Synovet: JamiiForums iliegemea upande wa CHADEMA uchaguzi mkuu 2010

Status
Not open for further replies.

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
Leo jijini Dar pale ubungo plaza,imezinduliwa report juu ya Media monitoring during 2010 election ambapo pamoja na mambo mengine imeeleza kuwa CCM ilipendelewa katika coverage kwenye radio ,tv na magazeti na katika upande wa mitandao wali-monitor Jamii forums na Issa Michuzi blog ambapo imeelezwa kuwa Issa Michuzi alipendelea CCM huku JF ikipendelea chadema.

Kuna mambo mengi yameongelewa lakini kwa ufupi habari ndiyo huyo.

Kwamba TBC 1 na mwananchi viliongoza kwa fair coverage kati ya vyombo 92 vilivyofuatiliwa ikiwemo JF na Issa michuzi

Walikuwepo waandishi kiibao,wawkilishi wa vyama vya siasa akiwemo Tambwe izza,mtatiro, nk

kijumla report hiyo unaweza kuipata hapa

Je, Synovate Tanzania wamesoma Footer ya JF?

jf-chini.jpg

usiku mwema
 
Ahhh!!haya yote ni mapambano ipo siku wananchi tutapata kile tunachokitarajia hasa kwa kuiunga mkono Chadema ambao wameonyesha nia ya dhati kupambana kwa kufichua mabaya yanayofanywa na Serikali hii ya ccm.
 
Kuna vitu vingine havihitaji hata mahesabu sasa kama JF wamejaa wanachama wengi wa CHADEMA unategemea response ya wachangiaji itakuwa upande wa vyama vingine, vyama vingine wakiambiwa wajiunge hapa JF hawataki, halafu uchaguzi umefanyika Oktoba mwaka jana ripoti inakuja kutoka mwezi wa sita mwaka huu
 
Leo jijini Dar pale ubungo plaza,imezinduliwa report juu ya Media monitoring during 2010 election ambapo pamoja na mambo mengine imeeleza kuwa CCM ilipendelewa katika coverage kwenye radio ,tv na magazeti na katika upande wa mitandao wali-monitor Jamii forums na Issa Michuzi blog ambapo imeelezwa kuwa Issa Michuzi alipendelea CCM huku JF ikipendelea chadema.

Kuna mambo mengi yameongelewa lakini kwa ufupi habari ndiyo huyo.

Kwamba TBC 1 na mwananchi viliongoza kwa fair coverage kati ya vyombo 92 vilivyofuatiliwa ikiwemo JF na Issa michuzi

Walikuwepo waandishi kiibao,wawkilishi wa vyama vya siasa akiwemo Tambwe izza,mtatiro, nk

kijumla report hiyo unaweza kuipata hapa

usiku mwema

Na Facebook Iliwapendelea CHADEMA au
 
Kuna vitu vingine havihitaji hata mahesabu sasa kama JF wamejaa wanachama wengi wa CHADEMA unategemea response ya wachangiaji itakuwa upande wa vyama vingine, vyama vingine wakiambiwa wajiunge hapa JF hawataki, halafu uchaguzi umefanyika Oktoba mwaka jana ripoti inakuja kutoka mwezi wa sita mwaka huu

Ningependa kuamini kuwa JF ina wasomi ambao ni wafuatiliaji na wachambuzi wa hoja. Na sote tunajua serikali na ccm (kama chama) vimekuwa vikendeshwa kwa 'mazoea', hakuna ku-hoji kitu hata kama ni madudu matupu. Sasa wasome wameamua kuchambua madudu hayo ndani ya mfumo wa utawala. Kwa hiyo kwa vyovyote vile ccm/serikali haiwezi kufurukuta ndani ya JF kwa sababu hakuna cha maana sana walichokifanya zaidi ya kuonesha ni jinsi gani wamefilisika kimawazo. Kuna uwezekano kabisa humu jamvini wapo wana-ccm waliochoshwa na uburuzwaji wa ccm na wanatumia JF kueleza hisia zao na madudu wanayoyaona yanafanywa na ccm.
 
Hakukuwa na masharti ya kujiunga JF. Hata hao Sinovet nao ni kama NAPE.
Labda tuseme kuwa JF ina wasomi wengi kuliko blog nyingine yoyote hapa nchini. hivyo inakuwa ngumu kwa wasomi kuunga mkono kila kitu kama ccm wanavyotaka, kama vile ndiyo mzee hata kama jambo halina msingi kwa jamii.

Sinovet inatakiwa wajua kwamba JF is the HOME OF GREAT THINKERS. wakijua hilo hakuna haja ya kufanya tafiti.
 
JF siyo kama gazeti au kituo cha runinga. Habari nyingi zinatokana na members na michango yao. Kwa hiyo ni members wa JF waliegamia upande wa Chadema ila huwezi sema JF iliegemea upande wa Chadema. Inaonyesha hawajui forum ni nini na madhumini yake ni nini.
 
Siyo kweli. Statement is wrong

Labda wangesema JF users..... na siyo JF

Uwongo mwingine TBC ilikuwa fair! Ni kweli

Hili shirika siyo credible
 
halafu uchaguzi umefanyika Oktoba mwaka jana ripoti inakuja kutoka mwezi wa sita mwaka huu
Kwa kweli mkuu inaonekana kuwa hatujui kabisa umkuhimu wa timely reports... hata NEC wenyewe juzijuzi tu hapa ndo wamepeleka ripoti ya uchaguzi mkuu wa Kikwete, sijui walikuwaq wanaichakachua!
 
Hawa Synovet, kwa upande wa JF sijui walikuwa wanaangalia topics posted au michango iliyokuwa inachangwa ndani ya post moja. Nitajaribu kujiridhisha kwa kuangalia ripot yao kwa umakini ili isiwe wamekariri maneno ya kina kasesela kuwa JF ilikuwa inaipendelea cdm
 
Hawa synovet si ndio walichakachua matokeo ya kura za maoni kuhusu mgombea anayekubalika zaidi wakatiule wa uchaguzi? Ni wapuuzi tu!
 
Hapana yako mambo ya kuzingatia katika hilo huenda hata jf imeisaidia mpaka hapa tulipo ila jambo la msingi ni wakati wa kwenda na si kurudi
 
waambie watuambie tusichojua... so they wasted donors money to tell them kwamba vijana wengi na wenye upeo na access ya mitandao, umeme na weledi wanaweza kuaccess JF majority yao ni chadema???

Khe khekeheheheeeeeeeeeeeeeeee.... kituko!!

Majority ya vijana na wazee wanaolitakia mema taifa lao hawaridhishwi na CCM na ndio wenye access ya sophisticated facilities

I started as hardcore CCM transformed to soft now i hate CCM to the core
 
JF walitoa uwanja huru ila wana CCM hawakuwa na ubavu wa kutoa maoni humu kutokana na chama chao kujaa uozo, mbona malaria sugu tunaye siku zote wengine pengine wanaogopa, TBC haikuwa fair asilani, pamoja na radio ya bongo fleva cloudsfm
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom