Synovate wamejitakia wenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Synovate wamejitakia wenyewe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Njilembera, Sep 22, 2010.

 1. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Vuguvugu la uchaguzi nchini Tanzania limechochewa sana na ujio wa Dr Slaa katika ulingo wa kugombea kiti cha uraisi. Kila kona ya nchi na gazeti habari ni Slaa Vs Kikwete. Ingalitegemewa kampuni yenye hadhi kama Synovate ingeanzia utafiti wake kwa kuthibitisha kweli Slaa ni kichochozi katika kinyangiro cha uchaguzi huu au sivyo. Kinyume chake Synovate wakachapisha eti ni gazeti lipi linachapisha habari bila kuegemea chapa fulani. Bila shaka hawakutoa kipaumbele pale palipokuwa panastahili, na ni kwa nini wakafanya hivyo?

  Kutoa kipaumbele kwa magazeti? Hapana hawakufanya hivyo, waliangalia joto la siasa na hasa upande wa CCM, LAKINI iliwabidi watoe taarifa kama alivyodai CEO wao, mteja wao alitaka taaarifa kila quarter. Basi ilimradi atoe chochote akatoa ya magazeti.

  Hata kama ingekuwa mgombea wa CCM ndiye mwenye mvuto kuliko wa CHADEMA, bila shaka CCM wangelalamika mbona Synovate hamzungumzii umaarufu wa mgombea wetu, mnazungumzia utendaji wa magazeti?

  Hivyo Synovate wamejitakia wenyewe kushutumiwa na bora wakae kimya! Huo umaarufu wao ni sifuri na sidhani kama tunauhitaji tena. Tena napata wasiwasi CEO wao anadai anatekeleza maagizo ya mteja wao, ni nani mteja wa Synovate? Ni Serikali au ni CCM au ni vyote kwa pamoja? Je Synovate ni mgando kiasi hajui CCM ni vigumu wao kujiona sio serikali kama vile Serikali isivyoweza kujiona kuwa sio CCM?
   
Loading...