Taaluma ya Ualimu

Opportunist

Member
Mar 19, 2009
17
12
Mwenzenu huwa natatizwa na Selection ya Form IV kwenda Form V, Vyuo nk. Huwa inakuwaje waliofaulu vizuri wanaenda A-Level, vyuo vizuri nk, lakini wale wa karibu na kufeli kabisa kama Div IV.28 hivi ndo wanaopelekwa ktk kozi za Ualimu, tunategemea nini kwa watoto wetu mashuleni wanapofundishwa na 'failures'? Nisaidieni
 
mwenzenu huwa natatizwa na selection ya form iv kwenda form v, vyuo nk. Huwa inakuwaje waliofaulu vizuri wanaenda a-level, vyuo vizuri nk, lakini wale wa karibu na kufeli kabisa kama div iv.28 hivi ndo wanaopelekwa ktk kozi za ualimu, tunategemea nini kwa watoto wetu mashuleni wanapofundishwa na 'failures'? Nisaidieni
walio feli ni division 0 sio 1v.
 
ualimu ni wito bwan mkubwa............... sio profession.................

ahah.......... ndiyo TZ bwana mkubwa........... hushangai mwalimu akipata degree anahamishiwa kufundisha high school???............. as if shule za o/levela ama za msingi hazitahili walimu wenye degree!!!!........... wakati hata chekechea zinataka wenye degree!!!!!!!!.... tanzania ya kushangaza mbona meng tu?????.............
 
its all going down to payment, taalima ya ualimu ktk nchi ii hailipi ndio mana watu wanaikimbia so wanaenda wale ambao hawana alternative, itaheshimika tu pale maslai ya walimu yatapokua kama ya mfanyakazi mwingine then watu automatic watataka kwenda uko bla bla za kusema wito cjui nini haitasaidia, wito uo uwe kwa walimu tu, mbona mtoto wake hapandi basi bure, mbona akiumwa hapati preference kwa kua ni mwalimu! acheni nyie! kwa kifupi walimu wengi wa sasa ivi ni wale waliokosa alternative na wanatafuta pa kutokea
 
Bado hatujawa na sera nzuri kuhusu elimu. Sekta ya elimu kwa ujumla wake ina matatizo lukuki. Kila ngazi kuanzia vidudu mpaka vyuo...ni kuzima moto mtindo mmoja. Takwimu zinaonyesha kudrop kwa kiwango cha elimu....but who cares?

Yangewekwa mazingira mazuri ya kazi kwa waalimu (resources: salary,incentives,offices nzuri kama za mabenki!) hata hao wa Div One wangeona ni ujiko kwenda ualimu.

Inahitakija nia ya kisiasa ni si kuuza maneno........still far from dreams!
 
Mwenzenu huwa natatizwa na Selection ya Form IV kwenda Form V, Vyuo nk. Huwa inakuwaje waliofaulu vizuri wanaenda A-Level, vyuo vizuri nk, lakini wale wa karibu na kufeli kabisa kama Div IV.28 hivi ndo wanaopelekwa ktk kozi za Ualimu, tunategemea nini kwa watoto wetu mashuleni wanapofundishwa na 'failures'? Nisaidieni

Ualimu ni wito,je wewe binafsi au mwanao akipata div 1 f6 let say pcb,utampeleka UD akasomee ualimu wa biology,chem??
 
du, we ulikuwa hujui kuwa taaluma hiyo ndiyo imepewa nafasi ya mwisho bila ya kufahamu kuwa huko ndiko kunakopikwa maofisa na maprofesa. nahisi tunaandaa vihiyo
 
Back
Top Bottom