Taabu ya kuipenda Yanga na Kuchukia ufisadi(Yusuph Manji---Yanga)

chidide

Member
Nov 11, 2010
91
9
Mimi ni mwana jangwani mzuri sana, toka nina umri wa miaka minne. Sasa nina miaka 36 still naipenda Yanga sana. Kuna wakati naamua kuacha kuifuatilia but unakuta nashindwa kufanya hivyo. Sasa kuna huyu mfadhili wetu Yusuph Manji toka aje ameisaidia sana Yanga hilo halina ubishi. But at the same time amehusishwa na ufisadi mwingi unaotokea TZ. Sasa inasemekana anaanzisha chombo cha habari kwa ajili ya uchaguzi wa 2015 na ameanza na gazeti letu la Yanga Imara.
Sasa sisi washabiki wa Yanga ambao tupo kwenye upande wa wapinga ufisadi inatupa shida sana kwa sababu siamini katika msemo wa "baniani mbaya kiatu chake dawa". Naomba wapenzi wa Yanga ambao ni wachambuzi wa habari za siasa wachangie katika hili.
 
Njaa mbaya sana ndugu yangu.
Hauna jinsi kwani pesa zake unazihitaji lakini ufisadi wake unakukera.
Kubali tu huo msemo wa wahenga ndugu yangu.
 
...na tayari ameishaanza Msimu wa kuwapelekesha viongozi hapo jangwani sasa hivi....!
 
Mimi nilikuwa naipenda sana Yanga, lakini baada ya kuingia huyu Bwana mdogo na kujifanya mfadhili mimi nimeacha kuipenda Yanga, hata mpirani siendi. NAIPENDA TANZANIA ZAIDI YA YANGA. Kwanza kwa wachunguzi wa masuala huyu jamaa ana malengo yake tu Yanga, na sio mapenzi. Anataka huruma ya wana Yanga ili afiche ufisadi wake. JAMANI WA TZ TUMPENDE MAMA YETU TZ ZAIDI YA YANGA. TUMFUKUZE HUYO JAMAA. Tajiri na mali yake, masikini na mtoto. Walikuja wengi wakapita Yanga itasimama tu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Back
Top Bottom