System ikishindwa kuipatia Tanzania Katiba Mpya sasa, miaka michache ijayo tutakuwa Failed State

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
16,862
35,969
Sote tunaona!

Kwa hali ilivyo sasa, endapo hatujapata Katiba Mpya sasa inayowawekea Viongozi wa kisiasa speed governor huku ikiweka nguvu kubwa kwenye mifumo ya nchi kuendesha na kuamua masuala ya msingi kuna wasiwasi mkubwa sana nchi yetu kuenda kuwa failed state miaka michache ijayo.

Kwa sasa Tanzania, Katiba inatamka wazi kuwa Rais hatalazimika kufuata ushauri wa mtu yeyote yule.
Maana ya kipengele hiki ni kwamba mifumo rasmi yote ya nchi iko chini ya Rais na kamwe haiwezi kumlazimisha Rais kufanya lolote lile.

Leo hii ndo mana tunaona kashfa kubwa zikisemwa kuhusu familia ya Rais na hakuna lolote linalofanyika.

Leo hii ndo mana tunaona wanateuliwa watu wasio na uwezo kushika nafasi mbalimbali kwa sababu tu anayeteua ni Rais na hakuna wa kumfanya kitu.

Leo hii ndo mana tunaona Wananchi wanaweza kosa haki zao Mahakamani kwa sababu tu Mahakama haziko huru kuamua kwa sababu kwa upande fulani zimewekwa chini ya huyu anayeitwa Rais.

Leo hii ndo mana tunaona Bunge kutokuwa huru kuamua masuala ya msingi ya nchi kwa sababu tu Katiba imempa nguvu kubwa Rais ambaye ameweza hata kuliweka Bunge mfukoni.

Leo hii tunaona chaguzi zikifanyika kama geresha tu huku maamuzi ya wananchi yakiwa hayaheshimiwi kwa sababu Katiba yetu imetengeneza mtu ambaye hawezi kuhojiwa wala kushtakiwa popote pale. Kila siku wananchi wanazidi kukata tamaa na hii mifumo iliyopo.

Kwa jicho la kawaida tunaweza tusione madhara ya hiki kitu kwa sasa ila kwa jicho la tatu kuna hatari kubwa sana mbeleni.

Kuna maamuzi makubwa ya kitaalam hayafanyiwi kazi kwa sababu tu kuna Mwanasiasa mmoja amepewa nguvu na Katiba iliyopo.

Kuna kipindi kitafika watu wote nchi hii watakata tamaa si watumishi, si wananchi si wakulima si wafanyabiashara si vyombo vya dola. Na hii ndo hatari inayokuja kwa Tanzania.

Kuna muda utafika tutapata wajinga kama watu wenye sauti zaidi na maamuzi zaidi kwenye nchi na wanaweza kufanya maamuzi ambayo sio tu yataiweka nchi yetu pabaya ila yanaweza kutugharimu kwa kiwango kikubwa sana na kuathiri ustawi wa taifa kwa ujumla.

CCM kama CCM hawawezi kukubali kufanya mabadiliko ya hii Katiba iliyopo bila kulazimishwa kuanzia na wananchi na mwisho vyombo vya dola.

It's high time kitu kinachoitwa System kutumia huu mwanya uliopatikana wa Mwanasheria nguli Tundu Antipass Lissu kuwa Mwenyekiti wa Chadema kuifanya agenda hii ya Katiba Mpya kupata nguvu sasa na jambo hili kufanyika wakati huu maana endapo tusipopata Katiba Mpya sasa tunaweza kuja kuipata kipindi ambacho CCM watatuvurugia mchakato mzima na kutuletea Katiba ya hovyo zaidi kuliko hata hii tuliyonayo sasa.


Lord denning
Nairobi
 
I just finished the episode. I usually love MOS but this episode felt quite forced. Kusha definitely took control of the episode and at some point it just felt like this is less about a fun girly podcast and more about Kusha's rumours, mental health and loneliness.


Kodi
 
Back
Top Bottom