Synovate walilipwa na ikulu kufanya utafiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Synovate walilipwa na ikulu kufanya utafiti

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Oct 17, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  KILE kinachoitwa umaarufu wa Jakaya Kikwete, mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeelezwa kuwa ni “taarifa za kupanga” za asasi zinazoendesha kura ya maoni, MwanaHALISI limeelezwa.

  Kwa mujibu wa uchunguzi, asasi zilizotoa taarifa za umaarufu wa wagombea urais nchini, zina uhusiano wa karibu na ikulu, kampuni ya Synovate imekuwa na uhusiano wa kibiashara na ikulu.

  Gazeti la hili linazo nyaraka mbili zinaonyesha kuwapo kwa mahusiano ya karibu, ya kibiashara na kibinafsi, kati ya ikulu na kampuni ya Synovate.

  Mahusiano hayo yameonekana katika madokezo kadhaa yaliyotoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu kwenda kwa katibu wa rais, mwenyekiti wa bodi ya tenda ya ikulu na mkuu wa shughuli za ikulu (Mnikulu).

  Rweyemamu katika maelezo yake anasema, tayari amefanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Synovate Tanzania (zamani ikiitwa Steadman Group) na kukubaliana kufanya kazi ya kitafiti.

  Rweyemamu amemthibitishia katibu wa rais katika dokezo lake, kwamba kinachotakiwa na ikulu ndicho kitatekelezwa na uongozi wa Synovate, na kwamba baadhi ya huduma hizo watazipata bila kulipia chochote.

  Kuvuja kwa taarifa za kuwapo kwa mawasiliamo ya kibiashara na binafsi kati ya serikali na Synovate kulikuja siku tatu baada ya kampuni hiyo kutoa kile ilichoita, “Ripoti ya utafiti wa kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.”

  Katika moja ya madokezo, kutoka kwa Rweyemamu kwenda kwa katibu wa rais, mapema mwaka huu, mkurugenzi huyo wa mawasiliano anaithibitishia ofisi ya rais, kuwa tayari amefanya majadiliano na watendaji wakuu wa Synovate, na kuahidi kutekeleza kile ambacho ikulu inataka.

  Rweyemamu anataka Synovate iwaandalie kura ya maoni. Aidha, Rweyemamu anataka kampuni hiyo ieleze kuhusu “nguvu ya vyombo vya habari nchini kwa sasa kutokana na utafiti wao ambao unaonyesha ni chombo kipi kina nguvu ipi na katika maeneo yapi ya nchi au makundi gani ya wananchi.”

  Anasema tafiti hizo ni nyenzo muhimu kwao hasa kutokana na kujiandaa na matukio yajayo. Hakuyataja matukio hayo.

  Mkurugenzi huyo wa mawasiliano ya rais anasema amethibitishiwa na Synovate kwamba “presentation ya kura ya maoni tutaipata bure, lakini ile ya vyombo vya habari tutalazimika kulipia kama tunahitaji kupata ripoti kamili. Nitakujulisha gharama zao baada ya kuwa nimezungumza nao kwa kina.”

  Akisisitiza kuwa hakuna mabadiliko ambayo yatatokea, Rweyemamu anasema, “Nakuomba kama unaweza kuwaarifu maofisa wengine wa OBR – ofisi binafsi ya rais – ambao wako Dar es Salaam kuja kushiriki nasi katika kuona presentations hizo kuanzia saa tisa mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais.”
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mwaka huu hata CCM wafurukute vipi kila kona wamebanwa kisawasawa!
   
 3. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Some of us already smelt a rat and this revelation confirms everything...Hawa jamaa wa SYNOVATE bwana! Wapo hapa kuchakachua demokrasia yetu
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  of course.. ndio maana walikuwa na ujasiri wa kuja juu kwanini haikuwa asilimia 88 kama walivyotarajia (ahidiwa??)
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Very fun, Kinana alitegemea Synovate watasema asilimia 88 kama walivyokubaliana (terms) badala yake wakasema 61, basi huu ni ujuha wanadanganyana wao kwa wao.
   
 6. u

  urasa JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dawa ni kuwapa matokeo ya poll of polls
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kama SYNOVATE walilipwa na ikulu kufanya tafiti na tehm do that. hii ni doa baya sana kwa utakatifu wa IKULU yetu.

  Napata hisia kwamba watahairia uchaguzi kama alivyodadaiza Mwanakijiji. dalili zipo wazi wameelemewa. Ila wakihairisha ndo wanajichimbia kaburi zaidi maana upinzani pia itajipanga vyema zaidi na jamii itahamasika na kuhamanika na hii trick.
   
 8. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  CCM chama kizuri kabisa... stracture, idiology etc .... but Human value is ZERO... Hakina Uongozi ila Uhuni, Mizingwe and Maximum Corrupted - In that case kimekufa hakiko hai...! Ni jeneza la Maiti ....anybody dare to challenge THIS?
   
 9. e

  ejogo JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  I see!
   
 10. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  .....mwahahalisi ya tarehe ngapi hiyo?
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  .

  mfa maji haachi kutapatapa.
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mwanahalisi wanaokota taarifa hata bila utafiki, si vema kuamini taarifa zao bila uchambuzi wa kina.
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  watafiti wa TCIB walilipwa na nani ?.....Mwanahalisi? maanake umetoa ushindi kwa Dr Slaa
   
 14. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama Mwanahalisi wanachakachua habari si wapelekwe mahakamani?
   
 15. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  I smell something fish here. ule mpango wa kuiba kura ni kitu kinachoandaliwa uwalalishaji.wakishindwa kabisa watamtumia NEC kufikia nia yao.Nawatahadhalisha CCM wasijaribu kutekeleza adhima hiyo maana shingo wa kuku wengine zitakua halali ....
   
 16. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  huna lolote km avator yako
   
 17. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwani Synovate sio jamaa wa Kenya? na Kilonzo alipokuja juzi amesemaje? si yaleyale? Upupu huu unaofanywa na CCM ni kihoro tu kimebakia kabla ya kufwa...CCM Mtatumia nguvu za kiza nazo zitakwama.

  Huyo mungiki huyo amekuja anasema JK bado anahitajika na EAComunity, akafilie mbali, Watanzania ni zaidi ya EAC, bila watanzania hakuna EAC na kama Tanzania haina kiongozi makini hata hiyo EAC ni hewa chafu kwetu, maana tumeshaona ni kiasi gani jamaa toka huko Ke na Ug wanavyojichotea kazi ktk shirikisho, Arusha just because wanakumbuka tu kuusema lugha ya wazungu..Kikwete anashangilia kupigiwa debe na Kilonzo, hajajua kuwa wanamuona uchochoro wao! Akienda Dr Slaa nani anasema naye uchafu bila logic?? Ndio maana hofu imewajaa akina Kilonzo! Na akome!
   
 18. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2015
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,227
  Likes Received: 1,154
  Trophy Points: 280
  Kweli hizi taasisi njaa ni hatari kwa afya ya Maendeleo ya Jamii.
  Pamoja na madudu yote ya CCM badala ya asilimia kushuka yao inapanda !


   
 19. jogoo_dume

  jogoo_dume JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2015
  Joined: Oct 20, 2014
  Messages: 584
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Somebody had to pay them, excuse me!!
   
 20. a

  anophelesi JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2015
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 614
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 80
  Wapeleke huo utafiti gazeti la
  UHURU, J
  AMBO LEO,
  HABARI LEO,
  TBC
  CLOUDS
  STARTV,
  Hao ndio wanashida na tafiti hizo.
   
Loading...