SYNOVATE : Mambo mbofu mbofu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SYNOVATE : Mambo mbofu mbofu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyumbu-, Dec 28, 2010.

 1. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Kama kawaida, ukiacha taaluma yako na kuingiza uhuni kwenye kazi ujue mwisho wako ni wa aibu tu. Haingii akilini tasisi kama Synovate kukosa Tzs.75M wakati inapata support ya michango kutoka kwa wasamaria, donors na kutoka biashara yao wenyewe.
  Soma hii hapa :

  Synovate kwafuka moto


  na Ratifa Baranyikwa


  [​IMG] TAASISI ya Synovate, inayojishughulisha na masuala ya utafiti na masoko, imedaiwa kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake.
  Wafanyakazi wanaoidai taasisi hiyo ni wale wanaofanya kazi kwa mkataba maalumu ambao ni takriban 126 na kiasi wanachodai ni karibu sh milioni 75. Akizungumza na gazeti hili jana mmoja wa watendaji wa taasisi hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema wafanyakazi wanaodai ni wale waliokuwa wakiendesha tafiti za Synovate katika mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha.

  Alisema utafiti waliokuwa wakiuendesha ni ule ambao Synovate iliingia mkataba na Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusu wafanyabiashara wa kati jinsi wanayoweza kuchangia pato la taifa. Mtoa taarifa wetu huyo alidai kuwa, Wizara ya Viwanda na Biashara ilikwishailipa fedha Synovate na kwamba wafanyakazi hao walikwishakamilisha kazi yao tangu mwezi Septemba mwaka huu.

  Kutokana na hilo, hivi majuzi wafanyakazi hao walikutana kwenye ofisi za Synovate na kufanya mkutano wakiomba kukutana na meneja wa taasisi hiyo kudai malipo yao, hali ambayo ilizusha mzozo mkubwa.
  Mzozo huo uliibuka baada ya meneja huyo wa Synovate tawi la Tanzania, Aggrey Owino, kutamka kuwa ofisi haina hela na kuwataka wafanyakazi hao wakubali kugawana kiasi cha sh milioni kumi zilizopo kwa kila mmoja kupata kiasi cha laki na nusu.
  Wafanyakazi hao ambao kila mmoja anadai kiwango chake kulingana na kazi aliyopangiwa, walikataa kugawana fedha hizo, kwa maelezo kuwa kiasi hicho ni kidogo kwani hakifiki hata nusu ya madai yao. Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wafanyakazi hao alisema kuwa kutaaa kwao fedha hizo kulimlazimu meneja huyo kuwalipa watu 16 tu madai yao yote badala ya kuwalipa wote kidogo kidogo.

  “Hivyo kiasi kulichobaki ambacho taasisi inadaiwa ni shilingi milioni 65 na sisi tumewaambia hatuwezi kukubali kulipwa kidogo, wakitaka watulipe zote ingawa meneja alitoa kauli ya kejeli kwamba ambaye hataki aondoke…lakini watu waligoma, ” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
  Wafanyakazi hao pia katika suala la kudai malipo wanasema hii si mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kuwanyanyasa wafanyakazi wake.
  Gazeti hili lilipomtafuta Owino ofisini kwake kuzungumzia suala hili, mwandishi alielezwa kuwa hayuko nchini amekwenda kwao Kenya kwa ajili ya sikukuu za Krismasi.
  Taasisi ya Synovate ni moja kati ya taasisi ambazo zimekuwa zikiendesha tafiti mbalimbali hapa nchini.
  Moja ya tafiti ambazo zilizua maneno ni ule wa kura za maoni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ambapo utafiti wake ulionyesha kuwa mgombea wa urais wakati huo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, alikuwa anaongoza kwa asilimia 61. Wakati Dk. Willbrod Slaa aliambulia asilimia 16, Profesa Lipumba asilimia (5) na wagombea urais wengine asilimia 5.
   
Loading...