makosa yake ndani ya mchanga wao ni wajenzi huru wa dunia hii....bila wao mambo mengi halisi unayoyaona ya kimiundombinu yasingekuwepo

Kuna nyanja nyingi sana ambazo wahandisi wanaweza kung'aa na kubadilisha ulimwengu, kama vile kudhibiti na kuzuia uchafuzi wa mazingira, kutengeneza dawa mpya, kuchunguza na kuunda teknolojia za hali ya juu. Ni taaluma ya kusisimua.

Hii ndiyo taaluma iliyomtambulisha binadamu ktk mfano wa Muumba wake, fikiria hao wahandisi waliohenga MAPIRAMIDI ya mafirauni huko Masri. Hawa jamaa ni watu wa kuheshimika mno.

Ulishajiuliza jinsi ghorofa refu sana linavyoelea huko angani!? Fikiria daraja la baharini la kilometres 30 au barabara ya chini ya bahari.

Fikiria elopleni inayobeba watu 500 na kuruka nao salama salmini hadi upande wa pili wa mbali sana wa dunia kwa muda mfupi sana.

Hii ndiyo taaluma ya kustaajabisha sana ilomtofautisha binadamu na wanyama.

Narudi kumalizia chaji imeisha nipo julianna hapa nakunywa soda
 
Yaani umeweka hizo ila umesahau taaluma ya muhimu kuliko zote"udaktari"

Sent using Jamii Forums mobile app
Toa polisi na uanajeshi, weka udaktari kwa hiyo short list yako.Hakuna taaluma kwenye fani hizo mbili, hata bila kwenda shule you can fit. Wale watoto wanao ingizwa kupigana vitani umewafunza? Wale polisi wa f4f kuna ujuzi utamfundisha akauelewe?
 
Ni 4 tu hizi hapa

IMG-20211107-WA0006.jpg
 
Kila taaluma ina umuhimu na hakuna taaluma Bora kuliko nyingine zote ziko sawa na muhimu maana taaluma zinategemeana
Nakazia

Kila Mmoja Ni Muhimu Mkata Mkaa Ana Umuhimu Wake, Fundi Baiskeli Huwezi Kujua Umuhimu Wake Isipokuwa Wenye Baiskeli

Kwaujumla Umuhimu Wa Wote Hao Popote Walipo Ndiyo Tunapata Maendeleo Ya Taifa Lote
 
Mbona polis tunawatukana tu kila siku

Kwenye mitandao lakini usije kuwajaribu live utarud na meno umeshika mkononi nyumban kwenu
 
tafsiri na ukalimani ndio ya kwanza na muhimu kushinda hizo, maana maarifa yote yanayopatikana katita taaluma hizo ulizotaja yamehawilishwa
 
Si zaidi ya hapo; ni kama ifuatavyo:-

1. Mwalimu

Waelimishaji waliohitimu kwa viwango stahiki wanahitajika sana, na ikiwa utahitaji kujenga jamii imara walimu ni kundi muhimu na la lazima.

Ili vijana waweze kubadilisha ulimwengu na taifa, basi hii ndiyo taaluma ya muhimu na ya lazima popote pale duniani.

Taaluma hii ni kongwe na ya kuheshimika tangu dahari...kwenye dini zote walimu wanatajwa sana kwa sababu mchango wao uko dhahiri kwenye elimu ya kiroho na dunia.

2. Wanasheria

Wataalamu wa sheria husaidia kuhifadhi na kuzingatia utawala wa sheria. Hii ni taaluma adhimu na ya kuvutia, lakini yenye majukumu machache na muhimu mnoo.

Hawa huamua taabu ya jamii na raha ya jamii.

Fikiria unakabiliwa na kesi nzito na mwanasheria ndiye mtu pekee unaemtegemea kukubeba, utanielewa nasema nini.

3. Maafisa wa Polisi na Wanajeshi

Jukumu la usalama wa raia ni wito wa heshima. Maafisa wa polisi na jeshi daima wanapaswa kuwa tayari na kutarajia yasiyotarajiwa. Wanapaswa kuwa tayari kiakili, kihisia na kimwili kuwatumikia na kuwalinda wananchi dhidi ya wahalifu waovu, mara nyingi wakiweka maisha yao kwenye mstari mdogo sana unaotenganisha salama na hatari.

Kazi wanayofanya inahusisha ujuzi mkubwa. Iwe wanashika doria mitaani au wanafanya kazi ofisini, kazi wanayofanya ni muhimu sana kwa jamii. Wanalinda uhuru na kuzingatia sheria, wanahakikisha haki na kulinda maisha huku wakiweka amani na kuweka usalama wako mbele/ mfikirie mjeda aliepo DRC kulinda usalama wa ukanda huu wote, mfikirie polisi aliepo lindo.

4. Wahandisi

Katika msingi wake, uhandisi ni sayansi katika huduma ya ubunifu. Wataalamu hawa ni watu wenye tija na wa vitendo ambao hutatua shida muhimu kwa jamii.

Mhandisi hawezi kufukia makosa yake ndani ya mchanga wao ni wajenzi huru wa dunia hii....bila wao mambo mengi halisi unayoyaona ya kimiundombinu yasingekuwepo

Kuna nyanja nyingi sana ambazo wahandisi wanaweza kung'aa na kubadilisha ulimwengu, kama vile kudhibiti na kuzuia uchafuzi wa mazingira, kutengeneza dawa mpya, kuchunguza na kuunda teknolojia za hali ya juu. Ni taaluma ya kusisimua.

Hii ndiyo taaluma iliyomtambulisha binadamu ktk mfano wa Muumba wake...fikiria hao wahandisi waliohenga MAPIRAMIDI ya mafirauni huko Masri. Hawa jamaa ni watu wa kuheshimika mno.

Ulishajiuliza jinsi ghorofa refu sana linavyoelea huko angani!? Fikiria daraja la baharini la kilometres 30 au barabara ya chini ya bahari.

Fikiria elopleni inayobeba watu 500 na kuruka nao salama salmini hadi upande wa pili wa mbali sana wa dunia kwa muda mfupi sana.

Hii ndiyo taaluma ya kustaajabisha sana ilomtofautisha binadamu na wanyama.

Narudi kumalizia chaji imeisha nipo julianna hapa nakunywa soda
Anhaa kumbe akili za juliana ndiyo zinaongea😂😂
 
Kwa hiyo wengine hawaheshimiki, daktari haheshimiki, rubani haheshimiki, mchumi haheshimiki, mhasibu haheshimiki......hizi bange huwa mnavutia wapi?
 
Back
Top Bottom