Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,007
- 9,873
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema waasi nchini Syria wamewauwa wanajeshi 40 wa serikali na kuwajeruhi wengine zaidi ya 80, katika mashambulizi waliyoyafanya katika jimbo la Idlib.
Shirika la habari la Urusi, Interfax limenukuu tangazo la wizara hiyo, lililosema kuwa waasi walizikamata kambi mbili katika shambulio mojawapo. Shirika la habari la Syria, SANA limearifu kuwa waasi walitumia miripuko ya kutegwa ndani ya magari na silaha nzito nzito katika mashambulizi hayo ya Idlib mapema leo, na kuongeza kuwa jeshi la serikali limepeleka vikosi vya msaada katika jimbo hilo.
Idlib ni jimbo la mwisho linalodhibitiwa na waasi nchini Syria, na mamia kwa maelfu ya raia wamelikimbia mnamo wiki za hivi karibuni, kuepuka mashambulizi yanayofanywa na ndege za Urusi na za serikali ya Syria dhidi ya waasi hao.