igogondwa
JF-Expert Member
- Aug 1, 2021
- 2,590
- 3,346
Maelezo meeengiii utadhani mwalimu wa NIT.... huyo ni mzembe na alipe ili iwe fundisho... Yaani mnataka mpaka kwenye hizo nguzo za taa wazungushie concrete block??Using a free mind, ajali barabarani ni kitu kinaweza kutokea. Namaanisha isitafsirike kuwa aliyegonga amegonga makusudi? Ili apate faida ipi wakati gari lake linaharibika na yeye mwenyewe au waliokuwa ndani ya gari wana risk kifo au ulemavu wa kudumu?
Hiyo ni ajali kama zingine. Jambo moja la kuangalia kwa makini ni kuwa kwanini zimegongwa kipindi hiki?
Ukiangalia utaona barabara imetanuliwa kuanzia morocco kuelekea mwenge, imekuwa pana na nzuri na haina humps bado! Lakini kwa mtu anayetoka Mbuyuni anakuja morocco au kuelekea mwenge ila barabara mpaka hapo morroco ni nyembamba (kulinganisha na mpya ya morroco - Mwenge).
Kwa mtu mgeni wa njia hiyo, hasa usiku mwingi ambao barabara ni nyeupe na hasa kama ametumia vileo au yuko high speed au vyote speed na pombe, kama anatokea mwenge akifika mataa ya morocco kama asipojua kwenye taa hizo anatakiwa akunje kidogo kulia ili aingie barabara nyembamba ya morocco - city center basi anazivaa taa hizo vizuri tu. Drivers wataelewa nasema nini hapa.
Hivyo hiyo ni ajali. Mbona hakugonga zingine zoote alikotoka akaja gonga hapo?