TAA uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jioni hii ni aibu

Atclkwanza

JF-Expert Member
Dec 20, 2015
823
998
Muda huu naenda mwanza Security machine kwenye cheki point inatumika moja tu zingine hazina wafanyakazi ni usumbufu mkubwa, mnamwangusha Mbarawa acheni kufanya kazi kwa mazoea,Naomba wahusika wahojiwe kuna kitu gani mnataka kupitisha kwa magendo.

Badilikeni bwana.
 
Mbarawa kwa vile ni muislam mpemba ni mpole sana, by the way ngoja nimstue mdau pale atupe uhakika barafu
 
..ukienda kwenye TOILET za airport zetu utaona aibu.

..Hicho ndicho choo cha kwanza anachotumia mgeni mara baada ya kutua Tz.

..sasa waTz tujue kumbukumbu tunayowapa wageni wanaokuja Tz.

..kuna mtu aliniambia kuwa bad customer experience hutangazwa zaidi kuliko good customer experience.
 
Mola atusaidie tubadilike!
Nina Imani tutafika tu!
 
..ukienda kwenye TOILET za airport zetu utaona aibu.

..Hicho ndicho choo cha kwanza anachotumia mgeni mara baada ya kutua Tz.

..sasa waTz tujue kumbukumbu tunayowapa wageni wanaokuja Tz.

..kuna mtu aliniambia kuwa bad customer experience hutangazwa zaidi kuliko good customer experience.
Na wale madogo wasafisha vyoo wanavyopigaga mizinga kama wametumwa
 
Yaani wanasubiri tamko na ziara za kushtukizwa. Tanzania kweli tunailaza usingizi wa pono
 
Hii kitu ningekuwa DAR, ningetua AIRPORT na kupiga makelele hovyo huku nikilia kama yule shabiki wa Yanga, "RAIS MAGUFULI TUNAIBIWA na blah blah kibao" uone kama sitatolewa magazetini, video youtube zisambae mpaka zimfikie mkulu ntauaga umaskini. Ntapewa kacheo hapo Airport.
 
Back
Top Bottom